Nobunaga
JF-Expert Member
- Mar 22, 2019
- 1,169
- 4,985
Kwanza kwa heshima na taadhima nakusalimu na kukupa pole Mh. Rais kwa kazi nzito ya kuwaongoza Watanzania na taifa kwa ujumla.
Mimi sio mwandishi mzuri sana Mh. lakini naomba nikupe hints chache tu ili ujue na watu wajue ni kwa jinsi gani humo wizara ya afya kuna ki empire kimejengwa ambapo kwa namna moja ama nyingine kina negative impacts kwa jamii.
Kwanza kwenye wizara, nafasi za juu pale, yani top layer karibia yote wameshikilia Madaktari, hakuna kada nyingine japokuwa wana vigezo sawa na hao Madaktari.
Tukiachana na waziri pamoja na naibu wake ambazo ni nafasi za kisiasa (lakini wote ni Madaktari), nafasi zingine za juu pale wizarani zimekaliwa na Madaktari pia. Directors karibu wote ni Madaktari.
Ukija kwenye hospitali zote pia wakuu wake wanakuwa ni Madaktari. Sidhani kama kuna hospitali hapa nchini mkuu wake ni kada tofauti na udaktari. Mh. tukumbuke uongozi ni nafasi ya kuteuliwa haihitaji uwe umesomea kada fulani bali uwe na ujuzi na uwezo wa kuongoza. Lakini huko mahospitalini automaticaly Madaktari wameshajiwekea dhana kwamba wao ndio wanapaswa kuongoza hospitali. Hakuna cha muuguzi, mfamasia wala mtaalamu wa maabara anayeruhusiwa kuongoza hospitali hata awe na sifa sawa na daktari.
Sio kwamba napinga wao kuwepo hapo, hapana. Ila najaribu kuwaza tuu ina maana kada zingine hamna wenye vigezo vya kushika hizo nafasi mpaka wao tuu washike.
Huu mfumo umepelekea maamuzi mengi sana yanafanyika kwa upendeleo na Madaktari wanapeana favor zaidi kupita kada zingine. Angalia hata nafasi za kusoma level za juu wanaopata ufadhili wengi ni Madaktari.
Pili, kutokana na "mfumo daktari" huu hapo wizarani, umepelekea wao kujiamulia mambo wanavyotaka bila kuogopa sababu wanajua hapo juu yupo wa kuwatetea hivyo hawagusiki.
Mathalani, ukienda hospitali nyingi za umma kwenye inpatients wards Madaktari hawakai kabisa. Wakishapita ward rounds ile asubuhi kufika saa sita wanakuwa wameshapotea wanabaki wauguzi tu. Hata ikitokea dharura yeyote wanaohangaika na mgonjwa ni wauguzi, na wagonjwa wengi sana wanafariki bila daktari kuwepo, mgonjwa akishafariki ndio daktari anaitwa kuja kuidhinisha kifo na sio kumuokoa mgonjwa. Mida ya usiku ndio hali ni mbaya zaidi kwani hata daktari akiitwa kuja ni mpaka asubuhi.
Tukija kwenye scenario ya huyo daktari aliyekimbia hapo Tabora na kwenda Dar, kwanza kwa upande wangu Mh. naona kama amefanya fair kuweka wazi kaacha kazi. Mh. Rais naomba utambue 80% ya Madaktari wa hospitali za umma wana vijiwe.
Na hivi vijiwe ndiyo wanavipa priority zaidi kuliko vituo vyao rasmi vya kazi. Asubuhi wakishapita round huko vituo vyao vya kazi basi kuanzia mida ya saa nne/tano wanaenda huko vijiweni (private hospitals) ambako wanakaa full-time. Sasa mimi naona bora huyu aliyeacha kabisa kuliko hawa wanaoendelea kula kodi zetu kwa geresha tuu huku muda mwingi wakiutumia huko private.
Pia hawa Madaktari kingine kibaya zaidi wanachofanya huwa ni kuhama na wagonjwa kutoka hospitali za umma na kwenda nao huko vijiweni kwao. Mfano anaweza kuja mgonjwa kwenye hospitali ya umma akaonwa na daktari, lkn ataambiwa kwa vipimo na huduma kamili tuonane siku fulani kwenye hospitali fulani. Wakati anachoenda kufanyiwa huko private hospital pia kinafanyika kwenye hiyohiyo hospitali ya umma. Wanachoahidiwa huko private ni kwamba ukileta mgonjwa basi unakuwa na "cha juu".
Lakini haya yote hakuna wa kuyachukulia hatua madhubuti sababu kwenye uongozi mzima wameshikilia wao kuanzia wizarani mpaka huku chini kabisa. Hawa kada zingine hata wakijaribu kupeleka malalamiko wanaishia kuzimwa maana kote kuna "mfumo daktari".
