Mhadhiri Vicensia Shule: Rushwa ya Ngono inatawala Chuo Kikuu DSM

Usikute nayeye wakat anasoma alishatoa hiyo rushwa asiwaonee wenzie wivu basi
 
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) ameandika katika ukurasa wake wa twitter kuhusu kukithiri kwa rushwa ya ngono chuoni hapo

Baba @MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli

MY TAKE:
Taasisi zote zinazohusika zichukulie swala hili kwa uzito wake. Rushwa ya ngono inapelekea wahusika wengi kuonekana vizuri kwenye makaratasi kumbe kichwani ni 'kilaza'

=======

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt Vicencia Shule, amemuomba Rais Dkt Magufuli kuingilia kati, kutokana na kukithiri kwa rushwa ya ngono chuoni hapo. Dkt Shule alizuiwa kuonesha bango lake kuhusu vitendo hivyo, wakati Rais akizindua maktaba mpya chuoni hapo leo.

Mimi binafsi sipingi tuhuma zilizotolewa na huyu mama ila nina maswali kadhaa yananipa shida kutokana na namna alivyowakilisha wazo lake kwenye hadhira ya UDSM na watanzania wote kwa ujumla

MOJA: Huyu mama anadai kuwa tatizo hili lipo siku nyingi na alishawahi kuwasilisha malalamiko yake kwenye ngazi za zinazohusika na kwamba wasaidizi wa VC wanayajua malalmiko haya. Hata hivyo huyu VC wa sasa ni mpya hata mwaka mmoja hajamliza madarakani. Kama ni hivyo alijua kuwa VC wa sasa alikuwa hana taarifa, kwa nini asingechukua hatua ya kwenda kumuona ofisini na kumuuliiza kabla ya kulipua bomu la namna hii tena mbele ya Rais?

MBILI: Kama wasaidizi wa VC na ambaye ni mpya walikuwa wanalijua hili, ina maana kuwa VC aliyepita yeye possibly alikuwa analijua fika ila kwa bahati mbaya, labda muda wake wa kuondoka ofisini ulifika kabla hajaweza kulichukulia hatua. Still kwa nini VC wa zamani asingemu-alert VC wa sasa juu ya swala swala hili ambalo ni sensitive kipindi wakati wanakabidhiana ofisi? Kwa sababu kama wasaidizi wa VC yule wa zamani aliowaacha walikuwa wanalijua, obvoius VC aliyepita naye pia alikuwa analijua!

TATU:Juzi j4 Rais ametembelea UDSM kwa mara ya 5, mara mbili ndani ya kipindi hiki kifupi cha mwezi huu wa Novemba, na chini ya uongozi wa VC huyu mpya. Rais pia ametembelea UDSM mara 3 katika ugeni ambao ulikuwa na intervals ndefu sana kutoka ugeni mmoja hadi mwingine, wakati VC aliyepita akiwa bado madarakani. Je, kwa nini huyu mama katika safari zote hizo hii issue alikuwa amekaa nayo tu wakati nimsensitive hivyo? Kwa ni hakuamua kuilipua kipindi hicho na badala yake akafanya hivyo juzi? Inaonyesha KAMA alisubiria kwanza mpaka yule wa zamani atoke, halafu aingie mwingine ambaye wala hana hata taarifa ya tuhuma hizi, halafu aje afanye timing siku Rais akija kwa sababu tayarai ilikuwa inajulikana kuwa LIBRARY MPYA ilikuwa scheduled tangu mwanzo kuwa itakuja kufunguliwa na Rais

NNE: Kama wasaidizi wa VC walikuwa na tarrifa hizi na huyu mama alikuwa anajua hilo, na ukizingatia kuwa uongozi tayari ulikuwa umebadilika na kuwa na VC mpya, huyu mama alishindwa nini kuwakumbusha wasaidizi wa VC mpya wamweleze kuhusu issue hii hadi akasubiria ujio wa Rais, assuming alikuwa hana nafasi ya kwenda kumuona personally?

Hii issue ina KAMA siasa ndani yake na inataka kufanana kabisa na ile ya kipindi kile wakati DVC-Academics aliyepita, alizushiwa kuwa na wanafunzi hewa.
Huyu mama ningekuwa na mamlaka naye vizuri mtu kama mimi, ningemuita akanipa ufafanuzi kwa kina juu ya queries hizi nilizozitaja hapa. Hoja yake ni ya msingi, lakini why all these queries?

