ES
Mawazo yako hayana tofauti na baadhi ya watu wanaopenda kupata majibu ya haraka bila kutumia muda kutafakari.
Jana nilisikitika nilipoanagalia Taarifa ya Habari na leo niliposoma Tamko La BAVICHA,Mzee Mengi,Makunga,Sakina Datoo hawa nao niliona ni kwa kiwango gani walivokua wavivu wakufikiri pale walipo toa hukumu kabisa kua Kuvamiwa kwa kubenea kuna Uhusiano wa moja kwa moja na UANDISHI wake,hawa watu ktk matamko yao walitoa hukumu kabisa kua kubenea amehujumiwa,kama ilivo kwa JOHN MNYIKA ( ingiwa najua tatizo lake ni uanaharakati,na tabia yao nikutafuta majibu rahisi)kudai kua
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa kuwa badala ya kunyosha kidole moja kwa moja kuwa fulani anahusika kama alivyofanya Haji Duni juzi ni kutokuwa mwajibikaji.
vijana waliofanya tukio wametumiwa na mafisadi so wasitumike, bila kukumbuka kua mmoja alie kamatwa ana miaka 65 sijui kama ni kijana.
Umezungumza kama mtu mwenye mamlaka ya kujua unachosema. Na nikisoma vizuri unasema hakukuwa na MZEE aliyefanya kitu hicho. Na hutumii maneno ya "madai" ya vijana.. ila unasema vijana waliofanya hivyo na unashangazwa kwanini Bw. Mushi wa Kinondoni atajwe miongoni mwa vijana hao! mmmh...
RIOBA ktk waongeaji alikua more objective na hakutaka kuhukumu ingawa Prof wangu Shivji nae jana kidogo nilijiuliza is it uzee unamuanza au ni bcs nae ameaminishwa kua kubenea amehujumiwa na mafisadi, Mengi yeye simshangai ni mzee wa kuchukua oppprtunities na always hua ni mtu wa kukurupuka.
KUna kitu ambacho hukukisema alichosema Mengi ambacho ni kuwa kushambulia waandishi wa habari ni sawa na kushambulia kioo kwa vile tu kinakuonesha jinsi ulivyo mchafu! Hiyo ndiyo ilikuwa message yake. Na kuhusu being opportunist kweli unaweza kulinganisha na CCM.. kisa na mkasa wa serikali kuingilia kati na kumgharimia Kubenea ni nini? Ina maana leo hii kila Mtanzania anayepatwa na janga na anataka kwenda India au kwingine kwa matibabu serikali itaingilia kati..?
JANA NILIULIZA MASWALI HAPA JF KUA KAMA KWELI KUBENEA AMEKUA ANAKUMBANA NA VITISHO (JE ALISHINDWA KUWEKA ANGALAU MLINZI WA KIMASAI KTK OFISI YAKE? PIA WHY WATU WANAKIMBILIA KUDAI KUA AMEHUJUMIWA BCS YA UANDISHI WAKE NA TUSIJIULIZE MASWALI MADOGO MAY BE KADHULUMU,KACHUKUA MKE WA MTU,AU WALIOVAMIA NI VIBAKA,OR NI MATEJA BCS HATA SILAHA ZAO NI MAARUFU MIONGONI MWA MATEJA,etc)
Katika Tanzania jukumu la kulinda raia na mali zao haliko kwa wamasai ama wamakonde. Wenye haki na jukumu hilo kisheria ni Polisi. Hivyo swali lako lina makosa ndani yake. Ungeuliza "Hivi Kubenea alishindwa kutoa taarifa Polisi za vitisho hivi kwa muda huu wote na Polisi wakashindwa kumpatia ulinzi wa uhakika au kumshauri hatua za kuchukua?" Ungeuliza swali hilo jibu lake lingekutisha.. but your are too smart for that.. you had to ask the "wrong" question to imply a correct answer!
Watanzania wengi wanataka kuaminishwa kwamba tukio hilo ni hujuma kwa vigezo kua amekua akipata sms za vitisho,or ametaka kugongwa naGARI makusudi,hivi kwa siku ni wangapi wanapoteza maisha kwa kugongwa na magari either kwa uzembe wa DEREVA au wa mtumiaji wa njia mwenyewe,why tusijiulize kubenea inawezekana alikua amelewa akashindwa kufata sheria za barabarani or dereva aliemkosa alikua amelewa mzembe.
