MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

Kila siku nasema CCM kumejaa vichwa maji na Serikali yake, yaani madaktari wanaddai haki yao then wanakuja kufutiwa leseni zakoo, hatari kwa kweli na 2015 sio mbali......

Haki yao milioni 7,700,000 kwa mwezi mmeishaambiwa muajiri wako hana uwezo wa kutoa mshahara huo kama mnataka masalahi zaidi ruksa kwenda sehemu ingine wanapolipa vizuri.
 
interns huwa hawana liseni... serikali sasa iache ujinga wa kuhadaa kwani wananchi watajua inawahadaa na chuki itaongezeka

leseni yua practice hutolewa baada ya dr kumaliza intern na kufanya kazi miaka miwili na kuendelea na kupata approval

THIS IS ANOTHER CHEAP LIE TO PEOPLE


Kuna aina tatu ya leseni 1. provisional - inatolewa kwa interns, ni ya miezi 12 na katika kituo kimoja tu 2.temporary- inatolewa baada ya kumaliza intern na inatumika kwa miaka miwili 3. permanent - inatolewa baada ya kupractice miaka miwili.

Imefika wakati watu wa JF tuanze kuchangia kunakuweza kuwasaidia interns wahusika na sio kubwabwaja tu. Kubwabwaja hakutamsaidia yeyote kati ya waliofutiwa leseni. Kumbuka kwako wewe hii ni habari tu, lakini kwa aliyefutiwa leseni hili ni tukio la kukumbwakwa maishani.
 
regulatory body imefanya kinachotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu walizojiwekea. mtu kama haridhiki na huu uamuzi aende kwene ngazi ya juu zaidi..huo ndio utawala bora!. maana it seems tunataka kuishi kwene taifa ambalo kila mtu ni rais na anadai haki ya kujiamulia nini afanye na nini asifanye. hatupo ngomani wajameni kwamba waingia na kutoka kiholela..pamoja na unyeti wa fani ya udr na uchache wao, wao pia lazma waone umuhimu wa kufuata sheria na taratibu zilzopo, it is common sense hatuwezi kuruhusu kila mtu afanye anavotaka, hata kama inaumiza.
 
Haki yao milioni 7,700,000 kwa mwezi mmeishaambiwa muajiri wako hana uwezo wa kutoa mshahara huo kama mnataka masalahi zaidi ruksa kwenda sehemu ingine wanapolipa vizuri.
Kwa hili Ritz tupo pamoja.....sheria ni msumeno...ukitaka kazi zinazoruhusu kugoma kafanye ukuli bandarini...una hiari ya kusomea udaktari na kuamua kufanya kazi serekalini lakini huna hiari ya kuhudumia wagonjwa....sheria iko hivyo na mnaowatetea msiwadanganye wataishia kutimuliwa wote.. kama mnawapenda waambieni ukweli na kwasasa hawana haja ya kugoma kwani wameshaambiwa hawana haja ya kugomea 7.7 ambayo haipo na wala haitakaa itolewe....
 
Haki yao milioni 7,700,000 kwa mwezi mmeishaambiwa muajiri wako hana uwezo wa kutoa mshahara huo kama mnataka masalahi zaidi ruksa kwenda sehemu ingine wanapolipa vizuri.

Ritz, kuna makosa yamefanyika, lakini kuhusu interns nakuomba tujaribu kuangalia swala tofauti kidogo. Lets do a little bit more kuhusu hawa interns. Tukumbuke kuwa interns wako katika kujifunza, kujifunza sio kutibu tu bali hata jinsi ya kuishi kazini. Sasa hawa wanaowafundisha kazi wamewaambia kuwa hapa mambo ni kugoma, interns hawezi kumbishia senior wake anayemfundisha. Kumbuka wamekabishidwa kwa registrars na specialists ili wawafundishe na wao wamewafundisha kugoma.
 