By the way, sipingani na hoja yake, napingana na her manner of presentation ya hoja yenyewe. Hayuko sahihi sana na inaonyesha kama ana kitu cha ziada kifuani ameficha ambacho ni tofauti na hoja aliyotoa, na ndicho kilimsukuma kutoa hoja hii. Kwa hiyo hoja hii japo tunaiona sensitive, mama huyy anaweza akawa ameitoa BY THE WAY na wala hina mashiko kwake. Ana kitu chake kingine cha ziada anachotamani kukifanyia kazi.

Naomba kuwasilisha ila naomba awe mwangalifu utoaji wa hoja kwa staili hii, kuna siku utakuja u-backfire kwake. As a University Lecturer, she is supposed to be smart in all her presentations
 
umenikumbusha mnamo mwaka 2007, girlfriend wangu alidisco yeye na group lake la watu 5 pale the maarufu kama "The Only Faculty" kwa kuwakatalia wahadhiri wakware, akaenda zake Mzumbe kuanza upya na akafaulu vizuri tuu, kwa sasa ni wakili msomi.
 
Mbona hata yeye ana muonekano wa mtu aliepata udokta wake kwa kutoa rushwa ya ngono?

Na hii ndio fikra halisi ya walio wengi katika wanaume wa kitanzania/kiafrika (hao lecturers ni sehemu yao) kiasi hadi baadhi ya wanawake nao wana perception hii!! Muy estúpido!!
Chief kweli una utaalamu mkubwa kiasi hicho wa kubaini watu degree wamezipataje kwa kuangalia muonekano wao tu kwa picha?? If so, basi tumepoteza muda na pesa katika zoezi la uhakiki wa elimu za watumishi na wewe umepoteza fursa ya ku expand your primitive imagination + mkwanja, maana tungekutumia picha tu whatsapp then unatuhakiki!!
 
Hili suala la rushwa ya ngono nakumbuka lilishajadiliwa tena. Nilibahatika kusoma na bado nakumbuka mapendekezo ya mwanaJF mmoja ya kuundwa madawati ya jinsia na maadili kwenye hivi vyuo vikuu. Haya madawati yawe na uwezo wa kumhoji na kuwasilisha mapendekezo mahsusi ikiwepo ya kuachishwa ajira kwa wahadhiri bila kijali nafasi mhusika anayoshikiliq au kiwango cha elimu yake(prof, phd, mkuu wa idara, dean nk. ).

Vyuo vikuu inabidi viwe mwanga kwenye hizi tuhuma kwa kujisafisha vyenyewe. Visisubiri mpaka viingiliwe na mamlaka zilizo nje ya hivyo vyuo mfano PCCB, na wanasiasa.

Nawasilisha.
TCU kama mlezi wa elimu ya juu nayo inabidi iweke procedures nzuri zitakazopunguza mazingira ya rushwa hii.
 
Nimemsikiliza kwenye mahojiano asubuhi hii kwenye Radio nadhani ni Magic FM, ile ya akina Salum Mkambala. Alikuwa anahojiwa kwa simu na ukimsikiliza alivyokuwa anawajibu unaona kabisa kuwa huyu ana kitu kingine cha ziada kifuani, tofauti na hoja aliyoitoa

Kwa wewe uliesikiliza unawewza kutoa mwanga wa kitu hicho kilicho kifuani??
 
Magufuli hawezi kumuelewa huyu... Hapo wamejaa Vipanga tuh.
 
Kwa wewe uliesikiliza unawewza kutoa mwanga wa kitu hicho kilicho kifuani??
Mwenyewe yupo unaweza kumuuliza, usiniulize mimi. Kitu kikiwa kifuani mwa mtu maana ni sawa na kiko mbinguni. Huwa unaelewa nini mtu anapokuambiwa kuwa una kitu kifuani?
 
Kwa udsm hili nikweli kabisa mkuu kuna dada wawili nawajua kabisa nilisoma nae,prof akamtongoza mara kadhaa Dada akamkatalia,akamwambia hutagraduate nakweli hatumaliza naye, alihangaika sana nakulia sana hadi kumtumia doctor mmoja ambaye alikuwa padre wa kanisani, wakaenda kwa head of department baada ya kumwita prof akasema yaishe,baadaye walipokutana akamwambia nitakukomesha unanishtaki mm prof kwa vidocta.

Akampa sup,akamcarisha then hakugraduate.Akaja mwaka mwingine kuclear alipomwona Kwenye lecture akamwambia unione,alipomwona akamuuliza bado unamisimamo yako ya kishamba? Dada akakaa kimya tu then akamwambia usiendelee kuja njoo siku ya UE nitakupa B tu maana hutaki A na ushamba wako.

