Tukio hili kwanza limechochewa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Balozi Mwapachu, wiki iliyopita kwenye baraza la chuo alimtukana Mwenyekiti wa jumuiya ya wahadhiri kwa kumuita Mugabe kwa sababu hataki kuitisha uchaguzi. Na akaamuru kikao kijacho asiingie kama uchaguzi hamna. [Tunaamini wana mpango wa kupandikiza mtu wao]
.....
2. Kwenye baraza la chuo, walitangaziwa Prof. Shaban Mlacha ameongezewa miaka minne na Raisi Jakaya Kikwete. Wahadhiri wanahoji mgomo wa mwaka jana,wa walimu na wanafunzi,waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi atarudi kuja kutoa ufafanuzi hatua zilizofikiwa na serikali, hajarudi, wala ripoti ya tume alizounda haijatolewa, manunguniko ya wafanyakazi, na wanafunzi hayajafanyiwa kazi kabisa. Hili limesababisha wastani wa wafanyakazi watatu wakiwemo Prof. na madaktari huacha kazi kila mwezi. Kuanzia July 2011, hadi July 2012, jumla ya wafanyakazi 42 wameondoka chuo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuacha kazi (resignation). Mbaya zaidi kumekuwa na ulipizwaji kisasi wa hali ya juu. Wahadhiri wamefukuzwa sana kazi, na baadhi ya kesi zipo mahakamani. Kibaya zaidi imethibitika kikwete kawaongezea muda viongozi wote wa chuo. Prof. Kikula alistaafu 15 December 2012, ameongezewa nae mkataba, pamoja na lawama zote. Hili wamelichukulia kama Serikali haiwajibiki na imeonyesha dharau kubwa sana, lakini kibaya zaidi hili limechukuliwa kwenye taswira ya Udini, ambao umekuwa ukikitafuna chuo, kufikia hatua ya kuunda kamati ya kushughulikia suala hilo, ambayo pia inasemekana *ilivunjika bila mafanikio kabla hata ya kuanza kazi.
Ndugu mleta mada! Pole kwa kutumia muda mwingi kuandika hii habari kwenye ukurasa huu kwa faida ambayo mimi bado sijaijua bado, na kama wewe ulitumwa na hicho kikao uje hapa JF uelezee azimio hilo au la sijajua bado, kama ndivyo basi nina mashaka na uelewa wa wajumbe wa hicho kikao. Turudi kwenye point zako ulizotoa.
Kwanza kabisa umesema mwenyekiti wa baraza la chuo
ALIMTUKANA KIONGOZI WA UDOMASA KWA KUMUITA MUGABE ,Hivi unataka kuaminisha wanajukwaa kuwa Mugabe ni tusi??, Je ni tusi la kabila gani, kwa maana ktk misamiati ya matusi ya Kiswahili halipo. Kama huyo kiongozi alichaguliwa na wajumbe, na muda wake umekwisha taratibu si zinasema uchaguzi unabidi ufanyike? Ni imani yangu kuwa katiba yenu inaelekeza hivyo, sasa kama hakuna maelezo yenye mantiki ya kwa nini hajaitisha uchaguzi huoni kuwa mwenyekiti wa baraza la chuo ana kila sababu ya kuhimiza hilo lifanyike?? Kwa nini aamini kuwa yeye ndiyo kiongozi pekee mwenye uwezo wa kuongoza hiyo jumuiya? Huoni kuwa hilo ni tatizo??? Unataka kuniambia kuwa hao wahadhiri watagoma kwa kuwa kiongozi wao kaitwa Mugabe????
Suala la chuo kuletewa pesa kidogo kutoka serikalini hivyo kulazimisha kufanya cost sharing. Hembu tuwe wazalendo jamani, hivi vitu tujaribu kuviown!. Sasa kama Chuo kinapokea hela kidogo kutoka serikalini, mnatarajia pesa ya kugharamia hizo huduma zitatoka wapi??. Wewe kama mwalimu umetumia elimu yako kwa kiasi gani kukiingizia chuo kipato. Mimi nafahamu kuwa mwalimu unatakiwa uandike miradi na ufanye consultancy cervices, ambazo malipo yake partly yanaingia chuoni na kiasi kidogo unapata wewe, sasa kweli university lecturer unakaa unataka kugoma kwa sababu ya kuondolewa sh 500?? Kwa sababu zinazojulikana. Hata kama hamjapenda hilo suala haliwezi kuwa linacall for mgomo, ni suala linalovumilika wakati majadiliano na njia nyingine za kulitatua zinaendelea.
Kama Mlacha na hao wenzake wameongezewa mkataba tatizo ni nini? Kwani tatizo ni dini yake au ni utendaji wake wewe hujaupenda? Je unafikiri akiletwa mkristo tatizo unaloliona kwa mlacha hutoliona tena, au akisha kuwa mkristo tayar wewe uko happy??. Na unatuambia kuwa kuendelea kwa uwepo wa mlacha na wenzake kumefanya maprof na ma Dr kuacha kazi, mimi ninawasiwasi na elimu za hao walioacha kazi kwa hizo sababu!! Au walitarajia wangeteuliwa wao? Huo utakuwa ni ubinafsi uliokithiri!
Hivi unataka kutuaminisha kuwa, waajiriwa wengi hapo udom ni waislam, na hao hao waislam kwa wingi wao ndo wameadhimia kwenye hicho kikao chenu kumuondoa mlacha kwa sababu kuna uislamu sana hapo mahali????. Unajua mimi nawashauri kama mnataka mfanikiwe kwenye mambo yenu ya msingi hili suala la Udini msilizungumze kabisa, kwa maana linawagawa ninyi kwa ninyi kuwa ktk makundi mawili yenye interest tofauti, tumieni elimu zenu vizur kupambanua mambo.
Suala la kupunjwa mishahara na kuchelewa kupanda vyeo ni jambo ambalo halihitaji mgomo, mnaweza kutumia majadiliano na uongozi wa chuo mkishirikiana na watu wa hazina ili muone kuwa tatizo ni Mlacha ndiye hataki mpandishwe vyeo au ni nini? Hi indo namna ya kutatua mambo. Unapokuwa na Mtazamo hasi dhidi ya mtu matokeo yake ndo haya.