Mgomo wa wahadhiri UDOM wanukia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa wahadhiri UDOM wanukia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Oct 31, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Jana wahadhiri Chuo Kikuu cha Dodoma walifanya mkutano mkuu wa mwaka (General Assembly), pamoja na mambo kadhaa wameazima kuanza mgomo kuanzia kesho alhamisi saa 2 asubuhi.

  Tukio hili kwanza limechochewa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Balozi Mwapachu, wiki iliyopita kwenye baraza la chuo alimtukana Mwenyekiti wa jumuiya ya wahadhiri kwa kumuita Mugabe kwa sababu hataki kuitisha uchaguzi. Na akaamuru kikao kijacho asiingie kama uchaguzi hamna. [Tunaamini wana mpango wa kupandikiza mtu wao]

  Kati ya mambo yaliyosababisha wahadhiri hao kubaki Chimwaga kwa ajili ya mgomo ni kama ifuatavyo:

  1. Chuo kinadai serikali inawaletea hela kidogo sana, ambazo hazitoshelezi, hivyo wanataka kufanya cost cutting: Kuwanyanganya nyumba wahadhiri wote walio chini ya level ya udaktari,: kuanza kutozwa nauli kwenye mabasi, maarufu kama kitumbo au Zonda, kwa siku 2000, wakati nauli ya daladala kwenda na kurudi ni 600 tu.

  Wafanyakazi wote kama huna bima ya afya unajigharamia matibabu. Mwalimu atakayeenda kusoma kukatwa mshahara wake. Pia imepiga marufuku walimu kwenda kusoma nje ya UDOM.

  Hali ya kuwa chuo chenyewe hakina wahadhiri kabisa. (TA anafundisha shahada ya kwanza, wahadhiri ambao hata sio madaktari wanafundisha shahada ya uzamili, mtu amemaliza Masters anakwenda kufundisha masters).

  Kibaya zaidi wahadhiri walikuwa wakilipwa kwa ajili ya kusimamia mitihani (Invigilation) 15,000 kwa kipindi, na kusahihisha (Marking allowance) 500 kwa script moja. Na hii hela inatokana na ada ya mtihani ambayo hulipwa na kila mwanafunzi tsh 20,000, malipo hayo nayo yamesimamishwa, wakati huo huo wanafunzi badala ya kulipa 20,000 wanatakiwa walipe 40,000 kwenye hiyo proposal mpya.

  2. Kwenye baraza la chuo, walitangaziwa Prof. Shaban Mlacha ameongezewa miaka minne na Raisi Jakaya Kikwete. Wahadhiri wanahoji mgomo wa mwaka jana,wa walimu na wanafunzi,waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi atarudi kuja kutoa ufafanuzi hatua zilizofikiwa na serikali, hajarudi, wala ripoti ya tume alizounda haijatolewa, manunguniko ya wafanyakazi, na wanafunzi hayajafanyiwa kazi kabisa.

  Hili limesababisha wastani wa wafanyakazi watatu wakiwemo Prof. na madaktari huacha kazi kila mwezi. Kuanzia July 2011, hadi July 2012, jumla ya wafanyakazi 42 wameondoka chuo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuacha kazi (resignation). Mbaya zaidi kumekuwa na ulipizwaji kisasi wa hali ya juu. Wahadhiri wamefukuzwa sana kazi, na baadhi ya kesi zipo mahakamani.

  Kibaya zaidi imethibitika kikwete kawaongezea muda viongozi wote wa chuo. Prof. Kikula alistaafu 15 December 2012, ameongezewa nae mkataba, pamoja na lawama zote. Hili wamelichukulia kama Serikali haiwajibiki na imeonyesha dharau kubwa sana, lakini kibaya zaidi hili limechukuliwa kwenye taswira ya Udini, ambao umekuwa ukikitafuna chuo, kufikia hatua ya kuunda kamati ya kushughulikia suala hilo, ambayo pia inasemekana *ilivunjika bila mafanikio kabla hata ya kuanza kazi.

  3. Kumekuwa na maswala ya udini sana, na hili lawama zinaelekezwa kwa Mh. Rais namna ya uteuzi wake lakini na baadae ajira. Na hivyo waislamu kujiwekea territory. Mwenyekiti wa baraza, VC, DVC PFA, Bursar, Afisa Mwajiri Mkuu na baadae kundi kubwa sana la wazanzibari waliletwa kwa kupitia Mkurugenzi wa Stadi za elimu ya juu Dr. Ahmed Ame.

