Mh. Rais, Wizara ya Afya ni ka "Empire" ka Madaktari, Kuna "Mfumo Daktari" Ulioota Mizizi

Mmmh!
Hapana, hapa umetudanganya.
Umekuza mambo.
Sifa za kusoma Pharmacy sio sifa za ajabu au kipekee. Kiujumla mtu mwenye sifa za kusoma MD anatoshea kusoma Pharmacy.....
Mzee Zanzibar-ASP huu ni msumari wa moto sana kwa vijana uliougongolea......huu unaitwa ukweli mchungu......tena mchungu sana.....unaweza ajiri pharmacist mmoja kwenye hospitali ya mkoa na mambo yakaenda tu vizuri,lakini hauwezi kua na MD mmoja huyo huyo na mambo yakaenda,hii inatukumbusha kua MD ni ya muhimu kuliko pharmacy.......ukifungua pharmacy ukiona umepata hela jua MD amezipata na kukutengenezea wewe
 
Mkuu ivi unajua criterial za kuisoma pharmacy wewe??? Labda nikwambie tuu

Nirahisi kupata nafasi ya kusoma MD kulipo kupata nafasi ya kusoma pharmacy....

(Nilipitia MD kupata pharmacy na nashukuru nilifanikiwa).....and am proud to be pharmacist
Your fucked up again...pharmacy pale MUHAS kupata ni kazi sababu ya competition(VYO VICHACHE)......Lakini world wide MD ni very competitive kuliko bachelor ya pharmacy......ukiweka nafasi zile zile.......MD itaanza kujaa kwanza kuliko pharmacy
 
Unanifurahisha sana brother. Ni hivi nilipomaliza kidato cha sita nilikuwa na uwezo wa kusoma kozi yoyote pale Muhimbili ikiwamo hiyo Pharmacy. Nafurahi kwamba nilichagua MD. Kwa critetia za ufaulu zinaanzia na MD then zinafuata hjzo nyingine. Kama ukiwa na qualifications za kuchaguliwa MD unaweza kusoma Pharmacy, Nursing etc ila hauwezi kwenda kinyume kutoka Pharmacy, Nursing kuja MD. Sasa huo urahisi wa kupata MD kuliko Pharmacy sijui unautoa wapi?
Narudia Tena criteria za kusoma pharmacy,ni hizo hizo za MD ubishe ukatae.


Alafu kingine pharmacist sio lazima aajiriwe hospital mkuu, pharmacist anafanya kazi sana kwenye viwanda huko analipwa Pesa ndefuu sana kuliko Hata MD.
 
Ila MD nchi hii wanaumia sana basi tu ndiyo maana ni moja ya kazi za wito, huwezi kuhangaika 6 yrs kubuild profession yako darasani halafu mtu aje akulipe 1.4m... kwa kweli lazima utafute vijiwe vya pembeni
Mfano MD akiajiriwa TAMISEMI na kada ingine,hio kada ingine ipi inakua haiumii kwa kulipwa pesa nyingi zaidi ya MD?
 
Kuna vitu ni vigumu mnoo kuvibadili kimfumo, maana chimbuko lake lina mzizi mrefu kiutamaduni. Madaktari wana some sort of Superiority complex dhidi ya kada zingine za afya. Na kada zingine za afya zina inferiority complex mbele ya madaktari. Nahisi ni kitu kilichojijenga kijamii na kukuzwa darasani wakati wahusika wakiwa masomo...
You said it all...
 
Hivi wanajua kama daktari anasoma

1. Udaktari wenyewe
2. Uongozi
3. Maabara
4. Pharmacy
5. Nursing
6. Mazingira
7. Nutrition
8. Sheria
9. Radiology
10. Usingizi
11. Magonjwa ya akili
12. Entrepreneurship
13. Utafiti
14. Psychology
15. Takwimu
16. Sociology
17. Forensic medicine nk
Kwa kutaja vichache mnaweza ongeza.

Sasa unawezaje kulinganisha na watu wengine hapa. Ndo maana tunasoma miaka mitano.

Hatusomi miaka mitano kwaajili ya kuandika paracetamol,
 
Narudia Tena criteria za kusoma pharmacy,ni hizo hizo za MD ubishe ukatae...

Unazungumzia sayari gani kaka. Umesoma kweli hiyo Pharmacy au unasikiliza maneno ya watu humu. Narudia tena MD anaweza kusoma kozi yoyote kuanzia Pharmacy, Nursing etc lakini hauwezi kutoka huko kuja kusoma MD.

Halafu usihamishe goal kila mtu anaweza kufanya kazi popote na ndiyo maana MD wako kwenye miradi na mashirika mengine mengi kama wataalam / maboss halafu manakuja kulia humu.
 
