Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli


JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
14,025
Likes
7,992
Points
280

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
14,025 7,992 280
Basi bwana,
Hili bandiko sikuliona mwaka 2014.
Ulimfahamu vizuri sana huyu Ndugu Mkulu wetu!

..fuatilia hotuba zake haswa wakati wa ufunguzi wa miradi ya ujenzi utasikia akitupa vijembe ambavyo tafsiri yake ni kuwa haamini ktk demokrasia yetu ya vyama vingi na uhuru wa kujieleza.

..lakini pia utaona kwamba ni mwanasiasa asiye mkweli anaye-take advantage ya uelewa mdogo wa wananchi.

..Vilevile ana tabia ya kuwazushia na kuwalisha maneno wale wote wasiokubaliana na hoja au maamuzi yake.
 

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
11,155
Likes
29,626
Points
280

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
11,155 29,626 280
..fuatilia hotuba zake haswa wakati wa ufunguzi wa miradi ya ujenzi utasikia akitupa vijembe ambavyo tafsiri yake ni kuwa haamini ktk demokrasia yetu ya vyama vingi na uhuru wa kujieleza.

..lakini pia utaona kwamba ni mwanasiasa asiye mkweli anaye-take advantage ya uelewa mdogo wa wananchi.

..Vilevile ana tabia ya kuwazushia na kuwalisha maneno wale wote wasiokubaliana na hoja au maamuzi yake.
Hakuna kipindi nilichowahi kukata tamaa kama hiki.
Naona giza kali sana huko mbele;I hope i am wrong!
 

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
26,303
Likes
26,252
Points
280

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
26,303 26,252 280
Wewe umtakii mema Prof Mbarawa.
Mkuu, ingekuwa JF ndio tunafanya vetting, hapo ndio ungesema tunamharibia!. Ingekuwa JF tunaweza kumharibia mtu, soma bandiko hili ni la lini, na tulisema nini humu, na bado, akawa.

Kauli huumba, ukimuumbia kauli njema, the right man, linakuja kutokea kweli. By the time bandiko hili linapanda, usikute hata jamaa mwenyewe hakujua kuwa atakuja kuwa yeye!.

P
 

Getstart

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
6,092
Likes
667
Points
280

Getstart

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
6,092 667 280
Mkuu, ingekuwa JF ndio tunafanya vetting, hapo ndio ungesema tunamharibia!. Ingekuwa JF tunaweza kumharibia mtu, soma bandiko hili ni la lini, na tulisema nini humu, na bado, akawa.

Kauli huumba, ukimuumbia kauli njema, the right man, linakuja kutokea kweli. By the time bandiko hili linapanda, usikute hata jamaa mwenyewe hakujua kuwa atakuja kuwa yeye!.

P
Mazingira ya sasa ni tofauti. Tetesi kidogo zinaweza kuchukuliwa ni uasi...
 

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
6,165
Likes
8,177
Points
280

britanicca

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
6,165 8,177 280
This is a figment of your own imagination; na hiyo source yako imekwambia njozi zake tu kulingana na vested interests zake kisiasa; CCM ni taasisi kubwa yenye factions nyingi zenye interests tofauti tofauti ambazo lazima zipitie mizengwe na minyukano mingi kabla ya kufikia uamuzi! kumbuka a week in politics is a very very long time! Ukianza kuamini sasa hivi kwamba John "Pombekali" Magufuli ndie atakuwa mgombea wa CCM come 2015; that is too far fetched!!!
ulizingua wewe
 

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Messages
3,315
Likes
3,194
Points
280

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2015
3,315 3,194 280
Wanabodi,

Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi tuliyepotezana naye Kipindi kirefu, ambaye ni mtu wa sehemu na wa kuaminika sana ambaye yuko attached CCM kama kada tuu wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha, zimenisikitisha, kunihuzunisha, kuniogopesha, kunisononesha na kuninyongonyeza!, kuwa eti imeishaamuliwa (sitaji imeamuliwa na nani), kuwa mgombea wa urais wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli!.

Kilichonistua, kunitisha, kunihuzunisha, kunisikitisha, kunisononesha, kunigopesha na kuninyongoneza ni the reasons behind alizonitajia za why ni Magufuli, ambazo ndizo zimepelekea the inner core ya CCM kuamua mgombea wake wa urais wa 2015 ni lazima awe John Pombe Magufuli tuu, and no one else!.

Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi kweli ni justifiable na nyingine sio tuu ni unjustifiable!, bali hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!. Naomba kwa sasa nisizitaje kwanza hizo sababu, kwa sababu habari zenyewe nimezisikia from a single source, nahitaji kwanza kufanya verification kwa ku double check, na ku cross check ikiwemo kupata a collaborative verification na attribution ya third parties ili nijiridhishe kuwa hii ni habari za kweli na kuthibitisha kuwa kumbe hivyo ndivyo the inner core ya CCM inavyoweza kufikia maamuzi ya mgombea wake based on sababu nilizo tajiwa!, then nitaziweka hadharani hizo sababu za kwa nini CCM imeamua mgombea wake wa 2015 lazima awe ni Magufuli tuu!, na kiukweli mkizisikia hata nyinyi mtashangaa!.

Kwa kawaida sisi waandishi, ukipata taarifa kama hii, huwa inaitwa "a news tip", haukimbilii kuiandika mbio mbio mpaka kwanza uifanyie verification kwa kui double check na kui cross check ili kujiridhisha kwa kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe, baada ya kuthibitisha na kujiridhisha ndipo unaiandika.

Lakini kwa vile sasa tunaishi kwenye "the world of information age", nimeamua kuileta hii "news tip" humu jf, hivi hivi ikiwa kwenye hatua ya "tip" kabla hata ya verification, ili wewe kama mwana JF, uipate ile JF advantage ya "be the first to know!", hivyo nawaombeni tuu sasa wana jf mkae mkijua kuwa "Mgombea wa urais wa CCM kwa mwaka 2015 ni John Pombe Magufuli!".

Hili la kuamua ni Magufuli, limenistua kidogo kwa sababu kwa sisi tuliomfuatilia Magufuli utendaji kazi wake kwa kauli na matendo, huyu mtu ameonyesha sio mzima sana kichwani!, anafanya baadhi ya maamuzi na jazba, papara na kukurupuka mtindo wa liwalo liwe, mwisho wa siku yanakuja kutu cost, hivyo akipita na kuwa rais wa nchi, you can just imagine, atafanya maamuzi mangapi ambayo yatatucost kama taifa, ila pia ana chance ya kuja kuwa the worst dictator this nation has ever had!.

Nikiisha "confirm" neno "tetesi" litaondolewa na kuwa replaced na neno "confirmed!", na nitaziweka hizo sababu ili sasa ndio zijadiliwe!, na nawahakikishia wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, mkizisikia hizo sababu za huyo kada wa CCM alizonipa kwa nini ni Magufuli!, na nyinyi pia zitawashitua, zitawatisha, zitawaogopesha, kuwahuzunisha, kuwasikitisha, kuwasononesha na kuwanyongonyeza!.

Naomba nisiwatajie jina la huyo source wangu chini ya kinga ya kihabari kwa ma source inayoitwa "The Confidentiality of the source", na hapa wakati naileta taarifa hii humu jf, kwa vile zoezi la kumteua mgombea wa CCM bado liko mbali hadi mwaka ujao, unaweza kukuta hata Magufuli mwenyewe bado hajui kuwa ni yeye ndie atakuwa mgombea wa CCM, kwa sababu walio amua kuwa ni Magufuli sio kikao chochote rasmi na halali ndani ya CCM bali ni "The Inner Circle" hivyo hii ni tip from the deep inside ya "the inner circle", na bahati mbaya sana, Magufuli mwenyewe hayuko kwenye hiyo "the inner circle!".

NB. Sio kila thread ni lazima ichangiwe, saa nyingine itoshe kujisomea tuu na kujipitia bila kuchangia chochote!. Hii ni just a news tip, kwa vile nimewaahidi naifanyia verification kuithibitisha, nawaombeni msiniulize swali lolote at this stage, kwa sababu sitajibu chochote!, and if possible nawashauri na nyingi msome FYE only na sio lazime mchangie kwa sasa na badala yake mvute subira kusubiria verification.

