mansakankanmusa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 4,163
- 787
Katika ile thread yangu ya 'Kwanini moyo wa rais uwe mgumu kama wa pharao" nilimaanisha kuwa KIONGOZI wetu huwa ama hajali mambo ya msingi au anafanya makusudi..Kwanini huwa hapendi kuusikiliza umma na mahitaji yake?..anabaki kusema umma wa watanzania....au amestaafishwa kwa manufaa ya umma,...umma upi? sasa ni huo umma ndio unamuaibisha....Na kingine ni kwanini huwa HANA UWEZO AU ANAO ILA HAPENDI KUUTUMIA, UWEZO WA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU, kama hili la waalimu. Kwani waalimu wameanza kulalamika leo? Kwanini asubiri hadi mambo YAFIKIE HAPO YALIPO ndio atafute nini cha kuongea?.....jamani mimi nina maswali yasiyoisha, mwenye namba zake anitumie kwani nilizo nazo labda hazitumii tena au kabadili namba.......nitampigia sasa hivi nimuulize au nisaidie kumshauri kidogo,,,huenda akanisikiliza au Mungu akamgusa kutenda tofauti na kawaida.
Walimu wote nchini:
Jipeni moyo kwani saa ya ukombozi wenu imekaribia
Wanafunzi wote nchini:
Hao waalimu ni mama zenu na baba zenu, wanagoma ili wawezeshwe na serikali ili wawafundishe vizuri, msiwalaumu.
Jingine ni kile kichefuchefu cha mafao yetu kwenye hii mifuko fisadi ya pensheni...kwani rais alishindwa kuusikiliza umma unataka nini?...
Kwa hili, nimechefukwa na roho sana, ila nikafarijiwa na mbunhge wa kisarawe, Mhe Jafo. nilijaribu kumpigia simu yake ikawa haipatikani, nadhani alikuwa kwenye "session" kule bungeni. Lengo lilikuwa ni kujua amefikia wapi kuhusu kuorodhesha malalamiko ya umma kwa mwenyekiti wa bunge, Mhe. Jenista Mhagama...
Au jamani rais kwa kuwa anamaliza muda wa utawala wake hivyo anaona hana haja ya kuusikiliza umma.
umenisuuza sana, ukimpata jefo, nimp nmpe yangu