Mh.Freeman Mbowe wa CDM ndiye huyu ?

MPAMBANAJI.COM

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
712
331
Ni kitambo toka afahamike kama mtu machachari na anayejiamini na msimamo endelevu kwa manufaa ya wengi

Hakika ni wachache wenye ujasiri huu, au kuishi ndani ya siasa bila kuchuja kwa muda mrefu kama alivyo kamanda huyu.

Mh. huyu kwa sasa ameanza kugusa wengi hususani wazee na vikongwe ambo awali walikua waogopa upinzani hususani baada ya kujiimarisha katika kutoa hoja na kuzitetea kwa kujieleza kwa umahiri mkuu.

Kaka Mbowe kwa sasa anaonekana kuwa ameiva katika kufikisha ujumbe kwa makundi mbalimbali...hu ndio uongozi kaka yangu.

Nimekufuatilia toka january mwaka huu hadi sasa...kwa kweli umenikosha kwa staili yako nzuri ya siasa na uwezo wakuteka mass... heko kwa hili

Lamsingi hapa tunamwomba Mh. awaelekeze baadhi ya makamanda wa juu yuu ya umuhimu wa siasa zipendwazo ambazo kwa kweli hapa CHADEMA wanasimama kama wanaharakati wa Taifa hili changa ila lililozeeka kwa ukosefu wa ubunifu wa maendeleo ya kweli.

Kuna aliyevuliwa ubunge kule kaskazini, anaonekana kuwa bado na siasa zenye madoa kidogo lamsingi hapa awateke vijana au sijui ni kwamba ni nia ya Chama kujaribu kuteka watu wa kada mbalimbali kwa wasifu mbalimbali.

Je hapo alipo pametosha au tusubiri mengi mazuri toka kwake ktk elimu ya M4C?

Bravo HQ Leaders.......peoplesssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssssss''''sssssssssssssssssssss'
 
Mimi kanikuna zaidi recently kwa namna alivyolizima zimwi fake la harakati za urais ndani ya Chama. Yaani kasababisha nianze kufikiria kumsahau Mwalimu Nyerere. Kanithibitishia kwamba wapo watanzania wenye uwezo wa kukabiri hoja mfu zilizopakwa rangi za samawati kwa hoja badala ya kuzikimbia kama alivyotuzoesha Amiri Jeshi Mkuu, Rais, Alhaji, DR, Kanali na Mwenyekiti Kijana wa Chama cha Mapinduzi.
 
Kwa kuongezea tu uliyoyasema,
Ni kamanda mbunifu wa matumizi ya ndege, ccm wakamzomea, mwisho nao wakalazima kuiga ubunifu wake.
Ni kamanda aliyeanzisha M4C arusha na sasa zinatikisa nchi nzima.
Ni kamanda wa aliyeanzisha sare za chama.
Kwa ujumla ubunifu wake ndio imekuwa nguzo muhimu kwa ukuaji wa chadema. Bravo.
 
Mimi kanifurahisha jinsi anavyokwenda na mahitaji ya wakati. anapotakiwa kuongea kwa utulivu anafanya hivyo. katika mikutano ya hadhara anaweza kuongea kwa sauti kali inayohamasisha na kusisimua. anaweza kujenga hoja polepole na kuacha nguvu ya hoja isimame. anaposhambuliwa kwa matusi bungeni, mfano kuna wakati nilimsikia mbunge mmoja wa CUF anamuita mcheza disko, anakuwa mtulivu na ku-ignore, with maximum impact. anajua wapi akae kimya, wapi atoe tamko. kila la heri kamanda!!
 
Siyo kama wale walafi wanaotangaza kugombea urais kila siku
 
Mnamshabikia mpiga Disco kweli nyinyi ni wachovu khaa

Kwani sio mtu? Mbona yule wa Madagascar anaongoza nchi vizuri kuliko wengi wengine? Kila kitu na wakati wake!!

Andry Nirina Rajoelina (Malagasy: [ˈjandzʲ nʲˈrinə radzoˈel]), born May 30, 1974, is the President of the High Transitional Authority of Madagascar. He became president on March 21, 2009, during the 2009 Malagasy political crisis, after holding the office of Mayor of Antananarivo for one year prior. Before entering the political arena, Rajoelina launched several successful enterprises, most notably including a printing and advertising company called Injet in 1999 and the Viva radio and television networks in 2007. Over the course of his teens and early twenties, he gained popular recognition in Antananarivo as a DJ at local clubs and parties, and later for organizing and promoting musical events in the capital.
 
