Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli | Page 12 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Aug 15, 2014.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi tuliyepotezana naye Kipindi kirefu, ambaye ni mtu wa sehemu na wa kuaminika sana ambaye yuko attached CCM kama kada tuu wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha, zimenisikitisha, kunihuzunisha, kuniogopesha, kunisononesha na kuninyongonyeza!, kuwa eti imeishaamuliwa (sitaji imeamuliwa na nani), kuwa mgombea wa urais wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli!.

  Kilichonistua, kunitisha, kunihuzunisha, kunisikitisha, kunisononesha, kunigopesha na kuninyongoneza ni the reasons behind alizonitajia za why ni Magufuli, ambazo ndizo zimepelekea the inner core ya CCM kuamua mgombea wake wa urais wa 2015 ni lazima awe John Pombe Magufuli tuu, and no one else!.

  Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi kweli ni justifiable na nyingine sio tuu ni unjustifiable!, bali hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!. Naomba kwa sasa nisizitaje kwanza hizo sababu, kwa sababu habari zenyewe nimezisikia from a single source, nahitaji kwanza kufanya verification kwa ku double check, na ku cross check ikiwemo kupata a collaborative verification na attribution ya third parties ili nijiridhishe kuwa hii ni habari za kweli na kuthibitisha kuwa kumbe hivyo ndivyo the inner core ya CCM inavyoweza kufikia maamuzi ya mgombea wake based on sababu nilizo tajiwa!, then nitaziweka hadharani hizo sababu za kwa nini CCM imeamua mgombea wake wa 2015 lazima awe ni Magufuli tuu!, na kiukweli mkizisikia hata nyinyi mtashangaa!.

  Kwa kawaida sisi waandishi, ukipata taarifa kama hii, huwa inaitwa "a news tip", haukimbilii kuiandika mbio mbio mpaka kwanza uifanyie verification kwa kui double check na kui cross check ili kujiridhisha kwa kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe, baada ya kuthibitisha na kujiridhisha ndipo unaiandika.

  Lakini kwa vile sasa tunaishi kwenye "the world of information age", nimeamua kuileta hii "news tip" humu jf, hivi hivi ikiwa kwenye hatua ya "tip" kabla hata ya verification, ili wewe kama mwana JF, uipate ile JF advantage ya "be the first to know!", hivyo nawaombeni tuu sasa wana jf mkae mkijua kuwa "Mgombea wa urais wa CCM kwa mwaka 2015 ni John Pombe Magufuli!".

  Hili la kuamua ni Magufuli, limenistua kidogo kwa sababu kwa sisi tuliomfuatilia Magufuli utendaji kazi wake kwa kauli na matendo, huyu mtu ameonyesha sio mzima sana kichwani!, anafanya baadhi ya maamuzi na jazba, papara na kukurupuka mtindo wa liwalo liwe, mwisho wa siku yanakuja kutu cost, hivyo akipita na kuwa rais wa nchi, you can just imagine, atafanya maamuzi mangapi ambayo yatatucost kama taifa, ila pia ana chance ya kuja kuwa the worst dictator this nation has ever had!.

  Nikiisha "confirm" neno "tetesi" litaondolewa na kuwa replaced na neno "confirmed!", na nitaziweka hizo sababu ili sasa ndio zijadiliwe!, na nawahakikishia wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, mkizisikia hizo sababu za huyo kada wa CCM alizonipa kwa nini ni Magufuli!, na nyinyi pia zitawashitua, zitawatisha, zitawaogopesha, kuwahuzunisha, kuwasikitisha, kuwasononesha na kuwanyongonyeza!.

  Naomba nisiwatajie jina la huyo source wangu chini ya kinga ya kihabari kwa ma source inayoitwa "The Confidentiality of the source", na hapa wakati naileta taarifa hii humu jf, kwa vile zoezi la kumteua mgombea wa CCM bado liko mbali hadi mwaka ujao, unaweza kukuta hata Magufuli mwenyewe bado hajui kuwa ni yeye ndie atakuwa mgombea wa CCM, kwa sababu walio amua kuwa ni Magufuli sio kikao chochote rasmi na halali ndani ya CCM bali ni "The Inner Circle" hivyo hii ni tip from the deep inside ya "the inner circle", na bahati mbaya sana, Magufuli mwenyewe hayuko kwenye hiyo "the inner circle!".