Hivyo Mh ukitaka kuiponya hii sekta ya afya anza na kuvunja vunja huu "mfumo daktari" kwanza ndio tutapiga hatua kwenye hii sekta.
Ni hayo tuu kwa sasa Mh. Rais.
________________________

1. Sina 'farasi' kwenye mtifuano huu.
2. "Nasikia" zamani Madaktari walikuwa wakipenda Waziri wa Afya awe mtu ambaye "siyo" daktari (MD) kwa vile huwa "mnyumbufu" zaidi katika kushughulikia masuala yanayohusu madaktari. Sijui siku hizi kukoje.
3. "Nasikia" hospitali fulani iliwahi kuleta mkuu wa hospitali Mzungu. Ukazuka mjadala wa kwanini/kwinini . Wakaambiwa tunataka mtu mwenye digilii ya "Hospital Management". Hakuwapo kwa wakati huo, na Mzungu akapeta!
4. "Mfumo-Daktari" kwenye afya; "Mfumo-Wahadhiri" kwenye taasisi za elimu ya juu; "Mfumo-Mwanasheria-Msomi" kwenye kada za kisheria; "Mfumo-Wahandisi" kwenye baadhi ya kada, pengine ni vitu ambavyo vipo. Tatizo kubwa Afrika ni "Menejimenti". "Menejimenti" haijaweza bado kuonekana ni fani inayojitegemea, na kwamba mtu yoyote aliyeweza kufikia viwango vya vigezo na masharti ya "Menejimenti" angeweza kuonekana sawa na mwenzie aliyetimiza vigezo na masharti --- bila kujali ilmu zao za awali. Pana taasisi mashuhuri iliwahi kuletewa "Menejimenti" nzima ya kukodishwa ili kuboreshwa. Hili ni jambo la kawaida kutokea baadhi ya taasisi, hasa nchi za mbali. "Management-For-Hire".
Hitimisho: "Kasungura" kenyewe kadogo ... kila mmoja anataka aweko "jikoni" kwenye kazi ya "kutenga" kwenye "sahani" nani apate nini, lini na kwa nini. Menejimenti kama utaalam (Profession) iheshimiwe -- nafasi za menejimenti zisijali kwanza kuhusu usuli wa taaluma ya mtu, kabla ya kuangalia Utaalam wa Menejimenti.
Mkuu kwanza neno MEDICAL halina maana ya "Udaktari"
Mwanafunzi aliyehitimu masomo yake ya "Udaktari" ambaye ana degree yake moja huyo kiufasaha kabisa katika kada ya afya anatambulika kama GENERAL PHYSICIAN (GP)
GP ndo title sahihi kabisa ya madaktari wetu ambao wana wamemaliza masomo yao ya degree ya kwanza na jukumu lao kubwa ambalo linawatofautisha na kada zingine ni ubobezi katika kufanya diagnosis.
Kiufupi Kada za afya zina compliment to each other.. Yaani kila kada inamtegemea mwenzake kwa huduma bora zaidi za afya.. Ndo maana kuna term inayoitwa MEDICAL PERSONNEL ikimaanisha mjumuiko wa wataalamu katika mfumo Tiba.
Ukisema medical officer lazima awe daktari kwa kigezo cha uwepo wa neno medical katika iko cheo haupo sahihi 100%
Medical officer can be any medical personnel ambaye ana qualifications za hiyo post kwa mujibu wa taratibu ambazo wahusika wataona inafaa ila hauwezi kuipa hiyo post by default kwenda kwa madaktari kisa tu kuna neno medical ndani yake.
wale wahuni Hadi idara za preventive services wanajustify kuwa wao ndio wanafaa kuongoza kwa hoja ya kuwa huwezi kuzuia kitu ambacho kikitokea huwezi kukiondoa
Hadi idara ya epidemiolojia wanajustify kuwa huwezi kuongoza idara ya namna ya kudhibiti kuenea kwa magonjwa wakati hujui magonjwa
Hadi idara ya Tiba ya asili wanakuambia huwezi kuongoza idara ya Tiba ya asili wakati hujui Tiba
Hadi idara ya mafunzo watakuambia huwezi kuongoza idara ya mafunzo yenye mafunzo ya udaktari ndani yake wakati wewe hujausoma wakati wao wanasoma vyote vya Afya
Hadi idara ya elimu kwa umma wanakuambia huwezi kuongoza idara ya elimu ya Afya kwa umma wakati hujui afya ya binadamu vizuri kama wao
Hence
Idara zote wanaongoza wao isipokuwa zile ambazo zipo specific Kama idara ya uuguzi na ukunga,Idara ya madawa na vifaa tiba na idara ya rasilimali watu