Mhashamu Methodius Kilaini ahamishiwa Jimbo la Bukoba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhashamu Methodius Kilaini ahamishiwa Jimbo la Bukoba

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Ng'wanza Madaso, Dec 6, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na Mwandishi wetu
  6th December 2009


  [​IMG]
  Mhashamu Methodius Kilaini

  Baba Mtakatifu, Benedicto wa 16, amemhamisha Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini, kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba.

  Taarifa za uhamisho huo, zilitangazwa jana na Balozi wa Baba Mtakatifu nchini, kupitia taarifa ya Sekretarieti ya Kanisa hilo, iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

  Taarifa hiyo imesainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padre Anthony Makunde.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Askofu Kilaini, ambaye amekuwa akimsaidia Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa miaka mingi, ameruhusiwa kuendelea kushika Kiti cha Jimbo la Strumnizza.

  “Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania anayoheshima kutaarifu kwamba Baba Mtakatifu Benedikto wa Kumi na Sita amemhamisha Baba Askofu Methodius Kilaini kutoka katika ofisi ya Askofu Msaidizi wa Dar es Salaam kwenda kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba akimruhusu kushika Kiti cha Jimbo la Strumnizza,” ilieleza taarifa hiyo.

  Aliteuliwa kushika nafasi ya Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Baba Mtakatifu, Yohane Paulo wa Pili.

  Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, Kilaini aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), kuanzia mwaka 1991.


  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hii ni promotion ay Demotion?
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hii ni promotion au Demotion?
   
 4. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nina jiuliza kitu kimoja kwa nini hakupewa u Archbishop wa Mwanza? kapelekwa Bukoba kama Askofu msaidizi je anamsaidia nani? Kwa heshima kubwa aliyokuwa nayo pale Dar halafu anahamishiwa Bukoba kama Askofu msaidizi naona ni kama Demotion vile.
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Jamani haya ni mambo ya RC wengine hatujui, huwezi kutamatisha kwamba ni demotion, Je? unaelewa maana ya neno hili? Strumnizza
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Ndio mjue kuwa vyeo vya kanisa siyo kama vya siasa.Ni utumishi na unaweza kupelekwa popote. Mbona hata jimbo la Same liko wazi na hajapelekwa huko.
  Huenda uzoefu na umahiri wake unatakikana Bukoba zaidi ya PENGINE.
   
 7. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ohhh jamaniiiiiiiii!! Tutakumiss daima katika jimbo hili la Dar.
   
 8. P

  Paschal Matubi Member

  #8
  Dec 7, 2009
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Strumnizza ndilo jimbo lake liko Bulgaria. Linatiwa Titular Diocese. Kila askofu wa kanisa Katoliki ana jimbo.

  Hata Poplycarp Pengo alihamishwa toka Tunduru-Masasi kama askofu wa Jimbo hilo na kwenda kuwa msaidizi wa Jimbo la D'Salaam lilikuwa chini ya Kadinali Laurian Rugambwa. Haikuwa demotion. Aliyesema kwamba msifananishe vyeo vya kanisa na siasa alikuwa sahihi kabisa.

  Na ndiyo maana hukohuko kwenye siasa unaweza kutumia mbinu ya wanamtandao ukaeneza propaganda kwamba hakuna ufisadi wa RICHMOND au ukawashinda wapinga ufisadi kama kina Mwakyembe, Sitta au Kilango.

  Lakini ukileta uana-mtandao wako kujifanya kulipinga kanisa Katoliki eti kwa ajili ya waraka basi utanywea mwenyewe na hutatamani kuongea tena habari za waraka wa kanisa katoliki. Muulize Kingunge aalivyokemewa na Pengo kwamba msiwafundishe maaskofu kuandika barua za kichungaji.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,388
  Trophy Points: 280
  nadhani ni lateral move; sijui kama anahamishiwa bukoba akiwa na haki ya kulirithi Jimbo..
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nini maana ya Mhashamu?

  Nini maana ya Kardinali?

  Ipi cheo kikubwa katika hizo (elimu tu tafadhali)
   
 11. P

  Paschal Matubi Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Askofu mwenye haki ya kurithi jimbo huitwa Coadjutor Bishop au askofu mwandamizi. Kabla ya mwaka 1988 Polycarp Pengo alikuwa askofu wa jimbo Tunduru-Masasi. Mwaka huo akapelekwa D'Salaam kuwa askofu msaidizi wa D'Salaam na hivyo Dar ikawa na maaskofu wawili. yaani Rugambwa akisaidiwa na Pengo aliyeliacha jimbo lake la Tunduru-Masasi

  Lakini kwa usahihi zaidi ni kwamba Pengo wakati ule alienda kama Coadjutor Bishop (mwandamizi) na si kama Auxiliary Bishop. Hivyo wakati wowote wa kuondoka kwa Rugambwa basi Pengo angerithi. Na ndivyo ilivyotokea mwaka 1992 siku alipostaafu Rugambwa.

