Shakazulu
JF-Expert Member
- Feb 23, 2007
- 957
- 280
Nimeipata hii toka kwenye blog ya Michuzi
BREKING NYUUUUZZZZZZZ
SERIKALI itagharamia matibabu ya nje ya Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi, Saidi Kubenea, aliyesafirishwa leo, Jumatatu, Januari 7, kwenda India kwa matibabu zaidi.
Serikali inagharimia matibabu hayo ya Kubenea, kama inavyogharimia matibabu ya Watanzania wengine wanaokwenda kupata huduma za tiba nje ya nchi.
Msimamo huo wa Serikali umetangazwa mara tu baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amemtembelea na kumjulia hali Bw. Kubenea kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Bw. Kubenea ambaye alilazwa Muhimbili usiku wa Jumamosi iliyopita, Januari 5, wakati watu wasiojulikana walipovamia gazeti la kila wiki la Mwanahalisi na kumjeruhi Kubenea pamoja na Mhariri wa gazeti hili, Bw. Ndimara Tegambwage.
Katika shambulio hilo, Bw. Kubenea alimwagiwa tindikali wakati Bw. Tegambwage alipigwa panga kichwani. Wakati Bw. Kubenea alilazwa hospitali, Bw. Tegambwage alitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.
Kama alivyokuwa ameeleza katika taarifa yake rasmi kwa vyombo vya habari jana, Januari 6, 2008, Rais Kikwete amemweleza Bw. Kubenea jinsi alivyosikitishwa na kuhudhunishwa na shambulio dhidi yake, na dhidi ya Bw. Tegambwage.
Rais amesema kuwa kama wahariri hao wameshambuliwa katika hali ya kawaida basi ni jambo baya.
Hata hivyo, amesema kuwa ni jambo baya zaidi kama wahariri hao watakuwa wameshambuliwa kwa sababu ya kazi yao ya uandishi wa habari, kwa sababu hilo ni pigo kwa juhudi za Serikali katika kulea na kuunga mkono vyombo vya habari huru na vinavyojitegemea nchini.
Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.