Pesa zabure baibai hakuna kuongeza sifuri mbele Hapa kazi tu. Mtanena sana kwa lughaSiku utakapo toka kwa wazazi nakuacha kula ugali wa shikamoo. Ndo utaelewa alicho kiandika mleta mada.
Sisi machinga na mamantilie pesa za bute tuzipate wapi ndugu ysngu? Bure ni kwenu mlioko maofisini serikalini huko! Acha kukebehi maskini ndugu yangu hata km unashibe sana!Pesa zabure baibai hakuna kuongeza sifuri mbele Hapa kazi tu. Mtanena sana kwa lugha
Ukisoma hii utafahamu. wadanganyika tumezoea kuambiwa na kuamriwa na watawala tufunge mkanda.Kukaza mkanda bila umakini, utajiumiza!
Hakuna kitu huko mbele hiyo sahau, ulikuwa unauwezo wa kulipia watoto 3 academy kwa hali ilivo sasa unashindwa baada ya biashara kudorola halafu bado unasema utalia juani.Mheshimiwa rais Magufuli, hakuna kulegeza kamba, wembe ni ule ule hata kama watu walie namna gani. Hata waisrael walipokuwa njiani kuelekea nchi ya ahadi walilia lia hivyo hivyo wakamlaumu Musa na hata kumnung'unikia mwenyezi mungu, lakini hatimaye walifika. NI HERI TUKAPATA SHIDA SASA NA HAPO BAADAYE TUKAISHI KWA RAHA. Mchumia juani hulia kivulini.
Ulikuwa na katenda kakukusanya ushuru leo unaambiwa hapana tutakusanya wenyewe, kwa maana nyingine umefukuzwa kazi halafu bado unasema fanya kazi halali utapata hela.Mzunguko wa pesa haukwepeki,lakini bahati mbaya pesa ilitokana serikali kulipia huduma hewa,au ambazo hazina umuhimu.Kwa lugha nyepesi mzunguko wa pesa hasa miji mikubwa kama Dar ulitokana na serikali kuchapa usingizi.Jibu ni kujipanga upya fanya kazi halali upate ujira halali
Hapana alikuwa agawi pesa ila alikuwa anajua matumizi ya pesa
Unaonae! Kuna watu hawalielewi kanisa hili!Jamaa anasema tufanye kazi,mimi naamka alfajir kwenda job na kurudi saa tatu usiku,hela haipo,wateja wanalalamika,sasa tufanye kazi gani kila mmoja anasema hali mbaya.Jpm kaa na wachumi wako achia pesa iingie
mitaan
MMEYATAKA WENYEWE,,,,AIBU YENU MILELE..............Kwa muda sasa serikali imekuwa haiachii pesa iingie kwenye mzunguko kwa kigezo cha kubana matumizi. Pesa inakusanywa lakini hairudishwi mitaani ili mzunguko uendelee na uchumi ukue.
Serikali imebana sana au kuondoa kabisa matumizi ya fedha kama katika kutoa tenda mbali mbali, kukodi kumbi za mikutano na makongamano, n.k. Kwa ujumla serikali imeishikilia pesa.
Matokeo yake sisi watu masikini ndio tunaumia. Vibiashara vyetu vidogovidogo vimekosa mnunuzi, bia bar haziuki, n.k.
Kubana pesa na kwenda kuzinunulia ndege, au kujengea mabarabara sawa, lakini impact yake kwa sisi masikini ni ndogo. Kuhamia dodoma sawa, lakini impact yake kwa sisi masikini, machinga na mama ntilie ni ndogo.
Mh ebu achia pesa iingie kwenye mzunguko kama kawaida cha msingi tu matumizi sahihi yazingatiwe! Kuna tetesi kutoka Hazina kwamba umeamua kushikilia pesa kwa hofu eti ukiyoa mafungu kama budget ilivyopitisha zitaliwa na wafanyakazi hewa n.k! Inasemekana unalipa tu mishahara na kugharimia mahitaji ya lazima ya wizara, hela nyingine yote unaizuia.
Hebu pia kaa na wachumi wako mjaribu kutatua hii hali hii mapema. Wananchi watashindwa uvumilivu.
Hii hali ikiendelea usishangse watu wakaamua kuingia mitaani bila hata kuchochewa kulalamikia ugumu wa maisha. Haiwezeksni kila unayeongea naye analalamikia ugumu wa maisha.
Mh achia hayo matrilioni yaingie mitaani. Halafu baadaye utayakusanya tena yarudi serikalini. Ndivyo uchumi wa nchi maskini unavyoendeshwa. Hali ni mbaya huku mitaani, haviuziki, havinunuliki! Tutafika kweli? Unatuumiiza sisi maskini mheshimiwa.
Kama kuna kitu kitafanikisha UKUTA kwa kiasi kikubwa ni hili la ukata na ugumu wa maisha, ambalo wengi wanasema wewe ndio umesababisha, na wala sio hili la kuminya demokrasia! La kuminya demokrasia nalo ni kubwa lakini kwa sasa watu wengi wana hasira kwasababu ya ukata unaoaminika umesababishwa na sera zako za kukurupuka.
Ndio hiyo waswahili husema inzi kafia kwenye kidonda.Lakini mkuu usikate tamaa kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi,kufungiwa njia mmoja utatafuta njia nyingine labda ndio subcontractor wa Bomba la mafuta la Uganda,au Ujenzi wa Reli ya kati n.kUlikuwa na katenda kakukusanya ushuru leo unaambiwa hapana tutakusanya wenyewe, kwa maana nyingine umefukuzwa kazi halafu bado unasema fanya kazi halali utapata hela.