Kiwewe
Senior Member
- Nov 22, 2011
- 159
- 51
Mh. Saada Mkuya Salum, Mwigulu Nchemba na Dr. Shukuru Kawambwa, tafadhali tunaomba mtusaidie sisi wanafunzi wa shahada ya uzamivu tuliopo kwenye vyuo mbalimbali nchini Ujerumani. Tupo kwenye mpango wa elimu unaoratibiwa na DAAD ujerumani (20%) na Wizara ya Elimu Tanzania (80%), Sasa tumeanza mwezi wa pili bila kupata pesa za kijikimu. Kwasasa wengiwetu tumeathirika vibaya hasa kutokana na utaratibu wa kimaisha huku. Tumeshindwa kulipia pesa za pango, gharama za mwezi za usafiri, mawasiliani/internet, heating system, utupaji wa takataka, muhula wa semester inayokuja mwisho wa mailpo ilikuwa Januari nk. Hali hii imepelekea wengine kushitakiwa na kupigwa faini kubwa sana. Wengi wetu sasa tumeshindwa kuendesha shughuli za elimu, tumekuwa tukiokota chupa for recycling angalau tupate pesa ya mkate ili tusife njaa.
Tunaomba mlishughulikie tatizo letu kwa haraka ama kama programu hii imeshindikana, basi tunaomba mtujulishe na mtusaidie nauli za kurudi majumbani kwetu haraka kuliko kuadhirika huku ughaibuni. Tumeshapoteza kabisa matumaini kutokana na ahadi hewa tunazopewa na watendaji wa wizara zenu. Tukiwauliza wizara ya ELIMU wanasema hawajapewa pesa kutoka HAZINA kwasababu kuna uhaba wa pesa na sisi hatupo kwenye kipaumbele. Tunatambua kuwa Mh. Mkuya na Mwigulu ni wanafunzi wa shahada ya uzamivu pia, ila kusomea huku ughaibuni hasa nchini Ujerumani ni vigumu sana kufanya shughuli nyingine za kupata kipato sambamba na darasa hasa ukiwa unapewa pesa na DAAD. Tunaomba muelewe hali tuliyonayo na mchukue hatua maramoja.Mh