Ajali ambazo zinamfuata mtu mmoja na simu za vitisho zinazomfuata mtu mmoja na hatimaye kushambuliwa mtu huyo huyo huwezi kuweka kwenye kundi la "vitu vya kawaida". Ni wangapo ya "wanaopoteza maisha yao kwenye ajali ya gari" wanakutana na yafuatayo:
- Simu za vitisho
- Message za vitisho
- Gari kuungua katika mazingira ya kutatanisha
- Kuvamiwa na watu ambao hawataki kitu chochote zaidi ya kudhuru mwili
- Kumwagiwa tindikali?
Nioneshe mtu mwingine mmoja mwenye mkosi wa namna hiyo. Hata hivyo hoja yako ina jambo jingine la kutisha. Unataka fikra za watu zielekezwe "nje" ya uwezekano wa tukio hilo kuhusishwa na kazi yake? Kwa nini? Kwanini usiwe kama mimi na kuweka options zote wazi without excluding anything na kuacha Polisi wafanye kazi zao. Kwanini hutaki watu watoe fikra zao na kuzihusisha na sababu yoyote ile..? Unless of course.. YOU know why....
Nachoomba kuptia Forum hii WAANDISHI walifanye tukio hili kama matukio mengine mpaka pale uthibitisho utakapo kua kweli ni hujuma.
Nina habari mbaya kwako. Kwa bahati mbaya haiwezekani kulifanya tukio hili kuwa "kama matukio mengine"... naomba unisaidie tukio hili linafanana na tukio jipi jingine?.. ambalo halikuwa kutangazwa au liliwahi kutangazwa. Tukio jingine naweza kukufananisha nalo ni lile la waandishi kupigwa kule Ukonga (kina Bukuku) na serikali kulihalalisha kwa kusema ilikuwa sawa (alikuwa O. Mapuri aliyetoa baraka hizo). Ni tukio hilo ulikuwa unaliwazia uliposema "matukio mengine"?
Ni hatari kwa jamii kuwapa nafasi watu kama SAKINA DATOO wa SUNDAY CITIZEN bcs mara nyingi amekua ni mtu ambae ni opportunist wanao fanya nae kazi wanlijua hilo anapotoa kauli zake mara nyingi hana Facts,na anakua ni mtu wa kuongozwa na HISIA zaidi,MAKUNGA jana alionyesha kitu cha ajabu kua waandishi wanafanya uchunguzi kabla ya kuandika (theme ya maongezi yake) lakini nilishangaa je kabla ya kuongea alikua amefanya uchunguzi wa kiwango GANI? MAMA TAMWA sijashangaa ni NATURE ya kazi yake wana harakati mara nyingi ni watu hatari sana bcs to them kilakitu ni opportunity kama alivo wahi kusema PROF WANGU MAREHEMU CHACHAGE (TO TRUST ACTIVIST IS NOT SAFE AS TO TRUST REVOLUTIONIST)
Huwezi kuwaambia watu wasiwe na hisia kwa sababu hisia zao hazikubaliani na hisia za kwako. Hata hivyo point yako hapa ni kubwa. Ndio maana nimepiga sana kelele kuhusu Raila kwa sababu maneno huchochea hisia zaidi na hupofusha mtazamo wa ukweli. Baadhi ya yaliyosemwa na baadhi ya waandishi kama Mwitumba jana yalikuwa yanapakana na uzushi! Nilisikitika kuona waandishi wanampigia makofi Mwitumba kwa kudai wale wote walioandikwa kwenye magazeti wajitokeze kukanusha kwamba hawakuhusika kana kwamba kwa kufanya hivyo kutawafanya HAWAKUHUSIKA! Good point.
Wana JF inawezekana ni kweli kahujumiwa,nani hatujui thats why TIBA anafanya uchunguzi tusubiri matokeo tujaribu kuangalia jambo la kubenea kwa mapana zaidi isije tukaifanya FANI YETU YA HABARI NI CHAKA LA MAOVU kila mwandishi akiguswa basi tu conclude hujuma bcs ni mwandishi ifike mahali tuliangalie jambo kwa UHALISIA WAKE kuliko HISIA.
Kwa mara nyingine tena unaandika kama mtu anayejua kilichotokea (hasa kutokana na makala yako wiki kadhaa kuhusu Kubenea hapa JF). Kufikiri kuwa Tibaigana anafanya uchunguzi ni vituko vya karne! Unataka nikupatie jibu watakalolipata? Watawakamata watu kama walivyofanya na watu hao watakiri kuhusika na tukio hilo na sababu watasema walitaka kuiba vitu na uporaji ukatoka kombo na watasema hawakuwa na mpango wowote wa mambo ya uandishi wa Kubenea. Hivyo uchunguzi umeonesha ni tukio la kijambazi tu na hakuna ushahidi kuwa lilimlenga Kubenea kama mwandishi!
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
ndiyo! KIGUMU!