Mgomo wa madaktari

Mgomo wa madaktari

Tuki waajiri wengine msilalamike


Acha upuuzi wewe. Mtu mzima hatishiwi nyau! Kulingana na "World Map scaled by number of Physicians working and Population (LANCET 2004)", Tanzania ina Madaktari wachache sana. Daktari mmoja, anahudumia wagonjwa elfu hamsini (50,000); ratio ambayo ni mbaya kuliko nchi zote duniani! Linganisha na Daktari mmoja Marekani, anayehudumia wagonjwa 390 tu! Katika hali hii, mnasema mtawafukuza madaktari, na kuajiri wengine! Kutoka wapi? Poor Magamba! Nyinyi ndiyo wauaji wa Watanzania maskini!
 
Hii kitu ni kama haisomeki vile. Muda huu nasikiliza Dala dala ya Capital Radio, Fadili Haule anasema Muhimbili kama National Hopital hakuna mgomo. Mgomo ulikuwa MOI na Ocean Road. Kwa sasa nipo Moshi, kiukweli kwa KCMC nimeona shughuli zimeendelea kama kawaida. Nilitegemea kusikia kutoka kwa wadau mikoani hali ikoje.

Binafsi kuna maswali kadhaa nashindwa kupata majibu:
1. Inaonekana kama kumeishajitokeza mgawanyiko miongoni mwa madaktari, hii ina tafsiri gani?
2. Inawezekana kweli media zimetumika kupunguza makali ya zoezi hili?
3. Je, ndio kusema Muhimbili National Hosp. sio wanachama wa MAT?
4. Lakini pia, wakati vikao vinaendelea, MAT hawakuwa na mawasiliano na madaktari nchi nzima?
5. Je, ikiwa mgomo utakuwa 'sporadic' hivi, malengo na mahitaji ya hawa wanachama watiifu wa MAT yakafikiwa?

Tulimwona Kigwangala alikuja humu kufafanua kauli yake, ni matumaini yangu viongozi wa MAT wanapita pita humu,waje watufafanulie kadhia hii.
 
Shame on Bonge wa Clouds FM na kipindi cha Power Break Fast , asubuhi amesema hospitali zote Dar es salaam zinachapa kazi kama kawadida, jamaa yangu amewahi Mhimbili kuchukua namba kwa ajili ya kumwona Dr. saa 9 alasiri akakuta hakuna bonge la mgomo.
 
Shame on Bonge wa Clouds FM na kipindi cha Power Break Fast , asubuhi amesema hospitali zote Dar es salaam zinachapa kazi kama kawadida, jamaa yangu amewahi Mhimbili kuchukua namba kwa ajili ya kumwona Dr. saa 9 alasiri akakuta hakuna bonge la mgomo.


Mkuu hebu weka vizuri hapo kwenye green, ili tukuelewe.
 
Jamani tupatieni updates za mahospitali mengine hapo DSM na mikoani tafadhali?
 
Jamani tupatieni updates za mahospitali mengine hapo DSM na mikoani tafadhali?
mgomo hakuna ila kuna vikao endelevu sasa subiri matokeo ya hivyo vikao endelevu ndio utajua kuna mgomo au la.pigeni propaganda huku watu wakiendelea kufa halafu baadae muanze kuomba kuongea na madaktari.
 
mgomo hakuna ila kuna vikao endelevu sasa subiri matokeo ya hivyo vikao endelevu ndio utajua kuna mgomo au la.pigeni propaganda huku watu wakiendelea kufa halafu baadae muanze kuomba kuongea na madaktari.



Boss hapo kwenye red, unaniambia mimi au Nyoni? Sometimes uwe unasoma kwa makini post za watu, GTs hawakurupuki mkuu!
 
[/COLOR]

Boss hapo kwenye red, unaniambia mimi au Nyoni? Sometimes uwe unasoma kwa makini post za watu, GTs hawakurupuki mkuu!
soma post yako namba 23!!umeandika wewe au umeandikiwa?
 
Poleni kwa kusumbuliwa ni haki yenu kudai haki yenu ila mtuangalie nasisi maskini,

Yaani tunawafikiria sana wanyonge wenzetu watakoathirika ndo maana tulijaribu kwa kila tuwezavyo kutafuta chance tuelewane na waheshimiwa bila kufikia huku
 
nina mgonjwa muhimbili lakini bado ninaamini mna haki ya kugoma kudai haki zenu, wanasiasa wana kauli za utata sana, kazi ya ualimu na kazi ya udaktari kila siku wanaimba eti ni kazi ya wito, loh! siasa ni ajira, proffessional ni kazi ya wito, kaazi kweli kweli.

