Mgonjwa aidai TMJ, Hindu Mandal fidia ya shilingi milioni 500

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,127
10,414
Dar es Salaam. Mfanyakazi wa Wizara ya Kilimo, Frorence Samwel anadai fidia ya Sh500 milioni Hospitali za TMJ na Hindu Mandal za jijini Dar es Salaam na daktari Moirice Mavura kwa kile anachodai kuwa ni uzembe katika kumtibu.

Pia amedai alipwe Sh53 milioni kwa ajili ya gharama mbalimbali, ikiwemo ya matibabu na usafiri.

Frorence amefungua kesi hiyo dhidi ya Dk Mavura pamoja na hospitali hizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidai kuwa hospitali hizo zilifanya uzembe alipokwenda kupata huduma ya matibabu.

Akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhan Rugemalira huku akiongozwa na wakili wake Norbert Mlwale alidai kuwa Juni 27, 2018 alienda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na alifanyiwa uchunguzi wa koo ndipo alielezwa amuone Dk Moirice Mavura.

Alidai baada ya kumuona Dk Mavura alimwelekeza kuwa aende katika hospitali ya Hindu Mandal kwa kuwa ina vifaa vya kisasa kwa ajili ya upasuaji na anafanya kazi katika hospitali hiyo.

Shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa Julai 9, 2018 Dk Mavura alimfanyia upasuaji katika koo lake na alitoa sampuli za tezi la kushoto zikapelekwa katika hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi.

Alidai baada ya kufanyiwa uchunguzi wa sampuli hiyo hospitali ya TMJ ilitoa ripoti yake ikidai kuwa alikuwa na ugonjwa wa Rapillary Carcinoma of Thyoid ambayo alikabidhiwa Dk Mavura.

Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo Dk Mavura alimfanyia upasuaji wa pili na kuiondoa tezi iliyoambukizwa ugonjwa huo.

Anaeleza kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo zilichukuliwa sampuli za tezi zenye ugonjwa huo na zilipelekwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi mwingine ambapo ripoti ilionyesha kuwa tezi hizo zipo sawa hazina ugonjwa wowote. Mdai huyo alipopewa majibu hayo alienda nayo hadi katika hospitali ya Hindu Mandal na alipofika aliambiwa akamuone daktari aliyetajwa kwa jina moja la Mavunda ambaye alimweleza amekutwa na kansa ya Thyroid hivyo anatakiwa aende katika hospitali ya Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa ajili ya kuanza matibabu ya mionzi.

Anaeleza kuwa alipofika katika hospitali Ocean Road aliomba apimwe tena ili kujua kama ana tatizo hilo, ndipo walimwambia hawapimi upya kwa kuwa huwa wanategemea taarifa za mgonjwa kutoka hospitali husika.

“Nilipewa barua kutoka hospitali ya Hindu Mandal ili niende nayo hadi katika hospitali ya Ocean Road ili nianze matibabu ya mionzi,nilipofuatilia sikufanikiwa nikawa ninazunguushwa huku afya yangu ikiendelea kudhoofika huku ngozi yangu ikisinyaa kama mzee huku nywele zangu zikinyonyoka,” alidai Frorence.

Alidai baada ya kuikosa huduma ya mionzi alichukua uamuzi wa kukopa fedha benki na kuuza kiwanja chake huku ndugu zake wakimchangia fedha ili aweze kwenda hospitali ya Apollo iliyopo nchini India kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baada ya kupata fedha hizo akaenda katika hospitali ya Hindu Mandal ili apewe barua pamoja na sampuli za tezi hizo aweze kwenda nazo katika hospitali ya Apollo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Nilipewa sampuli ambazo zilifungwa kama nilivyokabidhiwa, nilizipeleka moja kwa moja hadi katika hospitali ya Apollo iliyopo nchini India, zilifanyiwa uchunguzi na ilionekana sikuwa na kansa ya Thyoid,” alidai Frolence.

Anasema madaktari wa hospitali ya Apollo walibaini tezi yote ya Thyoid ya kushoto inayosaidia kutengeneza homoni imeondolewa wakati alipofanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Hindu Mandal, jambo ambalo limemsababishia ngozi yake kusinyaa na nywele kunyonyoka.

“Mimi nilikuwa najua nimefanyiwa upasuaji wa goita na sikuwahi kuambiwa na hospitali ya Hindu Mandal kama wamenitoa tezi, nimekuja kujua baada ya kuelezwa na hospitali ya Apollo ya nchini India kuwa kinachonisumbua ni upungufu wa homoni na siyo kansa.

Anadai hospitali ya Apollo ilimuandikia dawa za kuongeza homoni ambapo alielezwa katika maisha yake yote atakuwa anatumia dawa hizo, hatakiwi kuacha na asipofuata masharti hayo ngozi yake itasinyaa na nywele zitanyonyoka.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Rugemarila aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 13,,2022 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mdai.