Ilikuwa inalipa zamani lakini kada inayolipa siku hizi ni maabara especially akijikita kwenye molecular biology ajue viral load testing na PCR.
Miradi mingi ya ukimwi imeajiri wataalamu wa maabara na wanapiga pesa ndefu.
Maabara kiujumla bado huwezi kuilinganisha na md kwenye soko la ajira.
Ni wataalamu wachache wa maabara wanaoweza kupata nafasi kwenye miradi mikubwa yenye kulipa fresh.

Wengi wa wataalamu wa maabara wanaishia kuajiriwa serikalini ambapo mshahara wao tunasikia ni almost nusu ya mshahara wa Daktari.
 
Civil engineer hawezi kuwa boss wa architectural engineer Kwasababu hawezi kuijua Architect zaidi ya architect mwenyewe. Issue ni team work siyo nani mkubwa, nani boss.
Umenena vyema shida ya Hawa watu wa afya ni dharau wanadharauliana sana dactari anamdharau nesi, nesi wa nyeupe anamdharau wa jani la mgomba.sasa kama dharau zitaendelea kwa kweli sioni kama Mambo yataenda.

Cha msingi ushirikiano kila mtu anathamani yake na kila mtu anamhitaji mwenzake pharmacist anamhitaji dactari na dactari pia vivyo amhitaji nurse jamani tupendane malumbano ya nini wakati wote mwajiri wenu mmoja? (Mgonjwa)
 
Huo ni "ujinga" unawasumbua ...MD hawezi kufanya kazi za kada nyingine za afya..kama ingekuwa rahisi hivyo hizo kada zisingekuwepo..don't you think?...

Matharani: Huwezi kabisa kufanya kazi ya afisa afya (Environmental health practitioner)....duniani kote iko hivyo, hakuna kichaa atamwajiri MD kwa nafasi ya Environmental health. MD.
Kama we ni afisa afya utaendelea tu kupigwa PUMBU na MD wewe na wajukuu zako.......huo ni mfumo tu.......duniani kote MD lazima awe juu ya kada zingine za afya.......maafisa afya mumejaa majungu tu na kuzunguka zunguka hila impacts yeyote.

hakuna kitu ulichosoma chuo na na MD asikijue/asikifanye. unadhani hao maafisa afya wanafanya kazi gani ya maana?_unadhani kila magonjwa yanaamhukizwa kutokana na mazingira,hapo ndio utaona MD anawazidi elimu na anawapiga PUMBU mchana kweupeee,na unadhani kubadilisha mazingira duni ya raia ni kazi ya afisa afya?
 
Mzee Zanzibar-ASP huu ni msumari wa moto sana kwa vijana uliougongolea......huu unaitwa ukweli mchungu......tena mchungu sana.....unaweza ajiri pharmacist mmoja kwenye hospitali ya mkoa na mambo yakaenda tu vizuri,lakini hauwezi kua na MD mmoja huyo huyo na mambo yakaenda,hii inatukumbusha kua MD ni ya muhimu kuliko pharmacy.......ukifungua pharmacy ukiona umepata hela jua MD amezipata na kukutengenezea wewe
Hakuna kitu kama hicho eti ukifungua pharmacy MD ndo kakutengenezea,

Unajua practice ya community pharmacy? Wewe unazani pharmacist anashindwa kufanya physical diagnosis na kumpatia mgonjwa dawa? Daktari kuwa wengi Ni haki yao I'll sipingi... kutokana na Mfumo wetu(pharmacist hapiti ward round,haangalii follow up ya mgonjwa baada ya kutumia dawa, pharmacist haakikishi compliance and Adherence kwa client akiwa wodini, pharmacist hatoi ushauri on how to reconstituting drug for better adminstration and to reduce interactions,)

Hii nchi zilizo endelea wanafanya na pharmacist wanaajiliwa wengi tuu
 
Sasa hivi MD ya Tanzania kila mtu anaweza kufanya aisee medicine ilikuwa ya zamani ya Muhimbili sio hii ya akina Udom ,IMTU habit kairukai ambayo hata khchukua history tu ya mgonjwa ni mtiha
Ni achilia mbali prescribe dawa .Medicine imebaki Jina hata mtu mwenye division 3 anasema medicine na anafauli
MD sio kuchukua history......MD ni certification..........kwa akili zako ndogo unafikiri doctor kigwangala anajua kuchukua history?
 
Sababu zenu ni zilezile miaka na miaka. Utasikia sisi tunasoma miaka mingi, sisi ndio tunatibu, sisi ndio wenye wagonjwa na blaah blaah nyingine nyingi zisizo na mashiko. Lkn naomba nikuambie dunia ya sasa imeshabadilika na hizo sababu zilikuwa za mwaka 90 kwa sasa zinapingwa kwa hoja nzito nzito.

