Umewahi kuombwa rushwa ili mgonjwa wako aongezewe Damu hospitali?

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Mpango wa Taifa wa Damu Salama ulianzishwa mwaka 2004 ambapo Wananchi wenye vigezo huchangia damu kwa hiyari ili kuhakikisha taifa linakuwa na damu ya akiba kwa matumizi ya dharura.

Baada ya watu kuchangia, damu hasambazwa katika Hospitali na vituo mbalimbali ambapo hutolewa bure kwa wahitaji hasa wale wa matibabu ya Saratani, Majeruhi wa Ajali au wanaofanyiwa Upasuaji.

Ni muhimu kwa Jamii kukumbuka na kutambua kuwa huduma ya damu salama katika Hospitali na Vituo vya Afya kote Nchini ni ya Bure hivyo wasiache kuripoti endapo watatakiwa kutoa chochote kitu pindi wakihitaji huduma hiyo.
 
Hizi hospital hizi ukitaka kwa bure mgonjwa wako atakufa. Sisi tuliambiwa tutafute watu wa kuchangia damu. Kisha damu nyingine ndio ikatolewa walizokuwa nazo mgonjwa akawekewa. Hapo ni baada ya watu zaidi ya watano kuchangia.
 
Hapa muhimbili damu ni Bure,na mgonjwa wako atapewa damu Kama group la damu yake inapatikana.

Ila tunawaambia ndugu waweze kuchangia kwa mahitaji ya wagonjwa wengine,ili wengine pia wasikose. Damu ni Bure na mahitaji ya damu ni makubwa kwa hiyo tunaomba watu wawe na kawaida ya kuchangia damu maana mtu yoyote anaweza kukumbwa na tatizo hili la uhitaji wa damu.

Tepende nchi yetu tuchangia kwa mahitaji ya wengine pia.
 
Back
Top Bottom