  Maaskofu waliowahi kupata bahati ya kuwa Coadjutor ni Pengo na Tarcius Ngalalekumtwa wa Sumbawanga. Lakini wakati Ngalaekumtwa aakiwa Coadjutor ghafla akahitajika Iringa kama Kilaini alivyohaimishiwa Bukoba japo Kilaini ni msaidizi. Na hiyo ikamfanya Ngalalekumtwa awe askofu wa Iringa hadi leo.

  Askofu Msakila angefariki mapema kabla Ngalalekumtwa hajahamishiwa Iringa basi moja kwa moja Ngalalekumtwa angerithi jimbo la Sumbawanga.

  Hivyo Coadjutor Bishop (mwandamizi) ndiye pekee mwenye haki ya kurithi Jimbo.

  Tofuti yake na Auxiliary Bishop (msaidizi) kama Kilaini ni hii ya kurithi jimbo. Leo hii askofu wa Bukoba yaani Nestory Timanywa akifariki upo uwezekano wa jimbo kubaki wazi likiendeshwa na askofu msaidizi kwa muda hata wa miaka likisubiri apatikane askofu mpya.

  Na inawezekana padri mwingine humuhumo Bukoba akapewa jimbo hilo na Kilaini akaendelea kuwa msaidizi. Ndivyo kanisa Katoliki lilivyo nndiyo maana wavivu kutafiti huishia kufananisha na taasisi kama serikali au vyama na badala yake wanaishia kutojua chochote.
   
 12. P

  Paschal Matubi Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25


  Hii ilishajadiliwa hapa jamvini watu wakasema tunaleta topic zisizofaa. Nadhani ndiyo maana MEDERATOR aliondoa ile subject isemayo KADINALI NI NANI.

  Mimi nimeipata kwa ku-search nje ya JF yaani google.

  Click here ujisomee mwenye ni nini maana ya ukadinali.
   
 13. P

  Paschal Matubi Member

  #13
  Dec 7, 2009
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 25
  Mambo ya heshima wanayajua wanaoidhani hiyo heshima. Vatican na kanisa kwa ujumla linawajua watumishi wake wote wakiwemo maaskofu. Kilichotokea kwa Kilaini ni kwa vile Dar ndilo jimbo lenye vyombo vya habari vingi na ndiko kuliko na viongoi wa serikali wengi.

  Hivyo askofu aliyeko D"salaam basi lazima atajulikana maana kila linapokuja suala la kanisa Katoliki basi wa kwanza kukimbiliwa ni yeye. Ilifikia kila jambo anaulizwa Kilaini hata kama linahusu majibo yote badala ya kumuuliza Rais wa Baraza la maaskofu ambaye ni askofu wa Jimbo la Dodoma.

  Ingekuwa uongozi wa kanisa unapatikana kwa kuangalia propognda magazetini basi hakuna askofu nchini anayeandikwa kama Kilaini. Kilaini anajulikana hata na mtoto mdogo wa Kigoma na kuna watu wanadhani ni msaidizi wa kardinali. Ingekuwa mbinu hiyo ya wanamtandao inafanya kazi hata kanisani basi Kilaini angefaidi propoganda za wanamtandao kwa kusemwa sana kwenye vyombo vya habari.

  Hivyo ile heshima tunyoisema ni sisi tunampachika lakini kanisa linajua wazi ni kila askofu ana heshima sawa hata jimbo lake liwe tajiri a lina vyombo vya habari kilko vyote duniani.

  Ingekuwa hivyo basi maaskofu wa America wangeongoza kwa heshima kwani huko ndiko kisima cha mitandao ya habari.
   
 14. K

  Kieleweke Member

  #14
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na wewe kwa nini hukuuliza swali hili huko nyuma wakati majimbo ya Kigoma, Musoma, Moshi na Kayanga yalipopata maaskofu wapya wakati Method Kilaini akiendelea kuwa askofu msaidizi pale Dar?
   
 15. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,065
  Likes Received: 3,993
  Trophy Points: 280
  Kwa tunaojua kinachoendelea tunanyamaza kimya subirini mtajua karibuni ni nini kinaendelea huko!
   
 16. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo ni nani msaidizi wa Cardinal Pengo?
   
 17. m

  matambo JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika mume wa mke mmoja (i timotheo 3:2), kisha mwenye kuisimamia nyumba yake vema,ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu (1 timotheo 3:4)
  hizo ni miongoni mwa sifa za askofu kulingana na mkusanyiko wa vitabu(kigiriki biblos,kiingereza bible) sasa hawa maaskofu wasiooa wamepata wapi kifungu kinachowaambia padri au askofu asioe?

  yaleyale mapokeo na historia za mababa wa kanisa
   
 18. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  As far as I know kwenye Kanisa Katoliki hakuna mwenye hati miliki ya jimbo au mahali fulani. Padre au askofu yeyote anaweza kuchaguliwa kuwa jimbo lotole.