Nilitegemea watu kama nyie mtajitokeza tuu.

Hatuwezi piga hatua kwa kuogopa kusema ukweli, ukweli utatuweka huru na tutapiga hatua.

Lkn huo "mfumo daktari" usipotolewa hii sekta haiwezi piga hatua.
Ila kusema ukweli wafamasia Ni wazinguaji kinomaaa yaani, wakiwekwa wao kuongoza wengine tegemea disaster kubwa Sana, those people are not caring hata kidogo, wacha madaktari kwa sababu zilizopo waendelee kuongoza wenzao katika afya .
 
Mtoa mada pole sana,najua maumivu unayopitia hasa kwenye huo mfumo.

Doctor of medicine ni moja ya degree kongwe ambapo mtu akiwa tu na degree ya kwanza huitwa doctor,ambapo ni tofauti na degree nyingine nyingi sana ambapo hadi uwe na degree tatu ndio huitwa doctor,pia MD anauwezo wa kusoma master of science yeyote ile uliyowahi isiskia hapa duniani.

Miaka 5+,MD hufundishwa vitu vingi sana,yaani MD husoma kazi za nesi,za mfamasia,za maabara,na hadi za afisa afya.
MD unaweza muweka popote pale na akafanya kazi vizuri tu,lakini mtu wa maabara ukimpeleka theater utahitaji umfundishe kila kitu upya.

So pamoja na p MD anakua na degree sawa na wenzake lakini ki "academic"jua amewazidi sana,maana wenzako ni bado bachelor wakati yeye ni doctor.

Hata vigezo vya TCU MD haitaji kuwa na GPA ya 4 master ili kuwa lecturer,anahitaji tu kua na MMED baaasi,tofauti na degree zingine.
Halafu specialization za MD haziingiliani na zingine popote pale duniani,yaani ili uwe na higher medical education level/specialization ni lazima uwe MD.

Huu ni utaratibu tu wa dunia nzima ndio mana hata marekani among higher paying job ni MD ,hata Tanzania MD anaanza na mshahara mara mbili ya mwalimu mwenye masters.

Yaani pesa ambayo serikali inamkopesha MD kusoma kwa mwaka mmoja tu,unasoma degree ya environmental science miaka 3 hadi unamaliza na chenji inabaki.

Hawa watu hawawezi kua sawa. MD ana advantage ya kuziba nafasi za kada nyingine ya sayansi sababu yeye anaweza soma vitu vingi/master kwenye elimu yake ya juu.

Hata wewe uwe rais kati ya pharmacist mwenye PhD na MD mwenye PhD yupi utamchagua kua waziri wa afya?,kua mkweli hapa?
Kati ya environmental scientist mwenye PhD na MD mwenye PhD huku master ana MPH yupi utamchagua kua mkurugenzi wa Tiba pale wizara ya afya?

Yaani mfumo wa kidunia una mfavor zaidi MD kuliko kada ingine,haya mambo ni vema wanafunzi wangeyajua hata kabla ya kuanza shule.

MD ndio anamsababishi nesi,mtu wa maabara na famasia wafanye kazi.....yaani yeye ndio anainitiate matibabu,

MD anaweza toa huduma ya afya/kujikinga na magonjwa,wakati mtu wa environmental health hawezi toa huduma ya tiba
Ameelewa bila shaka...
 
nakuwekea kabisa na screeshot, hata nesi ni mwana afya sijui kama unajua hilo achilia mbali mtu wa maabara, mtu wa maabari hawezi shindwa muongoza daktari (MD), kozi za ungozi zipo na hua zinatolewa! walio tofautisha huyu ni MD, Mfamasia, mtu wa maabara SIO WAJINGA...
Sasa kwa hio definition huoni kua MD yupo wide zaidi.....it covers DX,treatment na prevention......means MD anajua kazi za labs/radiology, anajua kazi za pharmacist etc za afisa afya.....wakati pharmacist ye hasomi mambo mengine hayo zaidi ya dawa zake,afisa afya hasomi treatment zaidi ya prevention.......kwa akili yako ndogo unadhani nani anafaa kiongozi kati ya hao?
 
Mfamasia na doctor of medicine ni watu wawili tofaut doctor of medicine jawa ndio wanaobun madawa wana priority zaid hao mafamasia wanaklemishwa tu majina ya madawa tu nipe asprin ndio anachojua yeye
Anabuni vipi madawa hata Drug discovery hajasoma?

Au unamaanisha kumuandikia mgonjwa dawa?
 
Back
Top Bottom