Unganisha huu mtandao kwa makini:
Mkiti wa baraza la madaktari Tz ni dr. Donan Mmbando,
Acting Chief Medical Officer (CMO) ni dr Donan Mmbando
Mkurugenzi wa idara ya Kinga ni dr Donan Mmbando

halafu, Kama CMO ndiye aliye draft barua ya Wizara kuwashitaki interns kwa baraza, na ndiye aliyefanya uamuzi wa kuwafutia leseni kama Mkiti aw baraza

Pia, kiprotokali ni dr Donan Mmbando ndiye huipatia ikulu pamoja na waziri wa afya majibu ya maswali yanayohusu mgomo. Kwa maneno mengine ukiona serikali ikitoa kauli yoyote kuhusu mgomo, hiyo kauli imeandaliwa na dr Donan Mbando

Dr Donan Mmbando kama CMO ndiye anayetakiwa kuhakikisha upungufu wa madaktari Tz unakwisha
.
Mkiti wa baraza la madaktari anachagulia na madaktari au unateuliwa na serekali? Kama anachaguliwa na doctors then ni vizuri atupwe nje huyu hasimami maslahi ya madaktari.
 
regulatory body imefanya
kinachotakiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu
walizojiwekea. mtu kama haridhiki na huu uamuzi aende kwene ngazi
ya juu zaidi..huo ndio utawala bora!. maana it seems tunataka kuishi
kwene taifa ambalo kila mtu ni rais na anadai haki ya kujiamulia nini
afanye na nini asifanye. hatupo ngomani wajameni kwamba waingia na
kutoka kiholela..pamoja na unyeti wa fani ya udr na uchache wao, wao pia
lazma waone umuhimu wa kufuata sheria na taratibu zilzopo, it is common
sense hatuwezi kuruhusu kila mtu afanye anavotaka, hata kama
inaumiza.
Ilichofanya serikali ni sawasawa,hawa watoto hawajui kama serikali ipo! wanafanya watakacho kiholela tu, wacha sasa wasage rumba mtaani mpaka visigino viende upande! wanafata mkumbo tu kazi yenyewe hawajapata, haya sasa! hawajui mgoma u,meathiri watu kiasi gani! watalijua jiji.
 
.
Mkiti wa baraza la madaktari anachagulia na madaktari au unateuliwa na serekali? Kama anachaguliwa na doctors then ni vizuri atupwe nje huyu hasimami maslahi ya madaktari.
dugu, elewa kwanza dhima ya regulatory bodies..uskurupuke.
 
hawawezi wakafanya suluhu kwa mtindo huu

Unataka suluhu gani tena wakati Madaktari ndio wameanzisha mgomo wakitaka mshahara mkubwa wewe ulikuwa unataka wanachotaka madaktari wanachotaka wapewe tu sababu ni madaktari serikali hawezi kutoa milioni 7.700.000 subirini Chadema wakichukuwa nchi watawalipa milioni 10.
 
Unganisha huu mtandao kwa makini:
Mkiti wa baraza la madaktari Tz ni dr. Donan Mmbando,
Acting Chief Medical Officer (CMO) ni dr Donan Mmbando
Mkurugenzi wa idara ya Kinga ni dr Donan Mmbando

halafu, Kama CMO ndiye aliye draft barua ya Wizara kuwashitaki interns kwa baraza, na ndiye aliyefanya uamuzi wa kuwafutia leseni kama Mkiti aw baraza

Pia, kiprotokali ni dr Donan Mmbando ndiye huipatia ikulu pamoja na waziri wa afya majibu ya maswali yanayohusu mgomo. Kwa maneno mengine ukiona serikali ikitoa kauli yoyote kuhusu mgomo, hiyo kauli imeandaliwa na dr Donan Mbando

Dr Donan Mmbando kama CMO ndiye anayetakiwa kuhakikisha upungufu wa madaktari Tz unakwisha

nchi hii bwana!!! anaelalamika ndio huyohuyo,anaetengeneza hati ya mashitaka ndio huyohuyo na anaeotoa hukumu ndio huyohuyo,sasa utegemee haki itatendeka kweli???
 
huu ni uonevu........nina uhakika hao interns walifuata msimamo wa seniors wao, kwa wao ni vigumu sana kusimama mmoja mmoja, kwa nini serikali inaumiza kichwa kwa hao vijana wanaojifunza .........mi nadhani serikali inajivunia uwepo wa intake nyingine ya interns ndani ya miezi miwili ijayo.
 
