Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

Kweli safari hii walimu wameamua maana kama maeneo ya sumbawanga nimejaribu kuwauliza baadh ya wanafunzi wa shule mbalili za msingi kama vile ndua na kizwite wanasema walimu walifika asubuh wakaondoka na akabaki mwalimu mkuu peke yake, pia nimezungumza na mwalimu wa mmoja wa shule ya sekondari kanda ananiambia kuwa hali ni tete.
 
niko huku korogwe kwasemangube hali ni tete walimu wako nyumbani tu wakiendelea na shughuli zao za mavuno ya mahindi..awali kuna wachache walifika shuleni ila mwenyekiti wa cwt wilayani korogwe aliwatimua walimu hao ...ivo kabaki mwl mkuu tu akiangalia mali za shule..lakini vitisho haviishi kuna mtu alipita ikisemekana ni usalama wa taifa na askari mmoja kumhoji mwl mkuu na kuchukua idadi ya walimu waliopo.
 
Shule ya msingi Ujiji Kigoma, wanafunzi wanarandaranda lakini mkuu wa shule anasema hakuna mgomo japo kuna walimu wawili tu!
 
Kumbe na walimu nao wana ushawishi mkubwa namna hii. Serikali isidharau huu mgomo.
 
kuna sister angu anatoka singida kuelekea moshi anasema huko kote anakopita wakibahatika kusimama anaulizia anaambiwa kimenuka mgomo kama kawa
 
huku kilombero shule ya kidodi sekondar mkuu amewalazimisha walimu kusaini mgomo au kukataa mgomo walimu wamesaini kuunga mgomo na kutokuja kazini.
 
Zanzibar haihusiki kwakuwa elimu si suala la muungano na chama cha walimu zanzibar ni tofauti na cha Bara. Cha zanzibar ni ZATU wakati cha Bara ni TTU AU cwt
 
Shule za Msingi Kigera, Buhongwa, Nyasho na sekondari kadhaa kimenuka hapa Musoma!
 
Arusha nako walimu waliwahi mashuleni wakasaini then wakasikilizia after saa nne leo wamegoma rasmi. hii nchi haitawaliki bila mashinikizo.
 
Hanang' shule ya sekondari Mahu wanafunzi wamefunga barabara ya kwenda Singida kwa kutumia madawati, hivi sasa polisi na ofisi ya elimu wamekwenda kule kutuliza hali.

Walimu wameitikia mgomo kwa zaidi ya 90% kwani shuleni wapo wapo wakuu wa shule na walimu wa field na wale wa kujitolea, shule za msingi wapo walimu wakuu tu.

Hivyo ndivyo hali ilivyo kwa Hanang' leo nilipofika hapa Katesh makao makuu ya wilaya.
 
Walimu endeleeni kugoma mpaka kieleweke na napenda kusikitika juu ya wanafunzi wa ilemela juu ya kuwafungulia kesi walezi wao badala ya serikali yao dharimu.
 
Back
Top Bottom