  Huu ubaguzi umetutafuna hadi kwa wanafunzi, utauona dhahiri wakati wa uchaguzi, na mwaka jana ghasia hizo za kidini zilipelekea vurugu na wanafunzi kujeruhiwa na mpaka sasa kesi zipo mahakamani zinaendelea.

  4. Uongozi wa chuo ulipandikiza watu waliojidai usalama wa taifa, na kuanza kupita kwa viongozi kwa ajili ya kuwatisha kuwaua akiwemo aliyekuwa kiongozi mahiri na machachari, Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi, na Makamu wa Jumuiya ya wahadhiri – UDOM.

  Kesi hiyo ipo Polisi na ilisharipotiwa Usalama wa Taifa Mkoa, pamoja na ushahidi wote kuwepo, inasemekana Dr. Shukuru Kawambwa alimuombea msamaha afisa huyo feki (Khalifa Kondo), ambaye mmoja wa ndugu yake inasemekana alitajwa kuhusika kwenye shambulio la Ulimboka (Angalia Mwanahalisi la mwisho). Tuhuma hizi pamoja na kufikishiwa viongozi mbalimbali wa Serikali hayajafanyiwa kazi.

  5. Tatizo la mishahara kupunjwa na watu kutopanda madaraja kwa wakati limeendelea kuwa tatizo sugu. Ajira bado taratibu haziko wazi, inasemekana ili uajiriwe Finance Department lazima uwe muislamu. Sijui?? Fika UDOM upate takwimu (Bursar- Mohamed Mwandege, Msaidizi wake Rukia, wengine Chang'a, Mwinyi, Athuman Chamosi na wengine watano wote waislamu), masuala haya ndiyo yanaleta mgogoro kwa kuwa hayana ufafanuzi.

  6. Kikubwa uongozi wa chuo umekuwa ukikataa kukutana na wahadhiri, walikutana mara moja baada ya Waziri mkuu kuwaamrisha baada ya hapo, walijibu barua kali sana wakionya wasiitwe tena, barua hiyo ilitoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa chuo – Taaluma, utafiti na ushauri), sasa hapa wameazimia hawatatoka chimwaga, ukumbi maarufu kwa ajili ya mapambano hadi viongozi hao waje, na Waziri Mkuu aje awaambie mbona hajawasaidia kutatua matatizo yao?

  (Ufafanuzi zaidi: Paul Loisulie, Mwenyekiti Jumuiya ya walimu au Lameck mjumbe kamati ya utendaji, jumuiya ya walimu au Richard Alphone huyu anaweza kukupatia hata baadhi ya documents)

  (Kwa upande wa uongozi wa chuo, taarifa hizi wanaweza kutolea ufafanuzi Makamu mkuu wa Chuo Prof. Idris Kikula, Mwenyekiti wa baraza la Chuo Balozi Juma Volter Mwapachu. Kuhusu usalama wa raia feki suala hili liko kwa Regional security Officer RSO)
   
 2. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Waislam nchi hii ya Udom washakuwa kero kero! Kumbe hadi ninyi waalim mwapata shida? Nkajua sie wanafunzi tu bwana. Hilo la maprof kuondoka limetuathiri weng cuz wametuondolea prof Nwoye wetu! Sasa jamani kitumbo buku 2 per day afu migari yenyewe ile ka mapango ya panya inawezekana kweli? They are so unfair to u jamani! Wanakusanya hela za kampeni za ccm 2015 kwa migongo yenu?

  Mkiyakubali hayo basi mjue mmekwisha! Yeye mlacha, kikula na wengneo hayo magari SU wanalipia how much? Wao kwanza ndo wangetakiwa walipe house alowance cuz wana hela ndefu! Yaani ktk hayo mtakayosimamia kugoma, basi gomeni mpaka kieleweke, ikibidi wafunge mchuo wao bhana.

  Nimegundua nyie mnanyanyaswa hvo afu hasira mnatumalizia sisi kwa kutukong'oli SUP na makarai sio? NAWAOMBEA USHINDI, HAO PIMBI WAZEE WAONDOKE CUZ WASHAKUWA KERO!!
   
 3. E

  EstoJ Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi siwahamini kabisa hawa waadhiri wa udom. Nafikiri wengi ni makanjanja ndiyo maana wananyanyasika mgomo uliopita walishindwa kusimamia msimamo. Wakawa wanaimba wimbo wa kuwa na imani na liwalo na liwe na dhaifu sasa sijui kama wanaweza kuuondoa huo uozo hapo hudom.
   
 4. E

  EstoJ Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo watu wnalijadili hili swala kwa point za kidini... Hata kama viongozi wote wangekuwa waislamu lakini wenye uwezo wa kitaaluma na wa kiuongozi siyo tatizo. Tatizo ni pale watu wanapo pewa kazi za kitaalam kwa kuangalia dini zao... hapo hapafundishwi bible au quran hivyo sifa za kitaaluma ziwe zinapewa kipaumbele.
   