  NB. Sio kila thread ni lazima ichangiwe, saa nyingine itoshe kujisomea tuu na kujipitia bila kuchangia chochote!. Hii ni just a news tip, kwa vile nimewaahidi naifanyia verification kuithibitisha, nawaombeni msiniulize swali lolote at this stage, kwa sababu sitajibu chochote!, and if possible nawashauri na nyingi msome FYE only na sio lazime mchangie kwa sasa na badala yake mvute subira kusubiria verification.

  Sababu ya kuiwahisha humu JF kabla ya verification ni ili tuu wewe kama mwana JF to be the first to know!. Information is power!, if you are the first to know, then you'll have the powers to make good things happen or not to happen if they are bad things!.

  Asante.
  Paskali


  Update: 12/07/2015

  Leo hili limetimia ni kweli aliyepita ni Magufuli, nimezitafakari sababu nilizotajiwa ile siku napewa tetesi hii, na kuzipima na hiki kilichotokea, nimejikuta nimelazimika kutoziamini kuwa zile nilizosikia ndizo sababu zenyewe halisi.

  Kwa sisi waandishi tuna kanuni, ukilisikia jambo, lipime uliamini ndipo uliandike, kama huliamini, then usiliseme wala kuliandika, hivyo hizo sababu nilizopewa siku hiyo, on why ni Magufuli, mimi siziamini, naomba nisiziseme kabisa, hivyo naomba tuchukulie bandiko hili nilijiandikia tuu kuwa atakuwa Magufuli, na kupitishwa kwa jina la John Pombe Magufuli, has nothing to do na sababu nilizotajiwa, bali kuhesabike kumetokea tuu naturally, by chance, bila any pre meditated moves, na hili bandiko lichukuliwe tuu kama just a coincidence, kuwa nilisema mgombea wa CCM atakuwa ni Magufuli na kweli ikatokea tuu coincidentally, mgombea wa CCM akawa kweli ni Magufuli.

  Kwa mtakaonielewa asanteni kwa kunielewa, na kwa msio nielewa poleni na samahanini sana!.

  Hongera sana John Pombe Joseph Magufuli kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM.

  Paskali
   
 2. m

  mike2k JF-Expert Member

  #221
  Jan 3, 2017
  Joined: May 12, 2016
  Messages: 413
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 80
  Ya bukoba yamedhiirisha hvyO
   
 3. Bedullah

  Bedullah JF-Expert Member

  #222
  Jan 4, 2017
  Joined: Dec 9, 2012
  Messages: 206
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Vigezo hivi ndivyo vilipaswa kuzingatiwa na wana Usalama wa Taifa katika kumshauri Rais aliyekuwa madarakani wakati ule juu ya harakati za kumtafuta mrithi wa JK. Kwa bahati mbaya nchi haina mfumo wa serious vetting haswa kwa wagombea toka CCM! Kuna siku nchi itatawaliwa na mzungu wa unga au chizi atakayeiangamiza nchi!
   
 4. Iceman 3D

  Iceman 3D JF-Expert Member

  #223
  Jan 4, 2017
  Joined: Sep 3, 2016
  Messages: 16,581
  Likes Received: 47,728
  Trophy Points: 280
  Nakuheshimu sana kwa kuona mbali
   
 5. Msafirishaji

  Msafirishaji JF-Expert Member

  #224
  Jan 4, 2017
  Joined: May 28, 2016
  Messages: 1,205
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  MUNGU akupe maisha marefu mkuu moja ya watu wachache wanaoweza kuona mbali ishi maisha marefu bona ishi maisha marefu jf
   
 6. Lupyeee

  Lupyeee JF-Expert Member

  #225
  Jan 4, 2017
  Joined: Jun 28, 2016
  Messages: 2,690
  Likes Received: 2,812
  Trophy Points: 280
  Chadema Lazima mseme haya, maana mafisadi mnanyooshwa kweli kweli.

  Magufuli kaza, kuna watu walijigeuza Mungu mtu nchi hii
   
 7. Super Sub Steve

  Super Sub Steve JF-Expert Member

  #226
  Jan 4, 2017
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 10,346
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Uliandika 2014
   
 8. Super Sub Steve

  Super Sub Steve JF-Expert Member

  #227
  Jan 4, 2017
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 10,346
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Aisee
   
 9. Super Sub Steve

  Super Sub Steve JF-Expert Member

  #228
  Jan 4, 2017
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 10,346
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  Aiseeee
   
 10. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #229
  Jan 4, 2017
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 11,703
  Likes Received: 3,397
  Trophy Points: 280
  Asante watanzania kwa kutuletea Rais Magufuli.
   