Mimi napita tu naelekea shamba kucheki mazao,ila serikali inafikiri hao madaktari waliokuwa kwenye mafunzo kwa vitendo wangeendelea vp na mafunzo ili hali waalimu wao ambo ni madaktari walikuwa wamegoma? Huo ni mchemsho. Unakimbilia kukata majani unaacha shina.Dhaifu nyie
 
Again swala la kuwafukuza kazi vijana walioingia internship bado inanitatiza kabisa..hawa vijana bado wanajifunza Udaktari kwa vitendo na sidhani kama ni wahusika hasa wa mgomo uliotokea isipokuwa wameshiriki ktk mgomo sawa na madaktari wengineo. Iweje hawa ndio waondolewe tena kabla ya uchunguzi kukamilika kujua chanzo ama nini suluhu ya mgomo mzima?.

Nijuavyo siku zote kamakweli kuna sababu ya kusimamisha watu kazi basi kuanza na viongozi, sasa iweje kuna kesi mahakamani ambayo Dr. Namala Mkopi ameshtakiwa kama kiongozi na mgomo naye ameyakana madai hayo hivyo nashindwa kuelewa huu uamuzi umetoka vipi hata kabla ya mahakama kuwaweka hatiani maana hata hiyo sheria ya Madaktari kifungu cha 15(2) sura ya 152 kitatafsiriwa mahakamani kwa ushahidi wa pande mbili zote...

Yes, sisi wengine tulipingana na uamamuzi wa madaktari kugoma kutokana na madai ya ongezeko la mshahara ambao hawakutaka kabisa ku negotiate isipokuwa kwa kiwango walichotaka wao kulingana na kazi zao lakini pia kazi hii inachukua ngazi tofauti kabisa ya uwajibikaji maana sii kazi kama kazi nyinginezo. Ni sawa na rubani anayeachia kuongoza ndege ikiwa angani kwa madai ya mshahara au jambo lolote lenye maana. Hapo huipoteza haki yake na kuitwa Hijacker hata kama yeye ni mwajiriwa wa shirika la Ndege..

Tunahitaji sana hawa vijana wetu, vita ya kuondokana na adui Maradhi haiwezi kwenda hivyo hata kidogo maana tunapigana sasa wenyewe kwa wenyewe. Tunaiomba serikali ifikirie upya swala na maombi ya madaktari nina imani wataweza kufikia makubaliano bila kulipelekea Taifa mahala pabaya zaidi kwa sababu Madaktari wote wanaweza kugoma kama walivyofanya mgomo wa kwanza kwa kudai tena vijana wa Internship warudishwe Dar (kama sikosei).. Tunarudishwa kulee tulikotoka!..

Tangazo hili limekuja wakati mbaya sana na hapakuwa na sababu kabisa ya kuharakisha kabla ya makubaliano au maamuzi ya mahakama kufikiwa..
 
Good grief! Regulatory body run amok. Where are the checks and balances? This is unwarranted and total misuse of regulatory powers.
akili za wadanganyika zimelemazwa na siasa..check and balance ndio kufuata sheria. run amok kwa kufuata sheria na taratibu ilizojiwekea na kuthibitishwa na bunge?
 