Nawajua wadada wawili cos tulisoma pamoja, ila hizi departments ngoja nizihifadhi tu
Kuna swala la upande wa wanawake kukalia kimya matukio ya unyanyasaji/udhalilishaji.

Elimu itolewe zaidi ili wanawake wawe wanaripoti matukio haya kwenye vyombo husika na viwe vinafanyia kazi
 
Nikweli mkuu,ila chuoni wale malecturer wananguvu sana aisee, na wanaushirikiano hawawezi kumsimamia mwanafunzi cos nikashfa kwa chuo au department husika
 
Kwa udsm hili nikweli kabisa mkuu kuna dada wawili nawajua kabisa nilisoma nae,prof akamtongoza mara kadhaa Dada akamkatalia,akamwambia hutagraduate nakweli hatumaliza naye, alihangaika sana nakulia sana hadi kumtumia doctor mmoja ambaye alikuwa padre wa kanisani, wakaenda kwa head of department baada ya kumwita prof akasema yaishe,baadaye walipokutana akamwambia nitakukomesha unanishtaki mm prof kwa vidocta.

Akampa sup,akamcarisha then hakugraduate.Akaja mwaka mwingine kuclear alipomwona Kwenye lecture akamwambia unione,alipomwona akamuuliza bado unamisimamo yako ya kishamba? Dada akakaa kimya tu then akamwambia usiendelee kuja njoo siku ya UE nitakupa B tu maana hutaki A na ushamba wako.

Nawajua wadada wawili cos tulisoma pamoja, ila hizi departments ngoja nizihifadhi tu
Hebu tutajie mkuu! Mtu kama huyo mbali na hamu ya ngono aliyonayo, nahisi ana tatizo kichwani. Umri hadi ukaitwa Profesa lazima uwe ulishakuwa mzoefu na kutongoza na kukataliwa. Huna sababu ya kuloga mtu kwa sababu kakukatalia.

Nitajie jina boss! Watu kama hao wasipotajwa hawakomi!
 
UDSM haikuwa na uongozi kwa muda mrefu. KIla mtu alikuwa ni mwamba. Hata miradi ya kawaida waliramba rushwa! Tangu Mlimani City; Ikapelekwa eneo nje ya chuo bila sababu na yote iliyofuata. Ubaya ilikuwa ni serikali ya hovyo hovyo tu!

KUle SUA pia tuliambiwa kuna kiongozi mmoja ambaye ni womanizer akapewa wadhifa bila kujali tabia yake. Kiongozi wa aina hiyo lazima atashabikia tabia hiyo. Njia aliyotumia mama huyu ni halali na nzuri kukwepa viongozi wa aina hiyo.
 
Kwa udsm hili nikweli kabisa mkuu kuna dada wawili nawajua kabisa nilisoma nae,prof akamtongoza mara kadhaa Dada akamkatalia,akamwambia hutagraduate nakweli hatumaliza naye, alihangaika sana nakulia sana hadi kumtumia doctor mmoja ambaye alikuwa padre wa kanisani, wakaenda kwa head of department baada ya kumwita prof akasema yaishe,baadaye walipokutana akamwambia nitakukomesha unanishtaki mm prof kwa vidocta.

Akampa sup,akamcarisha then hakugraduate.Akaja mwaka mwingine kuclear alipomwona Kwenye lecture akamwambia unione,alipomwona akamuuliza bado unamisimamo yako ya kishamba? Dada akakaa kimya tu then akamwambia usiendelee kuja njoo siku ya UE nitakupa B tu maana hutaki A na ushamba wako.

Nawajua wadada wawili cos tulisoma pamoja, ila hizi departments ngoja nizihifadhi tu
So painful,hivi Maprofesa mbona wajinga hivi,mtu una pesa unaanzaje kung'ang'ania mwanafunzi.Wakati mtaani kuna wanyange wakali pesa yako tu.Profesa kama huyo ni kumtegesha tu Bomu siku moja itakuwa fundisho
 
Kuna swala la upande wa wanawake kukalia kimya matukio ya unyanyasaji/udhalilishaji.

Elimu itolewe zaidi ili wanawake wawe wanaripoti matukio haya kwenye vyombo husika na viwe vinafanyia kazi
Wanawake wao Kwa wao hawapendani.Ukiona mwanamke anajifanya kumaindi huenda kapinduliwa kwenye himaya yake au kuna kitu kakosa
 
Hivi ukiripoti kuombwa rushwa ya Ngono TAKUKURU si wataweka mtego mtuhumiwa akamatwe sivyo au una maana tutumie njia tofauti?
Tatizo ni kwamba hao wanaoombwa hiyo rushwa hawana ujasiri wa kuripoti kwenye vyombo husika.