 11. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #230
  Jan 4, 2017
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 33,791
  Likes Received: 41,262
  Trophy Points: 280
  mkuu hakika umenena vema.
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #231
  Jan 4, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
   
 13. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #232
  Jan 5, 2017
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 18,019
  Likes Received: 19,978
  Trophy Points: 280
  aiseeee
   
 14. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #233
  Jan 5, 2017
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 18,019
  Likes Received: 19,978
  Trophy Points: 280
  kumbe waliunganisha ID zako!
   
 15. P

  Pohamba JF-Expert Member

  #234
  Jan 5, 2017
  Joined: Jun 2, 2015
  Messages: 16,247
  Likes Received: 25,106
  Trophy Points: 280
  Ulianza Uchochezi tangu August 15, 2015
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #235
  Jan 5, 2017
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 13,446
  Likes Received: 6,479
  Trophy Points: 280
  ..hiyo ni post ya 2014.

  ..lakini kashfa ya kuuza nyumba za serikali ndiyo ilinifanya nimuangalie kwa umakini zaidi.
   
 17. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #236
  Jan 13, 2017
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,524
  Likes Received: 523
  Trophy Points: 280
  Rais wa Kikwete huyu
  FEB 04, 2015by RAIA MWEMAin UCHAGUZI 2015
  WANACHAMA watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametajwa kuwa nyuma ya kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba kuna watu wana uwezo wa kurithi nafasi yake lakini hawajajitokeza bado, Raia Mwema limeambiwa.

  Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alizungumza hadharani mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Songea, Ruvuma kwamba chama hicho bado hakijapata mgombea na kwamba wanachama wa chama hicho wana wajibu wa kuwaibua ili chama kipate mgombea anayefaa.

  “Wapo wengine ni material ya kuwa rais. Hawajijui na wanahitaji kukumbushwa. Kuwakumbusha si dhambi. Tusifanye ajizi kwa jambo hili ambalo ni kubwa kwa maslahi ya nchi yetu,” alisema Kikwete wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 38 ya CCM.

  Katika mazungumzo ambayo gazeti hili limefanya na watu wa karibu na Kikwete na makada wa CCM, majina matatu yametajwa kama wanachama ambao japo hawatajwi kwenye vyombo vya habari na duru za kisiasa, wanachama wa chama hicho wanaona kwamba ni watu wanaoweza kuvaa viatu hivyo.

  Wanachama hao watatu wanatajwa kuwa na sifa za kutokuwa na kashfa ya ufisadi, kutokuwa na makundi, wanataaluma wasio na shaka na watu ambao tayari wameonyesha uwezo mkubwa wa uongozi.

  Raia Mwema limetajiwa majina matatu ambayo yanaelezwa kuwa kifuani kwa Kikwete wakati akitoa kauli yake hiyo.

  Brigedia Jenerali Jaji Augustino Ramadhani

  Tangu Desemba mwaka 2013, Augustino Ramadhani amekuwa akifanya kazi za kichungaji katika Kanisa la Anglikana, Zanzibar, mara baada ya kustaafu nafasi ya Jaji Mkuu wa Tanzania.
  Jaji Ramadhani ana sifa kuu tatu za kipekee. Mosi, ni Mzanzibari, pili ni Mkristo na tatu ni mtu ambaye hajawahi kukutwa na doa lolote katika utendaji wake.

  Kwenye hotuba yake hiyo ya Uwanja wa MajiMaji mjini Songea, Kikwete alisema; “Mgombea tunayemtaka ni yule ambaye wananchi wakisikia jina lake linatangazwa Watanzania waseme hapo barabara…. Isiwe wakiulizwa hapo vipi wanasema Aaah, hapo si sawa”.

  Katika vuguvugu la sasa la Muungano ambapo wapo Wazanzibari wanaoamini kuwa mara hii ni zamu yao kutoa Rais wa Muungano, Jaji Ramadhani anajitokeza kipekee kwa sababu pia ni Mkristo.

  Ingawa Tanzania inafahamika kama nchi ambayo haiamini katika kupokezana madaraka kidini, utaratibu unaonyesha kwamba kumekuwa na kupokezana kwa madaraka baina ya waumini wa dini hizi mbili.

