AbaMukulu
JF-Expert Member
- Jan 1, 2018
- 2,048
- 3,568
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) ameandika katika ukurasa wake wa twitter kuhusu kukithiri kwa rushwa ya ngono chuoni hapo
Baba@MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli
MY TAKE:
Taasisi zote zinazohusika zichukulie swala hili kwa uzito wake. Rushwa ya ngono inapelekea wahusika wengi kuonekana vizuri kwenye makaratasi kumbe kichwani ni 'kilaza'
=======
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt Vicencia Shule, amemuomba Rais Dkt Magufuli kuingilia kati, kutokana na kukithiri kwa rushwa ya ngono chuoni hapo. Dkt Shule alizuiwa kuonesha bango lake kuhusu vitendo hivyo, wakati Rais akizindua maktaba mpya chuoni hapo leo.
=====
UPDATE;
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Vicensia Shule ameitwa kwenye kamati ya maadili ya Chuo hicho kuhusiana na taarifa yake aliyoitoa kwenye mtandao wa Twitter akimuomba rais John Magufuli kuingilia kati kukithiri kwa rushwa ya ngono chuoni hapo.
Baba