Mgomo wa madaktari - Updates

Matakwa yao yapi sasa? kuondolewa kwa waziri na naibu wake au yale madai yao ya awali?

Hakuna madai ya awali na madai mapya....mpaka sasa hakuna dai lolote jipya ambalo serikali (Waziri Mkuu) hakupewa February. Kujiuzulu au kuachishwa kqazi kwa Waziri wa Afya na Naibu wake yalikuwepo kata ya madai ambayo WM aliyatolea majibu, na jibu lake lilikuwa amemuachia Rais kutolea uamuzi. Rais aligusia mgomo wa awali kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa February, hakujibu chochote kuhusu uamuzi wake juu ya Waziri wa Afya na Naibu wake...
 
Napata shida sana kuamini habari za mgomo wa madaktari.
...It is simple...pata ajali,vunjika mguu then wakupeleke MOI..utashuhudia kuwa hawa jamaa hawajagoma wala nini bali ni danganya toto tu.
 
Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa, mgomo huu ni wa kisiasa zaidi kuliko masilahi. Madaktari hawana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri, kazi yao ni kutibu. Inanisikitisha sana kuona madaktari wetu wanafanya upuuzi kama huu.

Polee sana mkuu!maana hata ulisemalo haulitambui
 
sikulaumu kwani avatar yako inaeleza unafanya nini
 

Umetushushia heshima walimu!!! Kututaka radhi haitoshi zaidi ya kusitisha mgomo wako wenye chembe lukuki za kisiasa na umimi!!! AFISA UHAMIAJI aliyefiwa na MTOTO wake na MZAZI wake unategemea siku unaenda kugonga PASSPORT yako kwenda BOTSWANA kwenye greener pasture naye akaleta MGOMO wa kibinafsi na wenye chembe za siasa utaenda wewe unakodai kuna maslahi bora? Kwa wakati huo kati ya daktari na afisa uhamiaji nani atakuwa na TAALUMA muhimu ambayo si kama madaktari ambao ndani pamewashinda wanataka torokea nje?.....! Tutumie vichwa kufikiri na si viungo vingine vya mwili!!!
 
Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa, mgomo huu ni wa kisiasa zaidi kuliko masilahi. Madaktari hawana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri, kazi yao ni kutibu. Inanisikitisha sana kuona madaktari wetu wanafanya upuuzi kama huu.

hebu kajitazame kwenye kioo, utakachokiona ndicho kitakuwa tatizo ulilonalo
 

Kwenye red unapotosha umma kuwa makini na siasa za chama cha maandamano kuna mkono wao
 

Uandishi wa kisharobaro haukubaliki hapa JF, hii forum inasomwa na mpaka maprofesa wa chuo kikuu.
 
Madaktari wetu wanatumiwa na vyama vya siasa, mgomo huu ni wa kisiasa zaidi kuliko masilahi. Madaktari hawana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri, kazi yao ni kutibu. Inanisikitisha sana kuona madaktari wetu wanafanya upuuzi kama huu.

Usilo lijua ni kama usiku wa giza.
Kesho utasikia Rais anaenda nje kwa mwaliko maalum na Obama
 
wafuasi wa chama cha maandamano wanafurahi sana kuona nchi inatikisika kwa mgomo huku watu wanakufa.
weka politic pembeni focus kwenye topic watu wanaumia unajua huku wengine wakikenua tu
 
Na usishangae kesho ukasikia ameenda kukusanya net kwa Obama!

Wanatupa neti zenye matundu ambayo hata nzi anapita,alafu sisi tunawapa madini!bora hata wale waliochukua hizo neti na kufanyia uvuvi na ufugaji,maana angalau wanajiongezea kipato hata kama ni kidogo!
 
Pumba Express!!
 

hehehehheh unatania wewe!
Uliona wapi kazi ikalazimishiwa mtu?
Si walishawahi kutishiwa halafu ikawaje?
 

Bilashaka wewe hujafatilia madai ya msingi ya hawa madaktari wetu. Wao wanapambana na serikali ili kuboresha huduma ya afya na kuweza kutatua tatizo la vifo vinavyohepukika. Sijui ulitaka watoe tamko gani, hayo ndiyo mambo ya kisiasa sasa. Mtaalamu amekwambia tukifanya hiki ambacho kipo ndani ya uwezo wetu tutahepuka madhara. Wewe unataka walete matamko hapa. Nao wamechoka kusimamia vifo visivyo vya lazima kutokana na dhamana/taaluma yao.
 
wafuasi wa chama cha maandamano wanafurahi sana kuona nchi inatikisika kwa mgomo huku watu wanakufa.
Wala haisaidii, utasema yote.,. Anaefurahia ni JK manake wanaokufa ni walalahoi wanaomfanya akose usingizi kila kukicha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…