Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli | Page 15 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Aug 15, 2014.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,668
  Likes Received: 23,949
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi tuliyepotezana naye kipindi kirefu nyuma, ambaye ni mtu wa sehemu na wa kuaminika sana ambaye yuko attached CCM kama kada tuu wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha, zimenisikitisha, kunihuzunisha, kuniogopesha, kunisononesha na kuninyongonyeza!, kuwa eti imeishaamuliwa (sitaji imeamuliwa na nani), kuwa mgombea wa urais wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli!.

  Kilichonistua, kunitisha, kunihuzunisha, kunisikitisha, kunisononesha, kunigopesha na kuninyongoneza ni the reasons behind alizonitajia kada huyu za why mgombea wa CCM ni Magufuli, ambazo ndizo zimepelekea the inner core ya CCM kuamua mgombea wake wa urais wa 2015 ni lazima awe John Pombe Magufuli tuu, and no one else!.

  Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi kweli ni sababu za msingi na ziko justifiable kwa any reasonable man, sababu nyingine alizonitajia sio tuu ni unreasonable, bali pia ni unjustifiable! na hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!.

  Naomba kwa sasa nisizitaje kwanza hizo sababu nilizotajiwa za kwa nini ni Magufuli, kwa sababu habari zenyewe nimezisikia juu juu tuu tena from just a single source, hivyo nahitaji kwanza kujiridhisha kwa kufanya verification kwa ku double check, na ku cross check ikiwemo kupata a collaborative verification na attribution ya third parties ili nijiridhishe kuwa hii ni habari za kweli na kuthibitisha kuwa kumbe hivyo ndivyo the inner core ya CCM inavyoweza kufikia maamuzi ya mgombea wake wa urais based on sababu nilizo tajiwa!, then nitaziweka hadharani hizo sababu za kwa nini CCM imeamua mgombea wake wa urais kwa uchaguzi wa 2015 lazima awe ni John Pombe Magufuli tuu na sio mtu mwingine yoyote!, na kiukweli mkizisikia hizo sababu nilizotahiwa, naamini hata nyinyi mtashangaa!.

  Kwa kawaida sisi waandishi wa habari, ukipata taarifa kama hii, huwa inaitwa "a news tip", haukimbilii kuiandika mbio mbio mpaka kwanza uifanyie verification kwa kui double check na kui cross check ili kujiridhisha kwa kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe, baada ya kuthibitisha na kujiridhisha kuwa ni kweli, ndipo unaiandika.

  Lakini kwa vile sasa tunaishi kwenye dunia ya taarifa moto moto, "the world of information age", ukipokea tuu taarifa, unashare na wenzio, ndio maana na mimi nimeamua kuileta humu jf hii "news tip" hivi hivi ilivyo ikiwa kwenye hatua ya "tip" kabla hata ya verification, ili wewe kama mwana JF, uipate ile "JF advantage" ya "be the first to know!", yaani ukiwa mwana jf, unakuwa wa kwanza kujua, hivyo nawaombeni tuu sasa wana jf mkae mkijua kuwa "Mgombea wa urais wa CCM kwa mwaka 2015 ni John Pombe Magufuli!".

  Hili la kuamua ni Magufuli, limenistua kidogo kwa sababu kwa sisi tuliomfuatilia utendaji kazi wa Magufuli kwa kauli na matendo tangu akiwa waziri, mtu huyu ameonyesha wazi sio mtu mzima sana kichwani in terms of stability in decision making!, amefanya baadhi ya maamuzi mengi tuu kwa jazba, pupa, papara na kukurupuka kwa mtindo wa nimeamua mimi na liwalo liwe!, mwisho wa siku baadhi ya maamuzi yake ambayo mengine ni very national yanakuja kutu cost sisi kama taifa, mifano ipo, ikiwemo kuvunjwa ile Petro Station Mwanza, Uuzaji wa nyumba za serikali, Samaki wa Magufuli, just to mention but few, hivyo akipita na kuwa rais wa nchi hii, kama huu ndio mfumo wake wa kufikia maamizi, then you can just imagine, akiwa rais, atafanya maamuzi mangapi ambayo yatatucost kama taifa, ila pia kwa hulka yake, ana chance ya kuja kuwa the worst dictator this nation has ever had!. Tuombe Mungu asaidie, hili likitimia, huyu mtu abadilike, vinginevyo.. !.

