Mh. Rais nipatie tu perdiem nipite kwa watanzania niwaeleze mambo haya

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,361
11,518
Naomba nami usinisahau ktk ufalme wako. Nimeona mambo makubwa uliyoyafanya mpaka nawaza ulikuwa wapi toka awamu ya kwanza? Una mazuri yote....huna baya mama. Huna baya na mtu. Umeifungua nchi sana.

Naomba tu niweze wezeshwa nauli na malazi nipite nchi nzima kuelezea mazuri yako na kule tulikotoka. Nchi imebadilika sana. Naona pesa kwa sasa ipo. Ipo sana. Watu wanapata pesa na wengine wanapata fedha wengi tu. Mama huna baya...mtu ashindwe mwenyewe tu.huna roho mbaya.

Kuna wakati natamani nami ngekuwepo katika wale wenye vyeti fake. Nilipwe. Maana kuna vyeti original mpaka sasa hakujanisadia chochote.

Nchi hii tulicheleweshwa sana. Miaka 5 magufuli hakuna alichofanya. Hakuna nchi ilisimama kabisa. Ila wewe tunaona kazi. Na Rais wa China amekukubali sana. Kakualika uende kwake. Hakuwahi taka mwalika Magufuli.... Ila wewe kakualika. Una nyota mama. Una nyota. Wacha watu waitumie nyota yako.

Mimi sitaki mengi. Nataka tu nipite niwaelezee watu waache ujinga wa kumfikiria mwendazake. Wakutizame jinsi ulivyobadilisha maisha yetu watanzani, wananchi na viongozi wetu. Niwaeleze mazuri yako mpaka sasa. Watu tupo huru. Mbowe yupo huru kwa sasa. Umemtoa ndani. Anakula nchi. Zitto ndo asalamaleko wallah apewe nini? Na wapinzani wengine wanakukubali.

Hawa akina Maria Sarungi ni njaa tu na habari zao za katiba. Katiba siyo issue. Hata mbowe nadhani kwa busara zake egundua hilo. Wala haangaiki nalo tena. Huna baya mama. Huna baya. Basi naomba unisaidie nipite huko na akina makamba na akina nape tuelezee utukufu wako.
 
Back
Top Bottom