  Kikwete ni Mwislamu na hivyo inatarajiwa kwamba mrithi wake atakuwa Mkristo. Mwanasheria huyu ni mmojawapo wa Watanzania wachache ambao wana bahati ya kuwa Wazanzibari na pia Wakristo.

  “Faida nyingine ambayo Augustino anayo ni ile kwamba yeye ni Muanglikana. Kulikuwa na kilio hapa kutoka kwa baadhi ya Wakristo kwamba marais Wakristo waliopita walikuwa Wakatoliki na hivyo hii ni zamu ya mtu asiye Mkatoliki.

  “Jaji Augustino Ramadhani ni mtu mwenye sifa za kipekee. Tatizo ambalo tunaliona ni kwamba itabidi ashawishiwe sana ili akubali kuingia kwenye kinyang’anyiro.

  “Yeye alishaamua kumtumikia Mungu baada ya kustaafu. Hana mawazo yoyote ya kutumikia tena wananchi kisiasa. Nadhani Kikwete aliposema wengine wanahitaji kushawishiwa, alimaanisha bwana huyu,” alisema mmoja wa wana CCM wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa jina lake.

  “Aaah, sasa si unajua namimi nagombea? Unataka uninukuu kabisa kwenye hilo.? This is my honest opinion (hapa nimezungumza ukweli mtupu). Sijui kama Jaji atakubali. Nafasi yangu iko palepale. Sasa wafuasi wangu watapata picha gani wakisikia nazungumzia uwezo wa mtu mwingine?” alihoji.

  Jaji Ramadhani ni miongoni mwa Watanzania wenye historia ya kipekee. Akiwa Jaji Mkuu, hakuweza kuficha mapenzi yake kwa mchezo wa mpira wa kikapu na alikuwa mlezi wa chama cha mchezo huo ngazi ya Taifa.

  Ni wakati huo pia ndipo alipoanza kufahamika kama mpiga piano wa kwaya ya Kanisa la Mtakatifu Alban lililopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

  Jaji Ramadhani pia alikuwa askari aliyestaafu katika ngazi ya Brigedia Jenerali na pamoja na kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, amehukumu pia katika Mahakama ya Kijeshi (Court Marshall).

  Jambo ambalo watu wengi hawalifahamu ni kwamba babu wa Jaji Ramadhani, Mzee Augustino Ramadhani, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa Chama cha African Association (AA) ambacho baadaye kilikuja kuwa sehemu ya muungano uliounda Chama cha ASP, ambacho sasa ni CCM.

  Swali pekee ambalo pengine limebaki moyoni kwa Kikwete ni endapo Mchungaji Augustino Ramadhani ataacha kazi ya kuchunga ‘kondoo wa Bwana’ na kurejea kuwaongoza Watanzania kwenda katika nchi ya ahadi?

  Dk. Augustine Mahiga

  Jina la Mahiga si maarufu sana katika duru za kisiasa hapa nchini lakini pengine ndiye mwanadiplomasia wa Kitanzania anayeheshimika kuliko wote.

  Mwaka juzi alimaliza jukumu lake la kuwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban ki Moon, nchini Somalia ambapo alisifiwa kwa kufanikisha kuwepo kwa serikali inayotambuliwa na Jumuiya ya Kimataifa pamoja na tishio la magaidi la Al Shabaab.

  Mwanzoni mwa miaka ya 1990, Mahiga alinusurika kuuawa na Majeshi ya Charles Taylor, nchini Liberia wakati wa Vita ya wenyewe kwa wenyewe wakati huo yeye akifanya kazi ya kuongoza shughuli za Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la UN (UNHCR).

  Mahiga amepata pia kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika kipindi cha kati ya mwaka 2003 hadi 2010, ambapo Raia Mwema limeambiwa alirejesha heshima ya Taifa hili kiasi cha kufikia kuwa mojawapo ya zilizounda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

  “Katika korido za UN, ni wana diplomasia wachache, tena labda wapya ambao hawamfahamu Mahiga ni nani. Amekaa pale muda mrefu na alikuwa mahiri sana. Kikwete anasafiri sana na nadhani ujumbe anaoupata nje ya nchi ni kwamba Mahiga anafaa kuchukua nafasi yake," kilisema chanzo cha gazeti hili kutoka Ikulu.

  Katika kipindi cha kati ya mwaka 1980 hadi mwaka 1983, Mahiga alikuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, nafasi ambayo ilimpa fursa ya kuifahamu Tanzania nje na ndani.