Kwa kuongezea tu uliyoyasema,
Ni kamanda mbunifu wa matumizi ya ndege, ccm wakamzomea, mwisho nao wakalazima kuiga ubunifu wake.
Ni kamanda aliyeanzisha M4C arusha na sasa zinatikisa nchi nzima.
Ni kamanda wa aliyeanzisha sare za chama.
Kwa ujumla ubunifu wake ndio imekuwa nguzo muhimu kwa ukuaji wa chadema. Bravo.

Mhe Aweda,

Hakika umenena. CHADEMA kinaendelea kudhihirisha kuwa kina watu makini ambao kweli wako tayari kuchukua uongozi wa Taifa hili ambalo kwa kweli sasa limepoteza kabisa heshima na maadili ya kiuongozi.

Mhe.Freeman Mbowe amejizolea umaarufu kwa kujenga hoja zenye mashiko nje na ndani ya Bunge letu. Mhe. Mbowe amekuwa akitoa hoja ambazo ni makini na msumari kwa serikali ya Magamba. Sote ni mashahidi jinsi alivyokuwa anampiga maswali PM Pinda akawa anaishia kuyajibu kihunihuni na kiubabaishaji zaidi. Kama kawaida ya magamba Maswali magumu kwa majibu rahisi yaliyojaa kebehi na dharau kwa upinzani!

Watanzania wa sasa wamekuwa werevu,wasomi na wachambuzi wa maswala kwa hiyo wanajua kila kitu kinachoendelea nje na ndani ya Bunge. Nani anayezungumza pumba na utumbo Bungeni na nani anazungumza hoja zenye mashiko na kuleta tija kwa Watanzania bila ya kubagua kama wanavyofanya chama Twawala-CCM.

Kuna haja ya Watanzania wote kwa ujumla wao kuungana pamoja kwa umoja ili kuipa CHADEMA ridhaa ya kuwaongoza kwa kipindi kinachoanzia 2015-2020. Kuna haja ya Watanzania kufanya mageuzi na mabadiliko ya lazima kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia katika mataifa ya wenzetu ambako kuna Demokrasia ya kweli. Hatuwezi kuongozwa na chama kimoja milele kama wanavyojidai CCM kana kwamba hii nchi ni yenye sera ya chama kimoja. Hili lisipewe nafasi katika Uchaguzi mkuu ujao wa 2015.

Kila lakheri CHADEMA. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA.
 
Kwa kweli juhudi za kamanda MBOWE zinaonekana wazi huyu ni kiongozi SHUPAVU na si mchumia tumbo kikubwa zaidi hapendi umaarufu wa wazi wazi kama wanavyofanya wengine.
 
Kwani sio mtu? Mbona yule wa Madagascar anaongoza nchi vizuri kuliko wengi wengine? Kila kitu na wakati wake!!

Andry Nirina Rajoelina (Malagasy: [ˈjandzʲ nʲˈrinə radzoˈel]), born May 30, 1974, is the President of the High Transitional Authority of Madagascar. He became president on March 21, 2009, during the 2009 Malagasy political crisis, after holding the office of Mayor of Antananarivo for one year prior. Before entering the political arena, Rajoelina launched several successful enterprises, most notably including a printing and advertising company called Injet in 1999 and the Viva radio and television networks in 2007. Over the course of his teens and early twenties, he gained popular recognition in Antananarivo as a DJ at local clubs and parties, and later for organizing and promoting musical events in the capital.

Yes. You have rightly put it. Wenzetu wanadhani elimu za wengine ni bora kuliko za wengine. Kubwa ni swala la specialization tu. Mtu anaweza kusomea muzic, mwingine akasomea Uchumi, Utawala, nk. la muhimu ni uelewa wa mambo kwa mapana yake na jinsi gani mtu anaweza kuona matatizo ya wengine na kufikiri namna ya kuyatatua. tukilijua hilo hatutadharauliana kwa aina ya elimu au specialization ambayo mtu ameamua au aliamua kuchukua. I think the man in question is smart and he knows what to say and where to say it. Wapo watu na PHd zao lakini ukiwasikiliza kila siku wanatema pumba tu. Tuangalie shule lakini pia tuheshimu vipaji na ubunifu wa watu wengine
 
Kwa kuongezea tu uliyoyasema,
Ni kamanda mbunifu wa matumizi ya ndege, ccm wakamzomea, mwisho nao wakalazima kuiga ubunifu wake.
Ni kamanda aliyeanzisha M4C arusha na sasa zinatikisa nchi nzima.
Ni kamanda wa aliyeanzisha sare za chama.
Kwa ujumla ubunifu wake ndio imekuwa nguzo muhimu kwa ukuaji wa chadema. Bravo.