Unganisha huu mtandao kwa makini:
Mkiti wa baraza la madaktari Tz ni dr. Donan Mmbando,
Acting Chief Medical Officer (CMO) ni dr Donan Mmbando
Mkurugenzi wa idara ya Kinga ni dr Donan Mmbando

halafu, Kama CMO ndiye aliye draft barua ya Wizara kuwashitaki interns kwa baraza, na ndiye aliyefanya uamuzi wa kuwafutia leseni kama Mkiti aw baraza

Pia, kiprotokali ni dr Donan Mmbando ndiye huipatia ikulu pamoja na waziri wa afya majibu ya maswali yanayohusu mgomo. Kwa maneno mengine ukiona serikali ikitoa kauli yoyote kuhusu mgomo, hiyo kauli imeandaliwa na dr Donan Mbando

Dr Donan Mmbando kama CMO ndiye anayetakiwa kuhakikisha upungufu wa madaktari Tz unakwisha
Kama ni ya kweli hayo mkuu basi hakuna la maana wala sheria kufuatwa haipo! mtu mmoja anafanya maamuzi anajigeuza kutetea hao hao aliowadhurumu pamoja na makadhia kibao! Lol
 
Ritz, kuna makosa yamefanyika, lakini kuhusu interns nakuomba tujaribu kuangalia swala tofauti kidogo. Lets do a little bit more kuhusu hawa interns. Tukumbuke kuwa interns wako katika kujifunza, kujifunza sio kutibu tu bali hata jinsi ya kuishi kazini. Sasa hawa wanaowafundisha kazi wamewaambia kuwa hapa mambo ni kugoma, interns hawezi kumbishia senior wake anayemfundisha. Kumbuka wamekabishidwa kwa registrars na specialists ili wawafundishe na wao wamewafundisha kugoma.

Nakubaliana na wewe kuwa kuna makosa ambayo yamefanyika. Hawa maiterns wako chini ya uangalizi wa maseniors wao. Hawa maseniors ndio walioamua mgomo na kuwakataza maitern kwenda kazini, kwa sababu kuna maitern waliokuwa wamekwenda kuripoti kazini na seniors wao wakawaeleza kuwa wao ndio hawataki mgomo na kuwashurutisha waondoke mawadoni.

Ni vyema maseniors wakaliangalia vizuri suala hili na waone namna gani wanaweza kuwasaidia vijana hawa. Pili vijana hao hawajapata muda wa kuhojiwa na hilo baraza licha ya kuandika barua za kujieleza. Nani alizipitiabarua hizo katika kipindi cha siku nne. Jopo la maamuzi la kuwafutia hawa maitern zile leseni zao liliundwa na nani? Hivi kweli kuna haki hapo?

Dr. Mbando hajui kama sio mgomo asingeupata huo Ag. CMO. Hivi anatarajia kuthibitishwa kwa maamuzi yake ya kijinga hayo? Kwa upande wangu ni vizuri mamlaka husika ikaangalia vizuri suala hili kwa ujumla wake. huwezi ukamfukuza mtu bila ya kupatiwa onyoau onyo kali.

Fuateni namna vyuo vikuu vinavyoshughulikia migomo otherwise kusingekuwa na wanafunzi vyuoni maana wangekuwa wanawafukuzan wote kila siku. Tuige mfano wa nchi ya Kenya na mgomo wa manesi pamoja na madaktari wao.
 
MGOMO:Madaktari 319 wafutiwa leseni
Waandishi Wetu
BARAZA la Madaktari Tanganyika limewafutia usajili madaktari wote waliokuwa katika mafunzo ya vitendo (Internship), baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mgomo wakiwa kazini.Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa Dar es Salaam jana imeeleza kuwa madaktari 319 wamepoteza sifa ya kuendelea na taaluma hiyo hivyo usajili wao umesitishwa rasmi kuanzia jana.Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk Donan Mmbando amewataka madaktari hao kurudisha hati zao za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari.

“Kwa kuzingatia masharti ya sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhia kwamba madaktari wote ambao walijihusisha na mgomo, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012.”

“Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya terehe 17 Julai, 2012.”

Dk Mmbando alisema, awali Baraza hilo lilipokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba baadhi ya madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kati ya Juni 23 na Juni 29 mwaka huu.

