kama kawaida ya wabongo wangetwambia bahati mbaya rais kaumia.
http://www.dailynews.co.tz/pics/11_09_hmaerh.jpg
Kumekuwa na maoni mbalimbali kuhusu picha ya Rais akiwa kwenye bembea Jamaica. Mimi binafsi nimejiuliza maswali kadhaa juu ya jambo hilo.
Kubwa kuliko yote ni potential threats to the president's personal safety kwenye lile tukio. Kwenye ile picha, tumemuona Rais wetu mpenzi na Mama Salma Kikwete wakiwa na maafisa wawili wa Jamaica kwenye bembea.
Swali la kujiuliza ni maafisa wa Usalama wa Taifa wa Tanzania (yaani Tanzania Intelligence and Security Service) walikuwa wapi? Moja ya kazi muhimu sana ya Usalama wa Taifa ni kuhakikisha kuwa Rais anakuwa salama wakati wote. Hii ni pamoja na kuchukua tahadhari ya hatari zote zinazoweza kutokea na kuhakikisha kuwa kuna askari wa Usalama wa Taifa hatua chache ya kila mahali ambapo Rais anakuwepo in public.
Je, Rais angeteleza, kupata shambulio au kuishiwa nguvu ghafla akiwa juu ya bembea iliyokuwa hatua nyingi kutoka ardhini, Usalama wa Taifa wangepaa juu kumuokoa au wangemdaka kabla hajadondoka chini?
Je, Usalama wa Taifa walishindwa nini ku-insist kuwa mmoja wa maafisa wa Jamaica watoe nafasi ili askari wetu apande juu na kuweza kutoa ulinzi kwa Rais na Mama Salma wakiwa kwenye bembea?
Tena wakiwa juu ya bembea, sijaona hata kama kulikuwa na mikanda ya kuhakikisha usalama wa kiongozi wetu mpendwa.
Kazi ya Usalama wa Taifa ni kutoa "physical protection" kwa Rais popote anapokuwa. Je, Rais alipokuwa kule juu kwenye bembea, Usalama wa Taifa walikuwa wanatoa physical protection gani kwake?
Nimejaribu kudodosa kwenye Mtandao kuhusu Secret Service ya Marekani ambayo ina jukumu la kumlinda Rais Obama na viongozi wengine wakuu.
"In general, permanent protectees, such as the president and first lady, have details of special agents permanently assigned to them. The protection of an individual is comprehensive and goes well beyond surrounding the individual with well-armed agents. As part of the Secret Service's mission of preventing an incident before it occurs, the agency relies on meticulous advance work and threat assessments developed by its Intelligence Division to identify potential risks to protectees."
Je, Usalama wa Taifa walifanya threat assessments gani kabla ya kumruhusu Rais apande kwenye bembea bila ya ulinzi wa karibu?? Ni Kudra tu za Allah kuwa alituepusha na janga. Kama Rais angeishiwa nguvu akiwa juu ya bembea kama ilivyotokea Mwanza, ingekuaje?
Kwa maoni yangu kama layman wa maswala ya Usalama wa Taifa, THIS WAS A VERY SERIOUS SECURITY BREACH!
Bahati nzuri "hakuchoka" kama Mwanza.Kama mzee mwinyi alipigwa kofi na wao wapo ije jk kuanguka kutoka kwenye bembea? Angetua chini kama nazi
Naona wamepelekwa kwenye bembea za chekechea huku jamaika anadanganywa kuwa ni kivutio cha watalii
Pia unatakiwa kukumbuka kwamba Bushi alikuwa likizo wakati jamaa yetu yuko kule kikazi ingawa hatujui hasa ni kazi ipi!!!!
Kuna swala moja naona kuna watu humu dani wanali shikia bango sana. Nadhani hilo lina tokana na ufahamu mdogo. Kuna watu wana sisitiza kwa nini counterpart wake kutoka Jamaica hakupanda. Kwanza mutambue kuwa kiongozi wa nchi hawezi kuacha kufanya shughuli zake kisa kuna mgeni. Kwa hiyo kiongozi fulani akienda nchi nyingine haimaanishi atakua na mwenyeji wake 24/7. Raisi mwenyeji anakua na ratiba zake na mgeni nae anakua na ya kwake siyo kwamba wana ongozana kila sehemu.
labda inategemea ni rais wa wapi na ameenda kule kufanya nini na kwa muda gani. angekuwa rais wa Marekani 'n the like labda shughuli zingine za rais zingesimama mpaka aondoke....
Sio mchezo Raisi tunaye!