Hii ndio tufauti ya wasiasa walio shiba na wenye njaa,si kama wengine wanaojikomba TISS na kwa magamba
 
Mnamshabikia mpiga Disco kweli nyinyi ni wachovu khaa

It doesn't matter. Rajoelina of Mardacasca pamoja na upiga mziki wake leo Madagasca imetulia tangia 2009 alipomuondoa Ravanomanana. Pamoja na kupitia kipindi kigumu, CDM imeimarika na kuongeza zaidi kuliko huko nyuma chini ya uongozi wake. Bado, ni katika uongozi wake alipitia nyakati ngumu sana. Wengi walidhani baada ya kifo cha Wangwe CDM kingekufa, bado ndipo kiliendelea kuimarika zaidi na zaidi. Baada ya kupandikiza ushabiki wa kidini, CDM kiliendelea kuimarika. Viva Mbowe, Slaa na Zitto
 
Mhe Aweda,

Hakika umenena. CHADEMA kinaendelea kudhihirisha kuwa kina watu makini ambao kweli wako tayari kuchukua uongozi wa Taifa hili ambalo kwa kweli sasa limepoteza kabisa heshima na maadili ya kiuongozi.

Mhe.Freeman Mbowe amejizolea umaarufu kwa kujenga hoja zenye mashiko nje na ndani ya Bunge letu. Mhe. Mbowe amekuwa akitoa hoja ambazo ni makini na msumari kwa serikali ya Magamba. Sote ni mashahidi jinsi alivyokuwa anampiga maswali PM Pinda akawa anaishia kuyajibu kihunihuni na kiubabaishaji zaidi. Kama kawaida ya magamba Maswali magumu kwa majibu rahisi yaliyojaa kebehi na dharau kwa upinzani!

Watanzania wa sasa wamekuwa werevu,wasomi na wachambuzi wa maswala kwa hiyo wanajua kila kitu kinachoendelea nje na ndani ya Bunge. Nani anayezungumza pumba na utumbo Bungeni na nani anazungumza hoja zenye mashiko na kuleta tija kwa Watanzania bila ya kubagua kama wanavyofanya chama Twawala-CCM.

Kuna haja ya Watanzania wote kwa ujumla wao kuungana pamoja kwa umoja ili kuipa CHADEMA ridhaa ya kuwaongoza kwa kipindi kinachoanzia 2015-2020. Kuna haja ya Watanzania kufanya mageuzi na mabadiliko ya lazima kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia katika mataifa ya wenzetu ambako kuna Demokrasia ya kweli. Hatuwezi kuongozwa na chama kimoja milele kama wanavyojidai CCM kana kwamba hii nchi ni yenye sera ya chama kimoja. Hili lisipewe nafasi katika Uchaguzi mkuu ujao wa 2015.

Kila lakheri CHADEMA. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA.

Ili tupige hatua tunahitaji mtu mwenye msimamo wa pekee, kujiamini, asiyebabaika na anayesimamia kile anachokiamini. Nchi inaliwa na wajanja wachache, hao ndio waliojipenyeza kila kona ya nchi yenye kuleta senti ktk mfuko wa taifa, wapo TRA, kwenye mikataba ya madini, gas, uzalishaji wa umeme, maliasili, nk.

Watanzania tunahitaji mtu mwenye roho ngumu ambaye atakuwa tayari hata kumpeleka jela mkewe, mtoto, baba, mama au kimada wake kwa kuiba mali au pesa za umma. Nimemfuatilia sana Mhe Mbowe, nikakumbuka alipojaribu bahati yake kutaka kuwa raisi mwaka 2005, alishindwa vibaya, akaona bado hajafika, akarudi na kujipanga kwa kujenga chama, akaona lazima kiwe na mtandao kila mahali kuanzia kijijini mpaka mjini, kuanzia kwa wababa mpaka watoto, vijana mpaka wamama, akajipanga kuwa na nguvu kubwa zaidi ya wabunge, akajipanga kuondoa majungu na fitina ya muonekano wa chama kuwa wa kikristo au kichaga. Huyo ndio Mbowe, anafanana sana na Kagame, mwanajeshi ambaye hana hata degree lakini anaijenga rwanda iwe kwenye kundi la 'Developed conuntries'!!!
 
Back
Top Bottom