 5. r

  rimoy Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ok for your info.
   
 6. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ukishawaingiza hawa jamaa ujue umeharibu. Angalia jamaa zao wa Muslim University of Morogoro...Kikwete ndiyo architect wa haya mambo yote ya udini...
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Wewe tena tumeishakuzoea una Allergy na Uislam.
   
 8. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mwanzo tulianza na NSSF, watu wakapandwa jazba sana ila ndio ukweli wenyewe,
  Now ni Udom,kiukweli chuo hicho kina udini sana angalia mawarden vilaza kutoka zanzibar wamejazana pale
  bila hata qualification za maana!!Njoo kwenye depart ya finance My God utaimba haleluyah,kajaza ofisi nzima
  masheikh!!Huyu prof uchwala mlacha ajiandae kwenda mahakama ya hague few years to come lol!!
   
 9. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yana mwisho.Hakuna marefu yasiyo na ncha.
   
 10. MALI YA BABA

  MALI YA BABA JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 461
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Udom ni kuna udini sana jamani hasa kwenye suala la ajira kiukweli hadi upate basi ni bahati tu ya mungu lakini jamaa mpango wao ni kuwapa waislamu nafasi nyingi na c wakristo huo ndo ukweli kuna mbegu za udini zimepandikizwa sana udom ni mungu mwenyewe tu aturuhumie tusije tukafikia pabaya.
   
 11. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Hivi hawajaanza tu huo mgomo hadi sasa??

  Lakini nijuavyo wahadhiri huwa ni waoga sana katika kudai haki zao. Ni wazuri kupiga kelele kama akina Dr Bana lakini ikifika kwenye kudai maslahi yao waoga kama waandishi wa habari.
   
 12. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Malalamiko hapo juu hayana uhusiano wowote na dini ya watu. Huyo Prof. Kikula ametumikia kama Director IRA pale UDSM, akaenda ARU/UCLAS kama Principal mbona hajawahi kulalamikiwa kuwa ni mwislamu? hata Juma Mwabachu ana CV kubwa sana lakini kwa sababu tu amekuja UDOM basi ni mwislam. JAMANI ACHENI HIZO BIASNESS ZA UDINI, unless una evidency ya jambo lililofanyika la udini - mwandishi unapotosha umma.

  hizo nafasi za juu kuna akina Mkapa, mbona hawatajwi? DVC academic ambaye anaajiri waalimu ni mkristo mbona hatajwi? acheni KUPOTOSHA jamani. unataka kusema kuna mwalimu alishindwa kuajiriwa akiwa na sifa kwa sababu ni mkristo?
   
 13. Niambieni

  Niambieni JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 599
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Viongozi wa UDOM ninawaelewa na nawajua vizuri sana, nimewahi kufanya kazi nao UDSM. Ukweli kabisa, viongozi wa UDOM hawana udini wala ukabila. Suala la udini halipo UDOM, bali labda kuna watu wanapenda masilahi yao binafsi na ndoto zao za kutajirika kwa haraka, ambazo hazijawafikia kwa kiutaratibu ndio maana wanaimba udini ili viongozi wasafi watolewe na waje wa kuwafanya wepate mwanya wa kuiba.

  Mimi niliwahi kufanya kazi na Prof. Mlacha UDSM, ni kiongozi mzuri sana. Prof. Kikula naye ndio kabisaa hana udini kabisa. Dr. Ame ndio anapenda watu bila ubaguzi wowote. Jamani hizi kuna sheria inayosema Wazanzibar hawatakiwi au hawaruhusiwi kufanya kazi UDOM au Tanzania Bara?.

  Ni chuo gani cha Umma hapa Tanzania kinachowasafirisha wafanyakazi wake bure?. Au UDSM wafanyakazi wana safirishwa na Chuo?. Mbona mnasema daladala kwanini msizitumie nasikia zipo dala dala za UDOM nyingi tu. Kwani sera zinasemaje kuhusu kupewa Nyumba? Nchi inafuata utaratibu wa kutibiwa kwa bima, au ndio ninyi wa UDOM tu mnataka kutibiwa bure jamani?. Kama kweli Dept. ya fedha ni waisilimu watupu basi nawapongeza. Maana ndio hao hao ambao waliowafanyia mipango mizuri ya kuishi vizuri, kwani nasikia ni Chuo Kikubwa na kizuri sana. Kwa hiyo Bursar wenu na timu yake inafanya kazi vizuri hadi kufikia kuongeza idadi ya wanafunzi na walimu. Mafanikio bwana ni mipango mizuri ya hawa mabwana.