Shukran kwa support mkuu
 
Kuna mtu katoka Muhimbili kaniambia MOI ndio inaonyesha dhahiri kuwa imeathiriwa na mgomo......mapokezi hakuna wagonjwa na pia kuna mgonjwa amemkuta kaletwa na ambulance tangu saa 12 alfajiri hadi saa tano hajapokelewa.

Moi na ocean road ndo wa kwanza kutusupport na wengine wapo njiani
 
hii serikali ina akili km za mbuni, Mbuni akiona adui anainamisha kichwa chake akdhani amejificha kumbe mwili wote unaonekana, loh!

Nikiangalia serikali yetu na viongozi wake nakumbuka story za mfalme juha
 
Dr. Chichi huku mikoani tunawategemea huko kukoleza nguvu ya moto huu,hebu basi wahimizeni na manesi,famasia,watu wa maabara,nk wawape nguvu!
Ninafahamu fika kuwa bila daktari huduma hakuna lakini hawa kada zingine za afya ni waoga sana....weka bidii moto usambae tumechoka kulipwa sh.10,000 kama on call allowance ya masaa 24 ambayo pia kuipata mpaka iwe birthday ya mkurugenzi!

comrade tupo pamoja,tunachochea moto ukolee watanzania waje wapate huduma bora za afya...support yenu ni muhimu sana kuifanya hii serikali ya mafisadi itusikie.tunajaribu kuwahusisha na wenzetu katika fani ya afya.nesi anauza mpaka drip au sindano ili tu apate nauli,haki iko wapi hapo?..the struggle continues
 
Najua hata mimi au mwanangu au yoyote provided ni binadamu hasa wa hali ya chini atauguwa na tiba yake ni nyinyi ma-DR mnaoendelea na mgomo,lakini kwa hili mi niko upande wenu tena nawaunga mkono kwa asilimia mia,maana siafiki mtu kumfanyisha kazi halafu usimlipe,siafiki mtu kumwambia unatakiwa kupewa nyumba au kupewa asilimia fulani ikiwa ni gharama ya nyumba tu kwa kuwa ofisi husika haina idadi ya nyumba kukidhi mahitaji,siafiki pia kumwambia mtu utalipwa kiasi kadhaa kama allowance ama ya kjuikimu au OT ama vyovyote halafu usitekeleze na ni mtu mzima na akili yake,na hapo anapofanyia kazi ndipo tegemeo lake,familia yake,ndugu zake nk halafu unamwambia ni wito.kama ingelikuwa hivyo nani yuko tayari kufanya kazi huko aliko tofauti na fani hii na asilipwe?au ukisomea fani hii maana yake ni kujitolea bila malipo?kama ni hivyo nani yuko tayari tena kusomea fani isiyokuwa na malipo?hapa tatizo ni serikali na chama chake.
onyesheni msimamo nanyinyi madaktari sio muanze mambo ya kujipendekeza pendekeza kwa serikali,ingefaa hili likawa fundisho kwa serikali legelege kama hii chini ya CCM.

Shukran kwa support
 
Aisee! Zumbemkuu, umenikumbusha habari ya mbuni! Mbuni ni ndege mkubwa sana. Mbuni mkubwa hufikia urefu wa FUTI TISA, na uzito wa Kilo 130! Lakini mbuni anachekesha! Akiona adui, anakificha kichwa chake ndani ya mchanga, halafu kiwiliwili chake chote kinakuwa kinaonekana! Ni sawa na Serikali ya JK, inayowatisha waandishi wasitangaze juu ya mgomo wa Madaktari, na kama wakitangaza, wautangaze kwa kupotosha! Serikali ya Mbuni, hiyo!

He he he kweli kabisa...
 
Japokuwa ushirikiano na wanahabari ni muhimu katika kipindi hiki cha mgomo wa madaktari, lakini inabidi wanahabari waelewe kuwa madaktari hawajagoma ili watangazwe kwenye redio na TV, au wandikwe magazetini! Hivi wanapoambiwa kuwa wapishe mikutano ya ndani kisha watapewa taarifa...halafu wanasusa eti tu kwa sababu wametolewa nje, wanawanyima waTanzania haki yao ya kupata habari.

Lakini habari ni habari tu, ikiwa hot mwandishi atakuja tuu hata hasipoitwa. Hii habari ya mgomo sasa ni hot, na kesho itakuwa hot zaidi, sasa mwandishi hasiyetaka kuuza gazeti au kureport kwenye TV au redio na hasije...kwa kifupi hicho hakitasimamisha mgomo!

nadhani kwa hilo lenu media zote zitatoa habari JF viva la JF..
 
Back
Top Bottom