Alisema madaktari hao walipangiwa kutoa huduma katika Hospitali za Muhimbili, KCMC, Rufaa Mbeya, Sekou Toure na Bugando za Mwanza, Amana, Temeke na Mwananyamala za Dar es Salaam, Haydom - Arusha, St Francis-Ifakara na Dodoma.

Alisema kutokana na mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo huo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Dk Mmbando alisema kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa kwenye Baraza hilo, Msajili wa Baraza, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la kufanya Uchunguzi dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Alisema baada ya kuyafanyia kazi malalamiko hayo, Baraza limebaini kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda.

Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (MAT), Dk Edwin Chitage alisema alikuwa hajapata rasmi taarifa hizo licha ya kusikia fununu... “Sijapata taarifa rasmi lakini ni jambo tulilolitarajia na hatutashangaa tukisikia hilo kwa sasa subiri nithibitishe halafu nitatoa msimamo wetu.”
Kiongozi wa madaktari kortini

Katika hatua nyingine, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kudharau amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi ya kuwataka kusitisha mgomo kupitia vyombo vya habari.

Amri hiyo ilitolewa Juni 22, mwaka huu na Jaji Sekela Moshi na kuwataka madaktari kurejea kazini mara moja, lakini amri hiyo haikutekelezwa.

Jana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alimsomea Dk Mkopi hati ya mashtaka na kumweleza Hakimu Faisal Kahamba kuwa kati ya Juni 26 na 28, mwaka huu, Dk Mkopi akiwa Rais wa MAT, alidharau amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi Juni 26, mwaka huu ikimtaka kutoa tangazo kwa wanachama wa chama hicho kupitia vyombo vya habari kwamba wasishiriki katika mgomo.

Kweka alidai kuwa Juni 27, mwaka huu Dk Mkopi aliwashawishi wanachama kushiriki kufanya mgomo kitu ambacho ni kinyume na amri iliyotolewa Juni 26, mwaka huu.

Hata hivyo, Dk Mkopi alikana mashtaka hayo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kiongozi huyo wa madaktari yupo nje kwa dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 8, mwaka huu itakapotajwa na kuangaliwa kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.

Afya ya Dk Ulimboka
Wakati huo huo, afya ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka imezidi kuimarika.
Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitage alisema jana kwamba: “Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, kwa sasa afya yake imezidi kuimarika, anakula mwenyewe lakini pia anazungumza mwenyewe na rafiki zake wa hapa nchini kwa njia ya simu.”

Katika siku za karibuni, hali ya Dk Ulimboka ilielezwa kubadilika ghafla na kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kutokana matatizo mbalimbali, yaliyotokana na kupigwa ikiwamo figo kushindwa kufanya kazi.

Alisafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi Juni 28, mwaka huu kwa ushauri uliotolewa na jopo la madaktari lililokuwa likimhudumia.

UN yanena
Katika hatua nyingine, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Dk Alberic Kacou amepokea barua ya MAT kuomba ulinzi kwa Dk Ulimboka anayeendelea na matibabu Afrika Kusini kwa madai kuna kikosi kilichotumwa kuhakikisha harudi nchini akiwa hai.

Akizungumza jana Dar es Salaam jana, Dk Kacou alisema suala hilo la kutoa ulinzi watalitoa baada ya kuwasiliana na wote waliohusishwa kwenye waraka wa ombi hilo.

Mgomo wamalizika
Mgomo uliokuwa ukiendelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Mifupa (Moi), Dar es Salaam umemalizika na huduma katika hospitali hizo zimerejea kama kawaida jana.

Waandishi wa habari waliotembelea hospitali hizo waliona wagonjwa wakiwa wanaendelea kupokewa na kupatiwa huduma kama ilivyokuwa awali, kabla ya mgomo uliodumu kwa takriban majuma mawili yaliyopita
Habari hii imeandikwa na Tausi Mbowe, Tausi Ally, Leon Bahati na Issa Lazaro, Geofrey Nyang’oro
Source gazeti la mwananchi
Huwezi kukimbia tatizo kwa mtindo huo! :thumbdown:
 
Back
Top Bottom