Nani aliyewaroga wabunge wa CCM kama huyu mheshimiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani aliyewaroga wabunge wa CCM kama huyu mheshimiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kalumbesa, Jun 21, 2012.

 1. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Spika: Sasa ni zamu ya mheshimiwa Udhaifu Sitaki

  Udhaifu Sitaki: Asante Spika kwa kuniona

  Kwanza nianze kwa kusema naunga mkono hoja hii ya bajeti kwa asilimia 500

  1.Sikubaliani na kuongeza kodi katika vinywaji(soda na pombe) na sigara. kodi hizi zipunguzwe serikali
  haiwezi kutegemea vyanzo hivi ya mapato,badala yake tutazame vyanzo vingine vya mapato

  2.Pili,sikubaliani na suala la sehemu kubwa ya bajeti yetu kwenda kwenye matumizi badala ya miradi ya maendeleo
  Mheshimiwa spika,asilimia 30 iliyotengwa kwa miradi ya maendeleo ni ndogo sana ukilinganisha na mahitaji ya wananchi katika
  nyanja mbalimbali.Tupunguze matumizi,katika gharama za uendeshaji wa serikali

  Mengi yameongelewa hapa ila mimi nimeona nichangie katika haya mawili ambayo nadhani tunahitaji kuyafanyia marekebisho, nimalizie tena kwa kusema Naunga mkono hoja asilimia 500! Asante


  Mimi: Hivi staili kama hizi za kuunga mkono hoja hazimaanishi huenda kuna nguvu za kurogwa hapa ?
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  HAhahahaah hao ndo CCM kuna mbunge mmoja jana wa Kigoma alianza kwa kuunga mkono budget kwa 200% akaanza kulia lia oooh Kigoma imesahaulika, akatoa takwimu za pesa kidogo za kiwanja cha ndege Kigoma, kulinganisha na Songwe, Arusha, KIA, Mwanza na malalamiko mengi sana na kuishia kusema hii budget haina tija wala maendeleo akamalizia na kibwagizo anaunga mkono kwa 200%

  NB

  Kama taifa nadhani tuna wajinga wengi sana bungeni na viongozi wetu wengi ni vilaza
   
 3. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huwa wanaanza na asilimia mia, wanakwenda mpaka 10%. Kwa mtu mwenye akili timamu, ukiwa unaunga hoja asilimia mia, unatakiwa kwaachia wabunge wenzako wenye nyongeza au kasoro. Wewe unaeunga 100% unakaa kimya, hamna haja ya kuuza sura, kuongea hovyo tu. 100% maana yake huna nyongeza wala makosa. Wabunge wa CCM, wapelekwe kwa psychiatrist.
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wale wote wanaounga mkono hoja mia kwa mia, 200%, 500% lakini punde tu huanza kulalamikia mapungufu ya bajeti hiyo hiyo, wanastahili kusghughulikiwa/kusaidiwa kwa kufuata ushauri wa komba, na kwakuwa milembe haiko mbali na ukumbi wa bunge, ni vizuri spika wa bunge akafanya ze needful.
  Mkuu Masanilo nakubaliana na wewe mia kwa mia kwamba taifa hili lina watu wengi ambao ni wajinga sana na wengi wao wako bungeni.
   
 5. D

  Deofm JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mnyika pekee ndiye aliyegungua hilo, akaainisha vitu vitatu ambavyo ni Udhaifu wa Rais, Uzembe wa Bunge na Upuuzi wa CCM. lakini wale wanaojiona kuwa wana akili kubwa, kumbe hawaelewi wakamzuia asiwawafanulie maana yake. kwa alieleta uzi huu naona ni mwendelezo wa mchango wa mheshimiwa J. Mnyika.
   
 6. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  It is a symptom of psychiatric case.
   
 7. a

  andrews JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 8. peoples power

  peoples power JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 468
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Lingine jana likakurupuka na kusema linaunga mkono kwa asilimia 300%.alafu linaanza kulia kwetu hakuna hiki mara kile.sasa ulipokuwa unasema unaunga mkono hoja ninini.nyie magamba acheni unafiki na kujipendekeza haita wasaidia.
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kwanini wasishukuru mr dhaifu katoa waziri mmoja kutoka gombe huoni Hilo ni la kujivunia?
   
 10. w

  wade kibadu Senior Member

  #10
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependa speech yako.
  Hoja yangu ivi serikali inategemea mapato kutoka kwa pombe ivi itakuje kama watu watagoma kunywa pombe?
   
 11. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hio ni laana ya waislamu 2005 kwenye ilani ya jk na ccm yake waliahidi mahakama ya kadhi ilipo fika 2010 haikuwepo tena
   
 12. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  si ndio deni litafika trilioni 50 fasta! maana jamaa hawaoni hata aibu katika kukopa
   
 13. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwani hamkujua kwamba waliwaahidi ili muwape kura?
   
 14. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Satan incarnate. Maana yake shetani anashuka duniani na kuchukua mwili wa mtu. Hakika wengi wa hawa jamaa pale mjengoni ni mashetani yaliyochukua mwili!!!!!!!!!!!!
   
 15. m

  mullay Member

  #15
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanaitwa sura mbili, wanaikubali bajeti 100% at the same time wanaikosoa.
   
 16. K

  Kizotaka JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hili ni tatizo la kikatiba mkuu,ndo maana walikuwa hawataki iandikwe upya waendelee na huu uozo daima.
   
 17. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Haya Fumbeni Macho tuwaombee
  Baba waguse wabunge hawa, waguse baba, kila mtu aanze kukemea, kemeaa
  pepo wa udhaifu toka, pepo wa ujinga toka, pepo wa rushwa toka,pepo wa kushangilia mambo ya kijinga toka, nasema waachie wabunge wa ccm, waachilie, muachilie speaker, toka Pepo. Endelea kukemea, endelea

  wahudumu wasaidieni hao wanaoanguka mapepo ndio yanatoka sasa, pepo wachafu toka, pepo wa posho toka,Pepo wa uongo muachilie Mheshimiwa Pinda, Muachilieeee, navunja nguvu zote za kiccm, endeleeni kukemea jameni

  Asante baba Asante baba
   
 18. M

  Mta pter Member

  #18
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanafiki wakubwa hao!!
   
 19. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Filikunjombe naona kapigwa mkwara,jana kapooza then kaunga mkono hoja
   
 20. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Leo nimegundua ni kwanini Ngeleja hakufaa kuwa Waziri. Amelipotezea muda bunge kwa ubishi usio na tija yeyote. Huyu ni mtoro wa vikao vya Bunge. Badala ya kuwakilisha wananchi anakua ktk pombe,nyamachoma na wanawake,akikurupuka . Aibu zaidi akishangiliwa na mmoja wa wenyeviti wa bunge, Jenista Mhagama!
   
Loading...