Hii kitu ni kama haisomeki vile. Muda huu nasikiliza Dala dala ya Capital Radio, Fadili Haule anasema Muhimbili kama National Hopital hakuna mgomo. Mgomo ulikuwa MOI na Ocean Road. Kwa sasa nipo Moshi, kiukweli kwa KCMC nimeona shughuli zimeendelea kama kawaida. Nilitegemea kusikia kutoka kwa wadau mikoani hali ikoje.
Binafsi kuna maswali kadhaa nashindwa kupata majibu:
1. Inaonekana kama kumeishajitokeza mgawanyiko miongoni mwa madaktari, hii ina tafsiri gani?
2. Inawezekana kweli media zimetumika kupunguza makali ya zoezi hili?
3. Je, ndio kusema Muhimbili National Hosp. sio wanachama wa MAT?
4. Lakini pia, wakati vikao vinaendelea, MAT hawakuwa na mawasiliano na madaktari nchi nzima?
5. Je, ikiwa mgomo utakuwa 'sporadic' hivi, malengo na mahitaji ya hawa wanachama watiifu wa MAT yakafikiwa?
Tulimwona Kigwangala alikuja humu kufafanua kauli yake, ni matumaini yangu viongozi wa MAT wanapita pita humu,waje watufafanulie kadhia hii.