  Kama ilivyo kwa Jaji Ramadhani, Mahiga naye haonyeshi hamu ya kutaka kuwa Rais. Anatumia muda wake mwingi kutoa mihadhara katika vyuo vikuu mbalimbali duniani ambako mihadhara yake mingi huhusu masuala ya Utawala Bora, Utatuzi wa Migogoro, Ulinzi na Usalama na Uhusiano wa Kimataifa.

  Dk. John Pombe Magufuli

  Katika majina haya matatu, Magufuli ndiye pekee ambaye anafanya kazi za kisiasa na pengine umri wake ni mdogo kulinganisha na wenzake hawa wawili.

  Ingawa jina lake limekuwa likitajwa katika duru za kisiasa, Magufuli mwenyewe hajaonyesha dalili za kutaka nafasi hiyo na amewahi kukana hadharani wakati alipohusishwa na mojawapo ya kambi zinazotajwa kutaka kuwania urais kupitia CCM.

  Mmoja wa wasaidizi wa Kikwete aliliambia gazeti hili juzi Jumatatu kwamba kuna mambo makubwa matatu ambayo yamewafanya baadhi yao kudhani Kikwete alikuwa akimzungumzia Magufuli.

  Mosi, ni ukweli kwamba katika ziara ambazo Kikwete amekuwa akifanya ndani ya nchi, Magufuli amekuwa akionekana kama waziri anayeonekana kuheshimiwa na Watanzania.

  Mfano ambao Kikwete amewahi kuusema kwetu unahusu mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika Mwanza mwaka jana. Watu wa kule walikuwa wakizomea na kuonyesha alama za Chadema.

  “Lakini alipopanda jukwaani Magufuli mkutano wote ulitulia. Mpaka Kikwete alipopanda jukwaani, mkutano ulikuwa umetulia. Nadhani Kikwete ameona kwamba labda huyu ndiye mwana CCM ambaye Watanzania wanamuamini,” alisema.

  Wakati aliporejea kutoka kwenye matibabu nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana, Kikwete alitamka hadharani kwamba alitaka kutangaza mapema kuhusu ugonjwa wa kansa uliokuwa ukimsumbua, lakini ni Magufuli aliyemkataza kufanya hivyo wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri.

  Mwaka juzi, Magufuli pia aliwashangaza watu wakati alipopishana hadharani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu suala la magari ya mizigo kupita katika barabara yakiwa yamezidi mizigo.

  “Ile ilikuwa ni ishara kwamba Magufuli alikuwa akiamini nguvu iliyo juu ya Pinda. Katika hali ya kawaida, si rahisi kwa waziri wa kawaida kutofautiana na Waziri Mkuu hadharani,” kilisema chanzo kingine cha gazeti hili.

  Msaidizi huyo wa Kikwete alilieleza pia Raia Mwema kwamba katika mojawapo ya misiba ya karibuni zaidi iliyoikumba familia ya Rais, Magufuli alikuwa waziri pekee ambaye alilala msibani kijijini Msata.


  “Kama walivyo wenzake, Magufuli anaonekana ni mchapa kazi na mtu ambaye hahusishwi na masuala ya ufisadi ingawa kuna wanaonong’ona kuhusu suala la uuzaji wa nyumba za serikali,” Raia Mwema liliambiwa.

  FacebookTwitterGoogle+

  Rais wa Kikwete huyu – Raia Mwema


  Kumbe dalili zilinza kuonekana siku nyingi wengine walikua wasindikizaji.
   
 18. Mr.Junior

  Mr.Junior JF-Expert Member

  #237
  Jan 16, 2017
  Joined: Sep 8, 2013
  Messages: 8,817
  Likes Received: 4,413
  Trophy Points: 280
  ...
   
 19. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #238
  Jan 18, 2017
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,420
  Likes Received: 1,736
  Trophy Points: 280
  ....Kweli...
   
 20. Raynavero

  Raynavero JF-Expert Member

  #239
  Jan 18, 2017
  Joined: Apr 29, 2014
  Messages: 26,695
  Likes Received: 25,564
  Trophy Points: 280
  watu mna maonooo...
   
 21. pakaywatek

  pakaywatek JF-Expert Member

  #240
  Jan 18, 2017
  Joined: Dec 28, 2014
  Messages: 3,265
  Likes Received: 2,538
  Trophy Points: 280
  Maneno huwa yanaumba.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...