JACADUOGO2.
JF-Expert Member
- Dec 13, 2010
- 930
- 220
Nashangaa sana wabunge karibia wote wa CCM wanaposimama kuongelea suala la kuunga au kutokuunga mkono hoja utasikia wakisema "kabla sijaongea naunga mkono hoja asilimia mia" na ukiwasikia wakiongea wanalalamika kweli kweli kuhusu suala husika.
Je, wanajali maslahi ya wananchi au maslahi ya CCM?
Je, wanajali maslahi ya wananchi au maslahi ya CCM?
Hawa jamaa hawaeleweki kabisa Mbunge anasimama na kusifu Serikali kuwa ni sikivu,inajali watu wake,inamipango madhubuti kuiniua uchumi wa watu wake na kadharika ikiwa sambamba na kuunga mkono hoja zitolewazo na mawaziri katika kuwasilisha bajeti.
Wanapokuja kunichosha ni kuwa baada ya kutoa sifa zote hizo,Mbunge husika anaanza kulalamika mara ooh serikali imetutelekeza wakazi wa jimbo la ..... mara ooh serikali haikamilishi miradi kwa wakati muafaka na kero nyingi nyingi.
Ni bora mnapopata nafasi kuchangia muwe straight to point sio kuzunguka zunguka.
Spika: Sasa ni zamu ya mheshimiwa Udhaifu Sitaki
Udhaifu Sitaki: Asante Spika kwa kuniona
Kwanza nianze kwa kusema naunga mkono hoja hii ya bajeti kwa asilimia 500
1.Sikubaliani na kuongeza kodi katika vinywaji(soda na pombe) na sigara. kodi hizi zipunguzwe serikali
haiwezi kutegemea vyanzo hivi ya mapato,badala yake tutazame vyanzo vingine vya mapato
2.Pili,sikubaliani na suala la sehemu kubwa ya bajeti yetu kwenda kwenye matumizi badala ya miradi ya maendeleo
Mheshimiwa spika,asilimia 30 iliyotengwa kwa miradi ya maendeleo ni ndogo sana ukilinganisha na mahitaji ya wananchi katika nyanja mbalimbali.Tupunguze matumizi,katika gharama za uendeshaji wa serikali
Mengi yameongelewa hapa ila mimi nimeona nichangie katika haya mawili ambayo nadhani tunahitaji kuyafanyia marekebisho, nimalizie tena kwa kusema Naunga mkono hoja asilimia 500! Asante
Mimi: Hivi staili kama hizi za kuunga mkono hoja hazimaanishi huenda kuna nguvu za kurogwa hapa ?
Sijajua sasa wanawakilisha Serikali au Wananchi,
Utasikia naipongeza sana serikali yangu ya CCM kwa kuturetea maendeleo katika uongozi wake, mbele anaanza kuleta vilio kibao kutoka kwa wananchi wake, kwamba kuna ukosefu wa Umeme, Maji, Dawa, Barabara na huduma nyingi mbovu kwanini Serikali haiwasaidii Wananchi?,
Sasa unajiuliza Serikali aliyo isifia ni ipi? na anyoililia ni ipi.
CCM oyee