Source: Mwananchi, July 24

=========

NB:NDO MAANA VIONGOZI NA MATAJIRI HAWATAKI KUTIBIWA NCHINI PIA HIYO FIDIA NAONA NI NDOGO SANA MAANA TEZI YA THYROID INA UMUHIMU MKUBWA MNO KWA MWILI WA BINADAMU NI KAMA WAMEPUNGUZA SIKU ZAKE ZA KUISHI.
 
makaveli10

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
22,065
60,201
Ndio kilichobaki, tukianza kushitakiana kidoogo umakini utakuwepo, hatukatai kukosea ndio uwanadamu lakini ni too much.

Wale kenge wa dar group sijui, walifanya uzembe kiasi dada yangu akatolewa kizazi kabisa, ndugu zangu nawaambIa tuwashughulikie, wanasema mradi katoka salama, tuache tu., mtu kakosa mtoto na kizazi wametoa😠
 
feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,127
10,414
Ndio kilichobaki, tukianza kushitakiana kidoogo umakini utakuwepo, hatukatai kukosea ndio uwanadamu lakini ni too much.

Wale kenge wa dar group sijui, walifanya uzembe kiasi dada yangu akatolewa kizazi kabisa, ndugu zangu nawaambIa tuwashughulikie, wanasema mradi katoka salama, tuache tu., mtu kakosa mtoto na kizazi wametoa
Da group imeoza kaka haifai.
 
Luv

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
2,402
4,797
Ndio kilichobaki, tukianza kushitakiana kidoogo umakini utakuwepo, hatukatai kukosea ndio uwanadamu lakini ni too much.

Wale kenge wa dar group sijui, walifanya uzembe kiasi dada yangu akatolewa kizazi kabisa, ndugu zangu nawaambIa tuwashughulikie, wanasema mradi katoka salama, tuache tu., mtu kakosa mtoto na kizazi wametoa
Duh.....

Hawa mngewashtaki kabisa au muwanyofoe vizazi vyao bila ganzi
 
Loftins

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
9,678
11,932
Ndio kilichobaki, tukianza kushitakiana kidoogo umakini utakuwepo, hatukatai kukosea ndio uwanadamu lakini ni too much.

Wale kenge wa dar group sijui, walifanya uzembe kiasi dada yangu akatolewa kizazi kabisa, ndugu zangu nawaambIa tuwashughulikie, wanasema mradi katoka salama, tuache tu., mtu kakosa mtoto na kizazi wametoa😠
Sio vizuri sana kuwashitaki madaktari
 
feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,127
10,414
Ndio kilichobaki, tukianza kushitakiana kidoogo umakini utakuwepo, hatukatai kukosea ndio uwanadamu lakini ni too much.

Wale kenge wa dar group sijui, walifanya uzembe kiasi dada yangu akatolewa kizazi kabisa, ndugu zangu nawaambIa tuwashughulikie, wanasema mradi katoka salama, tuache tu., mtu kakosa mtoto na kizazi wametoa

Kesi inayotaka kufanana na hiyo iliwahi kumtokea dada mmo hapo hapo Dae group alienda kusafishwa baada ya mimba kuharibika kufika nyumbani kesho yake tumbo limejaa kumbe walitoboa kizazi.
 
chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
5,207
11,470
Madaktari wetu ni madaktari wa mchongo wanasoma historia ya magonjwa na sio utaalamu wa kueleweka yaani ommy dimpoz aliambiwa ana kansa sijui kwenda kenya na afrika kusini na ujermani ndio wakagundua tatizo na likatibiwa, wale wengine kosa wapasuliwe miguu wao wakawapasua vichwa na wa kichwa akapasuliwa miguu, yaani full janja janja vipimo havieleweki,
 
Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
9,992
18,470
Ndio kilichobaki, tukianza kushitakiana kidoogo umakini utakuwepo, hatukatai kukosea ndio uwanadamu lakini ni too much.

Wale kenge wa dar group sijui, walifanya uzembe kiasi dada yangu akatolewa kizazi kabisa, ndugu zangu nawaambIa tuwashughulikie, wanasema mradi katoka salama, tuache tu., mtu kakosa mtoto na kizazi wametoa😠
Mkuu mmatumbi hata mkishitakiana hatushtuki na hatubadiliki. Maisha yetu mengi yako mikononi mwa Mungu. Ni Mungu peke yake anatulinda na nakuturehemu. Tunafanya mambo kwa uzembeuzembe na kubahatisha bahatisha tu hatuangalii fyuchaa. Hatujali. Ni vigumu sana sisi kubadilika kwasababu tabia zetu zinazididi tu kuwa mbaya afadhali ya jana.
 
chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
5,207
11,470
Ukweli ni kwamba kwa janja janja zilizopo madaktari wetu uwezo wao ni mdogo natilia shaka elimu zao, ndio maana mwenye uwezo huwezi kuhangaika nao unaruka south au Apollo india kwao wabongo unapita tu kupata barua ya rufaa
 
101 Reactions
Reply
Top Bottom