  'Demotion' inatokea kama askofu au padre akikatazwa kutoa huduma fulani ili kuogopa kusababisha scandal/kusababisha uharibifu wa maadili. Inategemea pia kama Kilaini mwenyewe aliomba kwenda karibu na nyumbani etc.

  Kungekuwa na tatizo la kiuchungaji au kimafundisho asingeruhusiwa kushika wadhifa. Na kila uhamisho unapangwa na maaskofu wa nchi husika kwa kushirikiana na askofu husika na Papa ana'assent' kwa mapendekezo yaliyotolewa. Ndiyo Kanisa Katoliki linavyo'operate'. Papa hawezi kudi'ctate' la sivyo angekutana na upinzani mkubwa na hata kuachiwa majimbo ayaongoze yeye mwenyewe.
   
 19. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Na kwa nini majimbo hukaa muda mrefu wakati mwingine zaidi ya mwaka bila ya kuwa na Askofu wakati mapadre wapo kibao wa kuziba hayo mapengo? Na je ili kuwa Archbishop mpaka uwe na vigezo vipi? Na kuna tofauti gani kati ya Askofu msaidizi, Askofu na Archbishop?
   
 20. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Haya yote yanaeleweka na ni wewe tu usiyeyaelewa! For your information, mwanzoni mapapa, maaskofu na mapadre walikuwa wanaoa hadi karne ya 12, nadhani.

  Kwa muda huo Kanisa lilikuwa katika 'scandals' nyingi za kula mali ya Kanisa, kuwaweka kwenye uongozi - upadre, uaskofu, upapa - watoto wa kiongozi fulani wa juu. Kulikuwa na 'nepotism' ya hali ya juu na pia watu wengi walidai fidia hasa padre, askofu au papa fulani alipoaga dunia... wakidai ni watoto wake na hivyo wanataka sehemu ya urithi wao. Kulikuwa shida kujua ni nani alikuwa sahihi na ni nani hakuwa sahihi.

  Papa fulani alipoingia madarakani, akataka kuleta 'radical changes' ili kuondokana na matatizo ya wakati huo na ndipo 'discipline ya celibacy' ilipoanzishwa (na siyo divine law, muda wowote inaweza kubadilishwa).

  Of course, Biblia ni neno la Mungu na mstari fulani unaweza kukugusa wewe na mstari mwingine usikuguse ila ukamgusa mtu mwingine. Si unakumbuka pia kwamba hata baadhi ya mitume walikuwa na wake? Siku moja Yesu aliwapa fundisho la kuwagusa kuhusu kuacha familia na kumfuata yeye na Petro akasema: "Tazama sisi tumeacha yote na kukufuata wewe tutapokea nini?"

  Yesu akawajibu kuwa "walioacha familia - mke, watoto, wazazi kwa ajili yake - watapokea mara mia zaidi na kuurithi ufalme wa mbinguni." Pia kuna sehemu alifundisha kuhusu kumwacha mke na kumwoa mwingine kuwa ni kuzini dhidi yake na wao wakasema kama ndivyo hivyo hakuna haja ya kuoa kwani hakuna atakayeokoka.

  Na yeye akawajibu "si wote wanaoweza kupokea fundisho hili bali wale tu ambao wamefunuliwa". Kwa hiyo, kama mtu mwingine akisoma maneno haya na kuguswa nayo na kujitahidi kuyaishi kiaminifu, who am I to say, he's wrong? Ikitokea pia mtu mwingine akasoma mstari uliou'qoute' na kuguswa nao pia ni sahihi kuishi hivyo.

  By the way, unajua 'context' yake? Ilikuwa pia tatizo fulani lilikuwa limeshajitokeza katika viongozi wa Kanisa kuoa wake zaidi ya mmoja. Na Timotheo alitaka kurudisha heshima na kulinda 'permanency' ya ndoa na ndiyo maana alifunisha hivyo ili viongozi ndio wawe mfano kwanza. Hivyo, usidhani walikuwa hawana wake na yeye akawatungia sheria hiyo. Hapana. Ilikuwa katika kulinda heshima ya ndoa kwa viongozi ambao walikuwa wameanza kuoa zaidi ya mke mmoja.

  After all, kinachotakiwa kwa Mungu is not so much kuoa bali kuishi kama Mungu anavyotaka. Kama ndoa ingekuwa lazima kwa kila mtu basi watu ambao wangependa kuoa lakini kwa sababu wasiozijua wao hawawezi wangekuwa mara zote katika dhambi kwa kushindwa kuoa. That's what I can share with you.
   
Loading...