Mhashamu Methodius Kilaini ahamishiwa Jimbo la Bukoba

Iwepo blog kwa ajili ya masuala ya kiroho kama haya.

JF ni kama radio yenye station nyingi. Ukitaka RADIO One una-tune meter zake, Ukitaka CLOUDS FM ni chaguo lako.

Huna haja ya kung'angania stesheni moja tu ya RADIO TUMAINI eti kwa sababu ni ya masuala ya kiroho.

Hivyo hata hapa JF ukiona forum ina-bore kuna Jukwaa la Siasa, Entertainment.

Tumbukia huko mkuu!
 
Samahani mkuu kulingana na hiyo timothy aliyotoa mwana JF askofu anatakiwa awe mme wa mke mmoja. Wewe unasema mna mapadre wenye family sidhani kama umejisalimisha kwenye kweli ili Ikuweke huru. Nasema hivyo maana ninavyofahamu RC kufuzu upadre na kuaminiwa kukabidhiwa parokia ni sharti uwe huna mke. HAKUNA HIARI YA KUCHAGUA HAPO HILI NI FUNDISHO LA SHARTI NDANI YA RC!!
 
Samahani mkuu kulingana na hiyo timothy aliyotoa mwana JF askofu anatakiwa awe mme wa mke mmoja. Wewe unasema mna mapadre wenye family sidhani kama umejisalimisha kwenye kweli ili Ikuweke huru. Nasema hivyo maana ninavyofahamu RC kufuzu upadre na kuaminiwa kukabidhiwa parokia ni sharti uwe huna mke. HAKUNA HIARI YA KUCHAGUA HAPO HILI NI FUNDISHO LA SHARTI NDANI YA RC!!

Is that, what you know or that, which you think you know?
 
Huu uhamisho ukipeleka kwenye siasa tunaweza sema jamaa amemzidi Kardinali Pengo umaarufu kwa hiyo ameenda kuchomekea kwa Papa ili ampeleke mafichoni hukooo Bukoba sijui kama tutakuwa tukimwona na kwenye TV tena ukija kidini tunasema mtumishi wa Mungu ana hubiri neno sehemu yoyote ile.

True
 
Mbona unakuwa mkali sana? Au kuna kitu umepoteza kutokana na mabadiliko hayo? Mimi nimesema inawezekana kabisa...sijasema nina evidence yoyote na nijuavyo mimi vatican huwa haina haraka katika mambo inayokusudia kuyafanya kwa nia zake nzuri tu. Kupanga safu ya uongozi wa kanisa kwani ina tatizo gani? Kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho ni kuwa Dar siyo Bukoba.Namtakia kazi njema za kiuchungaji Askofu Kilaini

Hakuna kitu ninachopoteza hata kama Pengo naye atahamishwa au wote wawili wapelekwe nchi nyingine. Nilikuwa natoa namna 'appointments' katika ngazi ya askofu zinavyofanywa.
 
Padri Privatus Karugendo hakuwahi kuwa padri wa jimbo la Bukoba ambalo liko chini ya Askofu Nestory Timanywa tangu mwaka 1974. Yeye amekuwa padri wa jimbo la Rulenge lilikouwa chini ya Askofu Mwoleka na baadae akarithiwa na askofu Severin NiweMugizi ambaye hawakuiva na Karugendo.

Hata hivyo jimbo lake la Rulenge limegawanywa mwaka jana na kuzaa jimbo jipya la Kayanga lililoko wilaya ya Karagwe na Rulenge ya NiweMugizi ikaitwa Rulenge-Ngara.


Umenikumbusha huyu rafiki yangu Padre Privatus karugendo. Huu nilikaa nae vizuri sana kule kayanga, karagwe enzi zile . Yeye anatokea Ibwera, ndugu zake ni Primu, na Prudence wote ni waandishi.

nazipenda sana makala zake pamoja na zile za mdogo wake Prudence.

nasikia anaishi tabata siku hizi.
 
Hakuna kitu ninachopoteza hata kama Pengo naye atahamishwa au wote wawili wapelekwe nchi nyingine. Nilikuwa natoa namna 'appointments' katika ngazi ya askofu zinavyofanywa.
Asante mkubwa. Ninaamini yote yanafanyika kwa heri kabisa na ni kwa utukufu wa wenyezi mungu. Ni kweli kabisa chochote kinaweza kutokea including watu wakubwa kama hawa kupewa uhamisho pale sababu zinapojitokeza.Kitu cha muhimu ni kuwa hata kazi za kanisa nazo zina dhamana yake na ndio maana tunaomba kila mtu atimize wajibu wake vile inavyopaswa kufanyika.
 
