abbas mwaki, hivi unajua maana halisi ya neno uchochezi au wewe ni mmojawapo wa wale tunaowaita Bendera Fuata Upepo?
Kama hujui kitu fulani bora uulize kuliko kukurupuka kama nyau aliyetimuliwa akiiba mboga jikoni.
Enzi za Apartheid nchini Afrika Kusini makaburu walikiita chama cha ukombozi ANC kuwa cha kigaidi na kumkamata kiongozi wake Nelson Mandela kwa makosa lukuki, mojawapo likiwemo uchochezi.
Wadai haki wakaitwa magaidi na wachochezi. Mandela akaishi gerezani miaka 27 ambako aliandika kitabu Long Walk to Freedom.
Hatimaye Mandela, mchochezi na gaidi aliachiwa huru, huku watawala makaburu wakiwa wamejawa hofu kubwa ya Mungu.
Wananchi walitoa tamko kwamba iwapo Mandela angefia gerezani kutokana na hali yake kuwa mbaya kiafya, basi wangemwaga damu yao wazalendo na makaburu hadi bahari igeuke nyekundu.
Walisema: Tumefikia ukomo wa uvumilivu. Tumechoka. Imetosha. Mwachieni Madiba wetu la sivyo tutawanchinja ninyi wote na vizazi vyenu vyote, popote mtakapokimbilia.
Kuliko kuchinjwa kama kuku, makaburu wakaogopa na kumwachia Madiba, gaidi, mchochezi, mpigania haki na KIONGOZI SHUPAVU.
Mandela hakuwa mpenda madaraka kwa hiyo kilipokwisha kipindi chake cha kuwa rais wa kwanza mzalendo aliachia ngazi ili wengine waiongoze nchi hiyo. Alibembelezwa sana kubaki madarakani lakini alisema atabaki kuwa mshauri wa chama. Aliacha shughuli zote za siasa.
Unapotuambia tusiwasikilize wachochezi, unamaanisha nini? Hivi unafikiria kabla ya kutoa matamshi yako?
Hebu jifunze kufikiria. Jifunze historia. Nakushauri ukitafute kitabu cha Mandela ukisome. Utajifunza mengi.
Walevi wa madaraka daima huwaona wanaodai haki yao kuwa wachochezi.
Vijana amkeni. Mbona mnalala wakati kumekucha?