Nina shaka hawa ulio watupia hii hoja yako ni wale wale ama wanafaidika na huo utaratibu wa rushwa kwenye ofisi za TRA au ndio wapokeaji wa hizo rushwa Direct.
Sabbu wengi wa members humu ndani ni watumishi wa serikali.
Haingii akilini Rais anaonesha kusikitishwa na uovu wa watumishi walio chini yake, anaagiza hatua kali zichukuliwe juu ya wale walio fanya huo uovu halafu unamsikia member wa humu ndani anamtuhumu Rais huyo huyo alie agiza hatua zichukuliwe,
Bila shaka kuna ndugu za kina " Kilua steel " humu JF bila shaka hata wale walio mnyanganya yule mfanyabiashara mzigo wake tangu 2015 japo walijua si sawa wapo humu JF na hata wale walio waweka ndani wafanyakazi wa pale tumbaku Moro huenda nao wapo humu ndani kwa utambulisho bandia.
Na bila shaka wao ama ndugu zao ndio hao wanaomtukana na kumkashfu Mh, Rais kwa hatua hizo alizochukua, je mnataka afanye lipi ili roho zenu ziwe na furaha,?