  Nikiisha "confirm" neno "tetesi" litaondolewa na kuwa replaced na neno "confirmed!", na nitaziweka hizo sababu nilizotajiwa ili sasa ndio zijadiliwe!, na nawahakikishia wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, mkizisikia hizo sababu za huyo kada wa CCM alizonipa kwa nini ni Magufuli!, na nyinyi pia zitawashitua, zitawatisha, zitawaogopesha, kuwahuzunisha, kuwasikitisha, kuwasononesha na kuwanyongonyeza!.

  Naomba nisiwatajie jina la huyo source wangu chini ya kinga ya kihabari kwa ma source inayoitwa "The Confidentiality of the source", na hapa wakati naileta taarifa hii humu jf, kwa vile zoezi la kumteua mgombea wa CCM bado liko mbali hadi mwaka ujao, unaweza kukuta hata Magufuli mwenyewe bado hajui kuwa ni yeye ndie atakuwa mgombea wa CCM, kwa sababu walio amua kuwa ni Magufuli sio kikao chochote rasmi na halali cha Chama Cha Mapinduzi, CCM bali ni "The Inner Circle" hivyo hii ni tip from the deep inside ya "the inner circle", na bahati mbaya sana, Magufuli mwenyewe hayuko kwenye hiyo "the inner circle!".

  NB. Sio kila thread ni lazima ichangiwe, saa nyingine itoshe kujisomea tuu na kujipitia bila kuchangia chochote!. Hii ni just a news tip, kwa vile nimewaahidi naifanyia verification kuithibitisha, nawaombeni msiniulize swali lolote at this stage, kwa sababu sitajibu chochote!, and if possible nawashauri na nyingi msome FYE only na sio lazime mchangie kwa sasa na badala yake mvute subira kusubiria verification.

  Sababu ya kuiwahisha humu JF kabla ya verification ni ili tuu wewe kama mwana JF to be the first to know!. Information is power!, if you are the first to know, then you'll have the powers to make good things happen or not to happen if they are bad things!.

  Asante.
  Paskali


  Update: 12/07/2015

  Leo hili limetimia ni kweli aliyepita ni Magufuli, nimezitafakari sababu nilizotajiwa ile siku napewa tetesi hii, na kuzipima na hiki kilichotokea, nimejikuta nimelazimika kutoziamini kuwa zile nilizosikia ndizo sababu zenyewe halisi.

  Kwa sisi waandishi tuna kanuni ya kuandika only the truth, yaani kuandika nothing but the truth, sasa ili uweze kuandika jambo lolote, ni lazima jambo hili uwe umelishuhudia na kujiridhisha kuwa ni la kweli, ndipo unaliandika.

  Ikitokea ukilisikia jambo la mashaka mashaka, unapaswa ulipime kwanza, ujiridhishe na ukweli wake, ukiisha ridhika ndipo uliamini na ndio uliandike.

  Kama ikitokea wewe kama mwandishi wa habari, ukasikia jambo lolote ambalo ni la mashaka huliamini, then hupaswi kuliandika, tena hata ikibidi usiliseme wala kuliandika ili lisijulikane.

  Hivyo hizo sababu nilizotajiwa siku hiyo napewa tetesi hii kuwa mgombea urais wa CCM atakuwa ni John Magufuli, and why he has to John Pombe Magufuli only and nobody else, kwa sasa mimi siziamini, na kwa vile siziamini, naomba nisizitaje wala nisiziseme kabisa humu.

  Hivyo naomba sasa tuchukulie bandiko hili kuwa ni mwana JF mmoja kwa jina la Paskali, nilijiandikia tuu kuwa mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015 atakuwa ni Dr. John Pombe Magufuli, na ikatokea tuu kuwa mgombea urais wa CCM kwa 2015 kweli akawa ni John Pombe Magufuli.