  Jichunguzeni, Bunge lilianza Jana. Au wakuu wa Chadema waliwafikia na kuwapandikiza kitu na ndipo mmeanza?.

  Eti walimu wanaacha kazi n... kwani waliopo hapo walipotoka si waliacha kazi kwingine na kuja UDOM. Huyo Nowe si aliacha Chuo sijui SUA na kuja UDOM?. Mbona hamuwasemi walioacha huko India, Urusi, Kenya, Uganda, Rwanda na wengine toka humu humu wamehamia UDOM siku chache tu zilizopita. Nasikia, walimu wanaojiunga na UDOM ni wengi sana, soma Prospectus zenu na machapisho mengine ujionee.

  Mwacheni Prof. Mlacha na timu yake ambayo hadi sasa dunia nzima inashangaa Tanzania kuwa na maendeleo ya haraka na ya viwango. Angalia wanafunzi nasikia wengine wanatoka Msumbiji, Sweden... wanakimbilia UDOM. Acheni migomo fanyeni kazi, umoja wa waalimu ni kwa masuala ya ualimu na sio migomo isiyo ya kitaaluma.
   
 14. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kuna jamaa yangu nilisoma nae alikuwa social science kama asst. lecturer kwenye mambo ya procurement , ni mtaalamu mzuri sana katika fani hiyo kwa kufaulu vizuri , amepata kazi BOT juzi ameondoka pia ni pengo kubwa sana UDOM
   
 15. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata mi nna Alergy nao maana wanaweza kukulipua na bomu mda wote aiseeee
   
 16. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mlijipendekeza kwa ccm sasa ndo wakati wenu kuvuna matunda
   
 17. m

  mwamola Senior Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujui unalolisema maana;
  i) watu wakiacha kazi huko walikokuwa mwanzo wakifika UDOM wanastahili kukatwa mshahara wao 10% kwakuwa wanajiendeleza? Hili linafanyika chuo gani Tanzania zaidi ya UDOM?
  ii) Wewe ufanyae kazi MLIMANI (UDSM) tutorial assistant akijiendeleza na kuwa assistant lecturer naanza na PUTS 2/3, UDOM ni PUTS 2/1 na anakaa na scale hiyo kwa miaka isiyofanyika na hata akilipwa hiyo scale yake kwa mshahara aliokuwa promoted nao anakaa miaka isiyofahamika hadi kulipwa SALARY ARREAS. Je UDSM mnaishi bila annual increment? Maana UDOM management wanasema HAZINA NA WIZARA YA UTUMISHI wamewazuia wasiwalipe wahadhiri wa UDOM salary arreas na annual increment. Je UDSM Pro Mkandala nae kazuiwa kuwapa annual increment na arreas waliokuwa promoted?
   
 18. m

  mwamola Senior Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  iii) Hiki ni chuo ambacho non-christian anakuambia mwakani nataraji kuajiriwa UDOM na kweli akaajiriwa. Hiyo nayo ni nini? Taasisi gani ya UMMA ambayo mtu anaweza kupredict kuwa ataajiriwa nayo kama hajui chochote na kama taasisi hiyo itatangaza ajira?
  iv) Unadai umefanya kazi na Prof na Dr amme ambae ni Director Graduate studies, kama hawa watu ni wachapakazi inakuwaje alieajiriwa kama mhadhiri msaidizi mwaka 2009 analingana mshahara na mhadhiri msaidizi alieajiriwa hata jana ama kesho alhamisi tarehe 1/11/2012? Nakuuliza tena hayo UDSM, SUA, MZUMBE , DUCE ama MUCE yanafanyika?
   
 19. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  UDOM nacho ni chuo? mimi nilizani ni Jumuia ya CCM
   
 20. Niambieni

  Niambieni JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 599
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Wasomi wenzangu, je hamjui namna ya kufuatilia matatizo yenu kwa njia sahihi? Kwani migomo ndio inayotatua?. Mbona ni suala dogo tu?. Kama mnashida fulani mfano ya kifedha inavyoonekana sehemu kubwa ya mada yenu ya mgomo, ni vema mkatuma wawakilishi kuanzia ngazi ya idara kama mnayo and then faculty na baadae ngazi ya chuo na ikishindikana sehemu husika mfano hazina kama mnavyosema na sio kwa Mh. Pinda au sijui kuilaumu CCM sijui na kulaumu mtu binafsi kama Misilamu au Mkristo fulani au Mzanzibar ???????.
   
Loading...