Mgomo wa madaktari

Dr.Chichi

JF-Expert Member
Apr 30, 2008
2,394
631
kwa wale wanaoptosha habari kuhusu mgomo wa madakitari either kwa makusudi au bila kuelewa

kila hospitali tumeacha mtu wa kwaajili ya emergency cases.sisi sio wauaji,tunaelewa anayeumia ni mtanzania wa kawaida na kwa sasa tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuokoa maisha ya wale wanaokua considered as emergency..Mungu awabariki
 
Kumbe mmegoma kweli!! Nilidhani mnapiga mkwara kama walimu..
 
wana JF
Hem nielewesheni me nipo madongo kuinama huku et kuna mgomo wa madactari lini na wap? nimeishiwa nguvu
 
ndugu tumeshaanza....yaani wangetuma hata mwakilishi akatusikiliza siku ya kwanza tusingfika huku
nina mgonjwa muhimbili lakini bado ninaamini mna haki ya kugoma kudai haki zenu, wanasiasa wana kauli za utata sana, kazi ya ualimu na kazi ya udaktari kila siku wanaimba eti ni kazi ya wito, loh! siasa ni ajira, proffessional ni kazi ya wito, kaazi kweli kweli.
 
sasa mkuu mbona vyombo vya habari vimekataa kutoa taarifa zenu??huoni kama ni dharau kubwa sana na nyie ni watu wa muhimu??
 
sasa mkuu mbona vyombo vya habari vimekataa kutoa taarifa zenu??huoni kama ni dharau kubwa sana na nyie ni watu wa muhimu??

Japokuwa ushirikiano na wanahabari ni muhimu katika kipindi hiki cha mgomo wa madaktari, lakini inabidi wanahabari waelewe kuwa madaktari hawajagoma ili watangazwe kwenye redio na TV, au wandikwe magazetini! Hivi wanapoambiwa kuwa wapishe mikutano ya ndani kisha watapewa taarifa...halafu wanasusa eti tu kwa sababu wametolewa nje, wanawanyima waTanzania haki yao ya kupata habari.

Lakini habari ni habari tu, ikiwa hot mwandishi atakuja tuu hata hasipoitwa. Hii habari ya mgomo sasa ni hot, na kesho itakuwa hot zaidi, sasa mwandishi hasiyetaka kuuza gazeti au kureport kwenye TV au redio na hasije...kwa kifupi hicho hakitasimamisha mgomo!
 
sasa mkuu mbona vyombo vya habari vimekataa kutoa taarifa zenu??huoni kama ni dharau kubwa sana na nyie ni watu wa muhimu??

Ndugu hizo ni propaganda za serikali wanatujaribu ktuvunja nguvu kutumia media...
 
Kuna mtu katoka Muhimbili kaniambia MOI ndio inaonyesha dhahiri kuwa imeathiriwa na mgomo......mapokezi hakuna wagonjwa na pia kuna mgonjwa amemkuta kaletwa na ambulance tangu saa 12 alfajiri hadi saa tano hajapokelewa.
 
hii serikali ina akili km za mbuni, Mbuni akiona adui anainamisha kichwa chake akdhani amejificha kumbe mwili wote unaonekana, loh!
 
sasa mkuu mbona vyombo vya habari vimekataa kutoa taarifa zenu??huoni kama ni dharau kubwa sana na nyie ni watu wa muhimu??


Shame upon you vyombo vya habari vya Kitanzania! Hivi mnafikiri mgomo wa Madaktari, unahitaji vyombo vya habari, kuufanya ujulikane? Ni habari inayojitangaza! Hivi vinahitajika vyombo vya habari, kuwaeleza Watanzania kwamba Jua lipo, na linaangaza mwanga?
 
Dr. Chichi huku mikoani tunawategemea huko kukoleza nguvu ya moto huu,hebu basi wahimizeni na manesi,famasia,watu wa maabara,nk wawape nguvu!
Ninafahamu fika kuwa bila daktari huduma hakuna lakini hawa kada zingine za afya ni waoga sana....weka bidii moto usambae tumechoka kulipwa sh.10,000 kama on call allowance ya masaa 24 ambayo pia kuipata mpaka iwe birthday ya mkurugenzi!
 
Najua hata mimi au mwanangu au yoyote provided ni binadamu hasa wa hali ya chini atauguwa na tiba yake ni nyinyi ma-DR mnaoendelea na mgomo,lakini kwa hili mi niko upande wenu tena nawaunga mkono kwa asilimia mia,maana siafiki mtu kumfanyisha kazi halafu usimlipe,siafiki mtu kumwambia unatakiwa kupewa nyumba au kupewa asilimia fulani ikiwa ni gharama ya nyumba tu kwa kuwa ofisi husika haina idadi ya nyumba kukidhi mahitaji,siafiki pia kumwambia mtu utalipwa kiasi kadhaa kama allowance ama ya kjuikimu au OT ama vyovyote halafu usitekeleze na ni mtu mzima na akili yake,na hapo anapofanyia kazi ndipo tegemeo lake,familia yake,ndugu zake nk halafu unamwambia ni wito.kama ingelikuwa hivyo nani yuko tayari kufanya kazi huko aliko tofauti na fani hii na asilipwe?au ukisomea fani hii maana yake ni kujitolea bila malipo?kama ni hivyo nani yuko tayari tena kusomea fani isiyokuwa na malipo?hapa tatizo ni serikali na chama chake.
onyesheni msimamo nanyinyi madaktari sio muanze mambo ya kujipendekeza pendekeza kwa serikali,ingefaa hili likawa fundisho kwa serikali legelege kama hii chini ya CCM.
 
hii serikali ina akili km za mbuni, Mbuni akiona adui anainamisha kichwa chake akdhani amejificha kumbe mwili wote unaonekana, loh!


Aisee! Zumbemkuu, umenikumbusha habari ya mbuni! Mbuni ni ndege mkubwa sana. Mbuni mkubwa hufikia urefu wa FUTI TISA, na uzito wa Kilo 130! Lakini mbuni anachekesha! Akiona adui, anakificha kichwa chake ndani ya mchanga, halafu kiwiliwili chake chote kinakuwa kinaonekana! Ni sawa na Serikali ya JK, inayowatisha waandishi wasitangaze juu ya mgomo wa Madaktari, na kama wakitangaza, wautangaze kwa kupotosha! Serikali ya Mbuni, hiyo!
 
Kwa nini hawa viongozi wetu hawawezi kutoa haki mpaka migomo ipite kwanza? Hawaangalii mwananchi wa kawaida ataumia kiasi gani kabla ya kukubaliana na matakwa ya Madaktari. Wanajibaraguza but the end result, the govt will bow!!!!!

Tiba
 
mnapogoma ni sawa na kuuwa kwa Muda maana watu wakikosa matibabu watakufa huyo mmoja mnaemuacha wa emergency hatoshi......................... ila yote kwa yote nawaunga mkono kwenye kudai haki zenu
 
Back
Top Bottom