Nampongeza huyo Dr.kwa kupaza sauti bilashaka hatua stahiki zitachukuliwa
 
Mimi binafsi sipingi tuhuma zilizotolewa na huyu mama ila nina maswali kadhaa yananipa shida kutokana na namna alivyowakilisha wazo lake kwenye hadhira ya UDSM na watanzania wote kwa ujumla

MOJA: Huyu mama anadai kuwa tatizo hili lipo siku nyingi na alishawahi kuwasilisha malalamiko yake kwenye ngazi za zinazohusika na kwamba wasaidizi wa VC wanayajua malalmiko haya. Hata hivyo huyu VC wa sasa ni mpya hata mwaka mmoja hajamliza madarakani. Kama ni hivyo alijua kuwa VC wa sasa alikuwa hana taarifa, kwa nini asingechukua hatua ya kwenda kumuona ofisini na kumuuliiza kabla ya kulipua bomu la namna hii tena mbele ya Rais?

MBILI: Kama wasaidizi wa VC na ambaye ni mpya walikuwa wanalijua hili, ina maana kuwa VC aliyepita yeye possibly alikuwa analijua fika ila kwa bahati mbaya, labda muda wake wa kuondoka ofisini ulifika kabla hajaweza kulichukulia hatua. Still kwa nini VC wa zamani asingemu-alert VC wa sasa juu ya swala swala hili ambalo ni sensitive kipindi wakati wanakabidhiana ofisi? Kwa sababu kama wasaidizi wa VC yule wa zamani aliowaacha walikuwa wanalijua, obvoius VC aliyepita naye pia alikuwa analijua!

TATU:Juzi j4 Rais ametembelea UDSM kwa mara ya 5, mara mbili ndani ya kipindi hiki kifupi cha mwezi huu wa Novemba, na chini ya uongozi wa VC huyu mpya. Rais pia ametembelea UDSM mara 3 katika ugeni ambao ulikuwa na intervals ndefu sana kutoka ugeni mmoja hadi mwingine, wakati VC aliyepita akiwa bado madarakani. Je, kwa nini huyu mama katika safari zote hizo hii issue alikuwa amekaa nayo tu wakati nimsensitive hivyo? Kwa ni hakuamua kuilipua kipindi hicho na badala yake akafanya hivyo juzi? Inaonyesha KAMA alisubiria kwanza mpaka yule wa zamani atoke, halafu aingie mwingine ambaye wala hana hata taarifa ya tuhuma hizi, halafu aje afanye timing siku Rais akija kwa sababu tayarai ilikuwa inajulikana kuwa LIBRARY MPYA ilikuwa scheduled tangu mwanzo kuwa itakuja kufunguliwa na Rais

NNE: Kama wasaidizi wa VC walikuwa na tarrifa hizi na huyu mama alikuwa anajua hilo, na ukizingatia kuwa uongozi tayari ulikuwa umebadilika na kuwa na VC mpya, huyu mama alishindwa nini kuwakumbusha wasaidizi wa VC mpya wamweleze kuhusu issue hii hadi akasubiria ujio wa Rais, assuming alikuwa hana nafasi ya kwenda kumuona personally?

Hii issue ina KAMA siasa ndani yake na inataka kufanana kabisa na ile ya kipindi kile wakati DVC-Academics aliyepita, alizushiwa kuwa na wanafunzi hewa.
Huyu mama ningekuwa na mamlaka naye vizuri mtu kama mimi, ningemuita akanipa ufafanuzi kwa kina juu ya queries hizi nilizozitaja hapa. Hoja yake ni ya msingi, lakini why all these queries?

By the way, sipingani na hoja yake, napingana na her manner of presentation ya hoja yenyewe. Hayuko sahihi sana na inaonyesha kama ana kitu cha ziada kifuani ameficha ambacho ni tofauti na hoja aliyotoa, na ndicho kilimsukuma kutoa hoja hii. Kwa hiyo hoja hii japo tunaiona sensitive, mama huyy anaweza akawa ameitoa BY THE WAY na wala hina mashiko kwake. Ana kitu chake kingine cha ziada anachotamani kukifanyia kazi.

Naomba kuwasilisha ila naomba awe mwangalifu utoaji wa hoja kwa staili hii, kuna siku utakuja u-backfire kwake. As a University Lecturer, she is supposed to be smart in all her presentations
Braza mbona kama imegusa ugali wako
 
Back
Top Bottom