Sababu ya kuiwahisha humu JF kabla ya verification ni ili tuu wewe kama mwana JF to be the first to know!. Information is power!, if you are the first to know, then you'll have the powers to make good things happen or not to happen if they are bad things!.

Asante.
Paskali


Update: 12/07/2015

Leo hili limetimia ni kweli aliyepita ni Magufuli, nimezitafakari sababu nilizotajiwa ile siku napewa tetesi hii, na kuzipima na hiki kilichotokea, nimejikuta nimelazimika kutoziamini kuwa zile nilizosikia ndizo sababu zenyewe halisi.

Kwa sisi waandishi tuna kanuni, ukilisikia jambo, lipime uliamini ndipo uliandike, kama huliamini, then usiliseme wala kuliandika, hivyo hizo sababu nilizopewa siku hiyo, on why ni Magufuli, mimi siziamini, naomba nisiziseme kabisa, hivyo naomba tuchukulie bandiko hili nilijiandikia tuu kuwa atakuwa Magufuli, na kupitishwa kwa jina la John Pombe Magufuli, has nothing to do na sababu nilizotajiwa, bali kuhesabike kumetokea tuu naturally, by chance, bila any pre meditated moves, na hili bandiko lichukuliwe tuu kama just a coincidence, kuwa nilisema mgombea wa CCM atakuwa ni Magufuli na kweli ikatokea tuu coincidentally, mgombea wa CCM akawa kweli ni Magufuli.

Kwa mtakaonielewa asanteni kwa kunielewa, na kwa msio nielewa poleni na samahanini sana!.

Hongera sana John Pombe Joseph Magufuli kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM.

Paskali
Hongera kwa unabii na mafunuo mema juu ya dereva wa tipper.
 
Joined
Feb 27, 2018
Messages
44
Likes
110
Points
40
Joined Feb 27, 2018
44 110 40
Mgombea awe Bernard, awe Edward, Awe Samuel, awe John hata Harrison wote hao si suluhisho la ufukara, umasikini, ufisadi na matatizo yote tunayokabiliana nayo Watanzania...

Wote hao ni watoto wa baba mmoja wanaojivika tu mavazi tofauti, wote wapo kwa maslahi ya kutetea na kulinda sera na ilani za CCM...

Kama kutatokea mwanadamu atakayeingia kwenye fikra zetu na kubadilisha mitizamo yetu sisi Watanzania basi mtu huyo ndiye atayestahili kuwa kiongozi wa nchi...

Hawa mnaowataja kwao wao jukumu la kwanza ni kutetea chama chao (CCM), pili kutetea maslahi yao halafu tatu na mwisho ndio wanawakumbuka wananchi...

Bahati mbaya sana sisi Watanzania ni watu tusiojitambua, leo tunaweza kuonesha mahaba ya dhati kwa mtu fulani kwa shangwe na vigelegele lakini kitambo kidogo tu kijacho tutamtusi yule bwana tuliyempenda kwa roho na nafsi zetu na kumuona hafai...

Kiongozi akiwajibika kuyafanya yanayomfanya awe kiongoi wa nafasi fulani basi mtu huyo tutamuona Mungu mtu, tutapiga zumari na kupaza sauti kuwa huyu ndiye afaaye kwa kumpamba lakini tunasahau kwamba huyu katimiza tu wajibu wake na sio kwamba kafanya jambo la ziada...

Huwezi kukesha na kulisifia paa la nyumba yako kuwa limekukinga na mvua pamoja na jua, utaonekana mwehu kwa kuwa hizo ndio kazi za paa...lakini utaonekana wa maana kama paa hilo likikukinga na tufani ya kimbuka na dhoruba maana hapo limefanya kazi ya ziada.

Uwajibikaji thabiti pekee wa kina John, Edward, Bernard hauwafanyi kuwa ndio watu stahiki kwa uongozi wa nchi, uongozi wa nchi una zaidi ya kutimiza majukumu.

Hebu tujiulize hali za majimbo ya uchaguzi za hawa mabwana zikoje, wamefanya nini huko majimboni mwao, wametatua kero zipi, wamekuwa madarakani kwa nafasi za ubunge kwa muda gani...?

Ngoja niishie hapa....
This is deep.
 

Forum statistics

Threads 1,203,977
Members 457,048
Posts 28,136,708