  Nawaombeni sana tuchukulie kupitishwa kwa jina la Dr. John Pombe Magufuli, kuwa mgombea urais wa CCM, has just happened tuu na has nothing to do bandiko hili wala na sababu nilizotajiwa, bali kuhesabike tuu kuwa kumetokea tuu naturally, by chance, bila any pre meditated moves, na hili bandiko lichukuliwe tuu kama just a coincidence, kuwa mwana jf mmoja nilisema mgombea wa CCM kwa mwaka 2015 atakuwa ni John Pombe Magufuli na kweli ikatokea tuu coincidentally, mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015 kweli akawa ni Dr. John Pombe Magufuli.

  Kwa mtakaonielewa asanteni kwa kunielewa, na kwa wale ambao ni wazito kuelewa mambo ya kufikirika tuu au ambao msio nielewa poleni na samahanini sana!.

  Hongera sana Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi, CCM.

  Paskali
   
 2. kajembejr

  kajembejr JF-Expert Member

  #281
  Mar 10, 2018
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 1,342
  Likes Received: 870
  Trophy Points: 280
  Pascal!!!! Heburudi utuambie zile sababu alizokuambia Yule mtu wako wa karibu pale mwaka 2014 kwamba 2015 mgombea wa ccm atajuwa huyu jamaa!!! Tafadhali tuwekee wazi zile sababu labda tutajua namna yakuishi ktk malengo yake... Mana hali siyo kabisa... Uzi wako unasisimua na laiti tungeusoma vizuri sote Leo tusingekuwa ktk maisha haya...
   
 3. Dr Garangi

  Dr Garangi Senior Member

  #282
  Mar 11, 2018
  Joined: Oct 3, 2017
  Messages: 103
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  Salama mkuu,watu waliona mbali sana
   
 4. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #283
  Mar 13, 2018
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 3,550
  Likes Received: 681
  Trophy Points: 280
  Pascal Haya mambo ukiota uwe unsitisha press conference
   
 5. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #284
  Mar 24, 2018
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,381
  Likes Received: 2,589
  Trophy Points: 280
  Shikamoo Pasikali
   
 6. a

  antimatter JF-Expert Member

  #285
  Mar 25, 2018
  Joined: Feb 26, 2017
  Messages: 699
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 60
  Duh.. Huo ni unabii uliotimia. Mkuu Pascal uliona mbali
   
 7. kasolobela

  kasolobela Senior Member

  #286
  Apr 7, 2018
  Joined: Mar 25, 2017
  Messages: 101
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Hii ni hatari Sana wametuingiza chaka
   
 8. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #287
  Apr 7, 2018
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,117
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Aliona mbali kivipi tena? Mayala kasema kwamba kuna mtu kamwambia, na yeye kaja hapa JF kuleta hiyo habari. Wewe unasema "Mkuu paschal uliona mbali", mbali ipi? Jifunze ustaarabu wa kusoma bandiko kwa makini. Acha kukurukakara. Kumradhi kama nimekuudhi.
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #288
  Apr 12, 2018
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 9,285
  Likes Received: 2,988
  Trophy Points: 280
  Paschal ulikuwa sahihi kumtilia shaka hasa utimamu wake , ni bahati mbaya kuwa walimuandaa lakini hawakumpika vya kutosha, kama nilivyosema awali JPM needed few fine tuning to become the best ..ambazo huwezi kumfanyia akiwa Rais , ni maandalizi ambayo angetakiwa afanye kabla ...
  Lakini pia JPM binafsi amekuwa akijiandaa kimya kimya kwa kujiposition na kuwa mmoja wa wasifiaji wakubwa wa JK ....ni bahati mbaya au nzuri kuwa kambi ya Membe na Lowassa walim underestimate sana !!
   
