Mh Rais amemgundua mnyama mkali TRA

Mh Rais amemgundua mnyama mkali TRA

Na ukichunguza wafanyakazi wa tea wengi hata biashara ya nyanya hawajui hata inavyofanywa in practical ila wanakesha kuua za wenzao
 
Let's examine the facts on the ground. Kama unaamini mtazamo wako, kumekuwa na mabadiliko ya mawaziri na makamishna wa TRA mara ngapi tangu 2015? Kwa mtazamo wako, Hali inakuwa nzuri au mbaya zaidi?
I rest my case.
Suala la TRA ni confusions nyingi sio tu kiongozi... ni pamoja na utamaduni, watoto wa vigogo na attitude ya wakusanya kodi kuwa kodi ni adhabu...
Ama uko sawa ama siko sawa ila kupata mtu atakayemudu TRA kwa masrahi mapana na kuzuia rushwa na kero ni bahati
 
Mnafahamu kuwa makusanyo mengi ya TRA hayafiki serikalini na wengi wanatoa rushwa ili walipe less ama wasilipe kabisa..
Hata kama wanatimiza majukumu yao ... njia mbovu wanazotumia ndio zinaumiza biashara..
Ila kwakuwa tunamchukia kwa kumpenda JPM lazima tumsukumie lawama zote na ili tufanane na wanasiasa bingwa... you know...
Unazunguka mno. Nitashangazwa zaidi kama mkuu hakuwa anafahamu. Kwani hajawahi kuwa na biashara? Au labda kwasababu kipindi cha nyuma wa ccm na viongozi wa serikali, biashara zao TRA sidhani hata kama wanawalipisha kodi. Wale wafadhili wa chama nao hawalipi. Kwa kiasi kikubwa hilo limeota mizizi na kila mtu analifahamu, nina uhakika hata rais anafahamu.

Kule TRA hata wafagizi wana uwezo kuliko wajasiriamali.
 
Muda wa mavuno (UCHAGUZI) umewadia , hizi semina elekezi mtazisikia sanaa. Mtaitwa nyie ndio mabalozi, nyie ndio wenye nchi hii, nyie ndio mmeniweka madarakani, nyie ndio mmenichagua, hivyo mimi nawatumikia nyie, na maneno kama hayo, watu wanahamishwa idara, kwa muda na wanarejea baadaye kwa style mpya, hiyo ndiyo siasa.
TRA, na Polisi wanatumika kuwasafisha wakubwa, jana mmeona kakana kuwatuma isipokuwa alimtuma LUKUVI peke yake, lakini hawa TRA alio kuwa akiwahimiza wahakikishe wanakusanya kodi, na tunakumbuka kuna wafanyabiashara waliambiwa wafunge maduka na waondoke lakini jana tumesikia tofauti, Serikali ilikuwa hamtumi mtu, wao vwatawala ni wasafi isipokuwa TRA ndiyo wabaya sana hawa hahaha, Ngojeni mkiisha jaa upepo mkawachagua mtaona muziki wake tena, maana binadamu wepesi sana kusahau, akiumwa njaa siku tano, siku ya sita akila akashiba anasahau mateso ya zile siku tano zilizopita, tunasema yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Watanzania muwe nakumbukumbu, msidanganywe kirahisi hivyo.
Leo wamekataa katakata kwamba siyo wao kabisa hahaha, yangu macho mtakuja kukumbuka, mtaanza kuandika humu kwa uchungu, kazi yetu kusoma tu.
 
Yale ni maigizo tu, TRA wanachokifanya ni maelekezo / shinikizo toka juu! kila mwezi wanawekewa malengo ya makusanyo na Serikali ni wakali kweli kwa TRA wanapolegalega kukusanya ushuru.

Huko nyuma ya pazia shinikizo la kuwataka wawe 'aggressive' linatoka juu na wao wanatii, njia pekee ya kufikisha malengo ni kuwa wakali na kutoa makadirio makubwa ya kodi kwakuwa walipaji na walewale.

(japo ni kweli kuna tatizo la rushwa, ambalo sio la TRA peke yao bali ni Serikali yote)
Maelekezo ni kukusanya kodi na kufika malengo sawa kabisa. Shida inakuja pale fisa wa Tra anapotumia hayo maelekezo kujipatia rushwa. Atakutisha na maelekezo kisha anakupa makadirio ya juu na baadae mnaongea na hatimae unaambiwa 15mls weka mezani nazilizobaki kalipe
Hilo ni kosa la maelekezo..
Kama wafanya biashara wanakili kulipa nusu kwa nusu utasingizia maelekezo???
 
Kwa mfumo uliopo wa TRA, nchi haitapata maendeleo, bali watu wachache wachache.
 
Back
Top Bottom