Mh. Rais, mpandishe cheo askari huyu kwa uthubutu wake

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
1,692
Kuna clip inasambaa kwenye mitandao inayoonyesha askari wakimwokoa mtoto toka mikononi mwa mzazi wake aliyedhamilia kumdhuru.

Wanao onekana ni askari wengi, lakini kuna askari mmoja mwenye uthubutu aliyetumia weledi mkubwa kumrukia mtuhumiwa ndiyo nashauri mamlaka zimpandishe cheo.

Amefanya kazi kubwa ya kuokoa maisha ya mtoto aliyetakiwa kukatishwa maisha yake, .
Kwa kweli alijitoa mhanga, kama kazi yake inavyotaka

Mh. Rais atakuwa ameona tukio nzima, Kwa kweli askari wetu wanachapa kazi sana, hata wanao wabeza wanakosea sana
 
ibesa mau,

Mkuu sihoji juu ya uthubutu na utu Wema wa yule askari kitu nitakachohoji ni

1. Umesema yule baba alikuwa Anataka kumdhuru yuke Mtoto, una uhakika na hilo. Je vyombo Vya usalama vimeshathibitisha kuwa yule baba alitaka kumdhuru yule Mtoto?

2. Amefanya kazi kubwa ya kuokoa maisha ya mtoto aliyetakiwa kukatishwa maisha yake. Huu ni uzandiki na uzabizabina maana huna uhakika na unachosema n yule mzee sikuona jitihada zozote za kukatisha uhai wa yule mtoto..zaidi tu alikuwa anawakwepa askari wasimchukue yule Mtoto. Mkuu acha mamlaka zinazohusika zishughulikie lile tukio na majibu ya uhakika tunaweza kuyapata...tuache speculations za kizandiki.
 
Jamaa mwenyewe akunuia sana kumuua mtoto, askari wenyewe wanashauriana dk 1 nzima, inawachukua tena sekunde za kumwaga kumfikia mtuhumiwa na sekunde nyingine nyingi tu kumkwapua mtoto.


Huyo Jamaa kanisikitisha sana alivyotoa hukumu ya moja kwa moja.
 
hebu tone hiyo clip...

mi naskiaga tu watu mkisema kuna clip zinasambaa sjui voice record ila kwakweli hazinifikiagi kbsa,nyie mnazipataje? ebu namm nifundshen chakufanya nisipitwe.

hiyo clip sijaiona mkuu,nifanyie wepesi....
Ili uwe wakwanza kupata yote yanayo jiri mjini, ebu tenganeza connection mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mmoja alimpiga mtuhumiwa kichwani na kitako cha bunduki.... Huyu naye vipi? Afukuzwe??


Hata na Mimi nilishangaa sana maana walikuwepo askari zaidi ya watatu...INA maana walishindwa kumdhibiti yule bwana mpaka Jamaa akampiga na Kitako cha bunduki...tena kichwani...Je akienda kupimwa ikaonekana ameathirika kiakili kutokana na kile kitako cha bunduki hapa kesi itakuweje...maana tayari kuna tarifa kuwa yule bwana hakuwa sawa kichwani. Sasa hapo tutayofautishaje kati ya madhara ya kitako na madhara ambaye yalikuwepo tangia awali.
 
Back
Top Bottom