 10. Ngadu01

  Ngadu01 JF-Expert Member

  #289
  Apr 12, 2018
  Joined: May 4, 2016
  Messages: 290
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 80
  Kwani kakwambia yeye anahitaji teuzi uchwara kama Musiba au Harrison Kapiga acha uzwazwa
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #290
  Apr 12, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,668
  Likes Received: 23,949
  Trophy Points: 280
  Mkuu Phile, he is changing for the better, anabadilika. Kwani umeushazisikia tena zile ziara za kushtukiza?, umaishasikia tena tumbua tumbua za papara?, hujanote hata kupayuka kumepungua?.
  Tusilalamike Tuu, Kulaumu na Kulaani Kila Kitu, Kwenye Mazuri Tupongeze, Rais Magufuli is Changing For The Better!.
  Amini usiamini, yote anayoyafanya japo some are wrong na mengine ni udikiteta per se, lakini anayafanya kwa nia njema na dhamira safi.
  Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
  Kwa vile Tanzania, tulifikishwa mahali nchi ikawa inamhitaji mtu wa aina hii, then akiendelea kubadilika, changing for the better, he has the chances kuja kuwa the best president this country has ever had since Mwalimu Nyerere!.

  Ndio maana sisi wengine tunashauri
  Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?.

  P.
   
 12. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #291
  Apr 12, 2018
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 3,550
  Likes Received: 681
  Trophy Points: 280
  Mbona unamtetea tetea like kutaga
   
 13. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #292
  Apr 13, 2018
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 9,285
  Likes Received: 2,988
  Trophy Points: 280
  I agree with you , and having attended meetings anazokuwapo sometimes naona change of tone ...., ila ninachokiona ana washauri wazuri ila kuna wachache kwenye "kitchen cabinet " yake ndio wanaharibu haiba yake ..., nadhani unafahamu nguvu ya watu wa jikoni , mnaweza kwenda na ushauri mzuri tu , mkiondoka wao ndio they speak over it, watu aina ya Makonda wanamuharibia sana rais image yake , lakini pia wako wakuu wa mikoa kama Mnyeti ni tatizo kubwa ......angalau naona Gambo siku hizi anajaribu kukomaaa
  Mtu kama PolePole kaishiwa kabisa mbinu za uenezi na kufanya uenezi wa ccm uwe kwenye mfumo la 'manunuzi" ,
  Pia anatakiwa kupunguza kuongea hadharani mara kwa mara .....sio lazima kila event yake ifanywe live coverage ...watu wakimsikia mtu sana wanamzoea na kumuona wa Kawaida ........rais sio mtu wa kuongea kila siku ,mara nyingine atumie wasemaje ili siku akinyanyuka kuwe na uzito
   
 14. Nyanya mbichi

  Nyanya mbichi JF-Expert Member

  #293
  May 7, 2018
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 3,587
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  waona mbali
   
 15. britanicca

  britanicca JF-Expert Member

  #294
  May 9, 2018
  Joined: May 20, 2015
  Messages: 4,698
  Likes Received: 5,935
  Trophy Points: 280
  Kwelli
   
 16. britanicca

  britanicca JF-Expert Member

  #295
  May 9, 2018
  Joined: May 20, 2015
  Messages: 4,698
  Likes Received: 5,935
  Trophy Points: 280
  Sasa je
   
 17. britanicca

  britanicca JF-Expert Member

  #296
  May 9, 2018
  Joined: May 20, 2015
  Messages: 4,698
  Likes Received: 5,935
  Trophy Points: 280
  Kumbe
   
 18. britanicca

  britanicca JF-Expert Member

  #297
  May 9, 2018
  Joined: May 20, 2015
  Messages: 4,698
  Likes Received: 5,935
  Trophy Points: 280
   
 19. b

  bato JF-Expert Member

  #298
  May 9, 2018
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 2,552
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
 20. M

  MTK JF-Expert Member

  #299
  May 10, 2018
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 7,288
  Likes Received: 3,124
  Trophy Points: 280
  Anatunyolosa!
   
 21. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #300
  Jun 7, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,668
  Likes Received: 23,949
  Trophy Points: 280
  Mkuu Bato, mimi nipo sana tuu, ila pia its human nature, we human beings are not static, we are dynamic, and hence we change with time, tunaishi kwenye ulimwengu unaobadilika kwa kufuata the law of the jungle, "struggle for existence, survival is for the fittest", ili uweze ku survive ni lazima uwe fiti, na huwezi kuwa fiti kama huwezi kubadilika!. Saa hizi time zimebadilika, watu wamebadilika na Tanzania imebadilika, hivyo ili tuweze ku survive, na sisi lazima tubadilike, we have to change with time, hivyo nami nabadilika na nimebadilika.
  P
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...