Habari wana JF,
Nimekuwa na maswali mengi sana kuhusu utawala wa serikali ya kimabavu ya JK na bado sijajiridhisha na baadhi ya majibu niliyopata. Hivyo naomba wana JF mnisaidie kutafakari pamoja juu ya suala hili.
Suala lenyewe ni kuhusu kauli mbili za aliyekuwa spika wa Bunge lililopita na waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa sasa Mh. Samweli Sitta.
Kauli ya kwanza ni ile ya kupinga tamko la waziri mwenzake Mganga Ngeleja hadharani kwa kusema kuwa Dowans ni wizi wa kwenye makaratasi. Je, kauli ya Ngeleja haikuwa msimamo wa baraza la mawaziri?
Kauli ya pili ile ya kumpinga waziwazi waziri mwenzake wa katiba na Sheria juu ya kuandikwa kwa katiba mpya. Je, kauli ya Waziri wa katiba hakuwashirikisha mawaziri wenzake? Kama aliwashirikisha iweje Sitta atofautiane na mtazamo wao kama serikali?
Suala la kutafakari: Je, Rais mbabe JK anafahamu kuwa Sitta ameshamwasi yeye na Baraza lake la mawaziri? Na kama anafahamu mbona asitumie ubabe wake kumwajibisha? Au anaogopa nguvu aliyonayo huyu mwanaharakati?
Kufikiri ni jadi ya kila binadamu lakini uwezo wa kufikiri hutofautiana!!!!!