Samahani mkuu kulingana na hiyo timothy aliyotoa mwana JF askofu anatakiwa awe mme wa mke mmoja. Wewe unasema mna mapadre wenye family sidhani kama umejisalimisha kwenye kweli ili Ikuweke huru. Nasema hivyo maana ninavyofahamu RC kufuzu upadre na kuaminiwa kukabidhiwa parokia ni sharti uwe huna mke. HAKUNA HIARI YA KUCHAGUA HAPO HILI NI FUNDISHO LA SHARTI NDANI YA RC!![/QUOTE]

Ndugu yangu Kiby naomba nikufahamishe hivi, sio Wakatoliki wote ni Mapadri, na kama mtu ana huo wito wa kuwa Padri basi hapo hakuna kulazimishwa ni utashi wa mtu mwenyewe aliyeamua kwenda seminari huku akijua kuwa anakoenda kuna misingi ya namna fulani, KWA HIYO MTU KWENDA SEMINARI NA KUWA PADRI NI HAIRI YAKE MWENYEWE NA SIO SHURUTISHO

kuhusu kuoa kwa mapadri wa Kikatoliki nadhani kuna mtu huko nyuma alijaribu kukufahamisha kuhusu hiyo TIMOTEO, lakini kwa msaada wako na wengine wenye wasiwasi na hilo hebu tuangalie kitabu cha Mathayo

MATHAYO 19:1, Inaongelea mambo ya talaka na sheria za Musa za ndoa,

MATHAYO 19:10 "Wanafunzi wake wakamwambia, mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
MATHAYO 19:11 "Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa,
Sasa katika mathayo 19:12 Yesu anawaelezea watu wa aina tatu ambao hawajaoa au hawana uwezo wa kuona kwa maana ya kutofanya TENDO LA NDOA (MATOWASHI)

MATHAYO 19:12 Maana wako Matowashi walizaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao (yaani hawa hawana uwezo wa kufanya hilo tendo la ndoa kwa sababu wamezaliwa hivyo);

Tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi (kuna watu walikuwa wanawaathi watu ili wawatunzie wake zao au wafanyakazi wa ndani kwa hiyo wanakuwa hawawezi kuoa kwa sababu wanakuwa hawana huo uwezo tena);

TENA WAKO MATOWASHI WALIOJIFANYA KUWA MATOWASHI KWA AJILI YA UFALME WA MBINGUNI. AWEZAYE KULIPOKEA NENO HILO NA ALIPOKEE (Bwana Yesu anasema kuna watu waliojifanya wasioe kwa sababu ya ufalme wa mbinguni, lakini mwisho akamalizia sio lazima ni kwa mwenye WITO ni kwa yule mwenye uwezo wa kulifanya hilo fundisho na hapa ndipo ULIPO MSINGI WA USEJA KATIKA UKATOLIKI),

NIMEJARIBU KULIVUNJAVUNJA HILO ANDIKO LA MATHAYO 19, LAKINI KWA UELLEWA MZURI NI BORA UKALISOMA ANDIKO ZIMA
MATHAYO 19:1-12

TUMSIFU YESU KRISTU
 
Wakuu.
Aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Methodius Kilaini amepata uhamisho kwenda kwenye jimbo la Bukoba kuwa Askofu Msaidizi.Uhamosho wake umezua masuala kadhaa miongoni mwa wanajamii ya kikatoilik na wale wa nje ya katoliki.Wengine wamehusisha na siasa na kudai kuwa ukaribu wake na JK ndio uliomponza kwani amekuwa akiwa sana upande wa JK hata pale anapokosea.Inasemekana urafiki wao ulianza tangu JK akiwa Waziri wa Mambo ya Nje.Wengine wanasema kwamba Kilaini alikuwa karibu sana na wanajamii hivyo kuwafunika viongozi wake wa juu. Webgine wanahoji kwanini iwe Bukoba wakati kuna Majimbo Makuu yanayohitaji usaidiza kama vile Tabora,na paia wanahoji mbona kuna majimbo yaliyoko wazi kama vile Mwanza baada ya kifo cha Askofu Antony Mayala.

Wakuu hii imekaaje?
 
Haya ni majungu. Haina maana kujaribu hapa kuchambua kwanini kahamishwa, na kwanini bukoba. Kanisa Katoliki lina utaratibu wake wa utendaji na linajua linafanya nini na kwawakati gani. Huu ni uhamisho wa kawaida tu wa kichungaji.
 
Nini maana ya Mhashamu?

Nini maana ya Kardinali?

Ipi cheo kikubwa katika hizo (elimu tu tafadhali)

Pamoja na uelewa wangu mdogo, niseme tu kile ninachojua:
Mhashamu: Ni neno litumikalo kama tutumiavyo neno 'mheshimiwa' lakini kwa Maaskofu tu. Neno jingine ni 'Mwadhama', hili linatumika kwa makardinali. Mifano inaweza kuwa Mhashamu Baba Askofu Methodius Kilaini, na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Kardinali: Hawa ni maaskofu au mapadre wanaoteuliwa na Baba Mtakatifu (Papa) kama wasaidizi wake wa karibu katika masuala mbalimbali na pia ni washauri wake katika mambo ya uongozi. Makardinari kwa kawaida wanaishi huko Vatican, lakini Makardinari wanaoteliwa wakiwa maaskofu katika majimbo yaliyo katika nchi zao (mf. Kard. Pengo) wanaishi katika nchi zao, wakiendelea na kazi zao za kawaida, na wakati huohuo wanakuwa wasaidizi na washauri wa Papa. Hawa makardinali wana haki zote kama raia wa nchi ya Vatican City (Rais ndiye Papa) na ndio hawa ambao wanapiga kura ya kumchagua Papa, na Papa kwa kawaida anachaguliwa kutoka katika kundi hilo la makardinali.
Kwa kifupi ndio hivyo nijuavyo.
 
Back
Top Bottom