Mgomo mkubwa wanukia nchini

Mgomo mkubwa wanukia nchini

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,867
Reaction score
25,194
Baada ya "Serikali" ya CCM kuamua "kulipa madai" ya walimu huku wakiwabagua watumishi wa kada nyingine (madaktari, manesi, polisi, watumishi wa serikali za mitaa, wanajeshi, askari magereza, na baadhi ya walimu) watumishi hao wameonyesha kukerwa na kukatishwa tamaa na kitendo hicho cha kibaguzi. Aidha, watumishi hao wanashangaa kwanini malipo hayo yamefanyika KISIASA katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ilhali siku zote wamekuwa wakiambiwa hakuna pesa.

Pamoja na hayo, sio walimu wote waliolipwa kwani madai ya baadhi yao yalitupwa kwa kisingizio kwamba hayasomeki vizuri baada ya kupigwa photocopy kwa muda mrefu. "Imagine kuna walimu hawajalipwa madai yao tangu mwaka 1980 hadi wino umefutika kutoka kwenye nyaraka zao halafu wanaachwa bila kulipwa eti nyaraka zao hazisomeki, hii ni haki kweli?!", alisikika akilalamika mwalimu mmoja.

MAONI YANGU
Hili suala la CCM kuwalipa walimu peke yao kwa kisingizio cha wingi wao (kura nyingi) ndicho kitanzi chao mwaka huu. Hii mbinu ni ya kizamani mno.

:yield:
 
Sisiemu itaondoka Kama alivyoondoka firauniii # Achupuchaaa.
 
Hapo kwenye maoni yako ndo haswa ulichokilenga.Waache walimu walipwe na ccm kifo kiko pale pale hakikwepeki.Ivi polisi nao wana malimbikizo?
 
sisi tunangojea hilo pigo la ukawa mlilosema litatokea mbeya,,,,au mlikuwa mnaongelea kuhusu mgombea kushindwa kuongea....
?maana tushachoka na uzushi wenu sasa
 
Hapo kwenye maoni yako ndo haswa ulichokilenga.Waache walimu walipwe na ccm kifo kiko pale pale hakikwepeki.Ivi polisi nao wana malimbikizo?

...na hii hasa ndiyo target ya CCM (kura) ila mwaka huu naona kila ndoano wanayotupa wanaishia kunasa chura au kaa badala ya samaki. mkuu, watumishi wote wa umma, kuanzia wanajeshi hadi wafanya usafi, wanaidai serikali malimbikizo lukuki.
 
Mgomo unanukia kwa mujibu wa maoni yako siyo? huo mgomo unaanza lini?

Kwa hiyo wewe ulitaka walimi wasilipwe ili wakufurahishe wewe.

Toka lini nchi ikaendeshwa kwa maoni yako.
 
Mgomo unanukia kwa mujibu wa maoni yako siyo? huo mgomo unaanza lini?

Kwa hiyo wewe ulitaka walimi wasilipwe ili wakufurahishe wewe.

Toka lini nchi ikaendeshwa kwa maoni yako.

jibu hoja, acha kutoa mipovu kama panya aliyelishwa sumu. katika nchi hii watumishi wanaodai malimbikizo ya madai yao ni walimu tu?
 
Wafanyakazi wote wakataeni CCM siku ya 25.10.2015 ili tuanze ukurasa mpya.
 
jibu hoja, acha kutoa mipovu kama panya aliyelishwa sumu. katika nchi hii watumishi wanaodai malimbikizo ya madai yao ni walimu tu?
Jibu hoja ipi kamanda ebu acha masihala yaani maoni yako ndiyo hoja.
 
Jibu hoja ipi kamanda ebu acha masihala yaani maoni yako ndiyo hoja.

jibu hoja...acha kupaniki.

NCHI HII INA WATUMISHI WANGAPI, MBALI NA WALIMU, WANAOIDAI SERIKALI YA CHAMA CHENU MALIMBIKIZO YA MABILIONI YA MADAI?
 
Back
Top Bottom