Mgombea Urais matumizi yaongeza hadi Bil 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgombea Urais matumizi yaongeza hadi Bil 5

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Mar 23, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  BAADA ya Rais Jakaya Kikwete kusaini Sheria ya Gharama za Uchaguzi wiki iliyopita, Serikali imependekeza matumizi kwa mgombea urais yasizidi Sh bilioni moja kuanzia kwenye mchakato wa kuteuliwa na chama hadi kampeni.

  Kwa upande wa wagombea ubunge, gharama hizo zinategemea eneo la jimbo, idadi ya watu na hali ya miundombinu. Mgombea ubunge ambaye jimbo lake liko makao makuu ya mkoa ambalo watu wake ni zaidi ya 300,000 kiasi cha fedha anachotakiwa kutumia ni Sh milioni 40.


  Jana wadau mbalimbali zikiwamo asasi za kiraia na vyama vya siasa, walijadili rasimu hiyo ya kanuni na taratibu zitakazotumika wakati wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, CCM haikuwakilishwa kwenye majadiliano hayo ambayo yalifanyika kwenye ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.


  Kwa mgombea ambaye jimbo lake liko nje ya makao makuu ya mkoa na idadi ya watu haizidi 100,000 kiasi cha fedha anachotakiwa kutumia ni Sh milioni 20 wakati kwa jimbo lenye watu ambao hawazidi 150,000 kiasi cha fedha anachotakiwa kutumia ni Sh milioni 30.


  Mgombea ambaye jimbo lake liko nje ya makao makuu ya mkoa na wapiga kura wake ni kati ya 150,000 na 300,000, atatumia fedha isiyozidi Sh milioni 35.


  Lakini kwa mgombea ubunge katika majimbo yaliyoko kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza bila kujadili idadi ya watu, atalazimika kutumia fedha zisizozidi Sh milioni 20.


  Katika mchanganuo huo pia wagombea ubunge wa Zanzibar ambao majimbo yako katika makao makuu ya mikoa na wapiga kura wanazidi 10,000 watatakiwa kutumia Sh milioni 10.

  Wagombea ubunge wa Zanzibar ambao majimbo yao yako nje ya makao makuu ya mikoa na yana watu ambao hawazidi 10,000 watatumia si zaidi ya Sh milioni saba.

  Kwa upande wa viti maalumu Tanzania Bara ambao wapiga kura ni zaidi ya 10,000 kiasi cha fedha kinachopendekezwa kutumiwa ni Sh milioni tatu.


  Katika mpango huo wagombea udiwani katika maeneo ya mjini kiasi wanachotakiwa kutumia si zaidi ya Sh milioni saba na wale ambao kata zao ziko vijijini, matumizi yao yatatakiwa yasivuke Sh milioni 10. Wakati wagombea udiwani wa viti maalumu matumizi yao hayatakiwi kuzidi Sh milioni moja.


  Kwenye rasimu hiyo ya kanuni katika kipengele kinachohusu timu ya kampeni kwa ajili ya gharama za uchaguzi, mgombea urais wajumbe hawatazidi 50, mgombea ubunge wajumbe hawatazidi 20 wakati mgombea udiwani wajumbe hawatazidi 10.


  Wajumbe hao wa kampeni watatakiwa wathibitishwe baada ya mgombea kuwasilisha maombi kwenye Mamlaka iliyoamuliwa na sheria hiyo siku 10 kabla ya uteuzi au siku 10 baada ya uteuzi.


  Mgombea ambaye atabadili timu yake ya kampeni, atalazimika kutuma maombi kwenye Mamlaka inayohusika kwa ajili ya mabadiliko hayo. Katika rasimu hiyo mamlaka inayohusika inaweza kukataa kufanya mabadiliko kama itaridhika kuwa mjumbe huyo hawezi kuathiri kampeni za uchaguzi.


  Katika rasimu hiyo, licha ya kupendekezwa kuwa mgombea aliyepata kura nyingi kwenye chama ndiye ateuliwe na chama chake kugombea urais, ubunge na udiwani, lakini wadau walikikataa kifungu hicho.


  Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, alisema kipengele hicho hakifai kwani kuna baadhi ya wagombea wanaweza kutumia fedha kurubuni wapiga kura; hivyo akapendekeza kifungu hicho kiongezwe maneno kuwa “itakapothibitika kuwa aliyeongoza alitumia rushwa basi chama kitumie taratibu zake kumpata mgombea”.


  Mwenyekiti wa Chausta, James Mapalala, alisema eneo hilo ndilo msingi wa demokrasia na kama kanuni hazitasema wazi kuwa mtoa rushwa aondolewe, anaweza kuingia mtu madarakani akaharibu Taifa kwa rushwa.


  Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, alisema lazima kifungu hicho kirekebishwe, ili kuvipa vyama fursa ya kupokea malalamiko ya walioshindwa na ikithibitika kuwa aliyeshinda alitumia rushwa, aondolewe.


  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema utaratibu uliopo ndani ya vyama utumike. Alisema iwapo kifungu hicho kitaachwa kilivyo, CCM itasaidia wagombea wa upinzani ambao ni dhaifu, ili kushinda kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya vyama.


  “Tukikiacha hivi hiki kifungu vyama vingine vinaweza kupata wagombea dhaifu ambao hawauziki … na hii ndiyo kazi ya Kamati Kuu na Baraza Kuu kuchambua ni mgombea gani anakubalika anayeweza kukipa ushindi.


  “Ili kutopata mgombea dhaifu, tupeni nafasi ya kurekebisha hili, wewe Msajili (wa Vyama vya Siasa) na meza yako hiyo hamna vyama, sisi ndio tunajua mambo yaliyoko ndani ya vyama vyetu, tunaomba mturudishie taratibu za kupata wagombea,” alisema Profesa Lipumba.


  Msajili wa Vyama John Tendwa alikubaliana na mapendekezo ya wadau hao “hizi ni kanuni zenu na wala si za CCM. Kwa mapendekezo yenu na sisi tunakubaliana nayo,” alisema Tendwa ambaye alifuatana na Mwandishi wa Sheria, Casmir Kyuki.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kiini macho.
  Hivi sasa tunaongea UWAMA inamwaga fedha mikoani, zote zikilenga kuwashika wanawake wasimtupe mkuu!..Je hizi nazo zimo kwenye hiyo 1b?
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi hilo semi traila la Komba analozunguka nalo ni sh ngapi eti au hilo nalo halimo kwenye bil 1.
   
 4. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna baadhi ya vipengele havitekelezeki kama wajumbe wa kampeni ya urais wasizidi 50 kwaya ya TOT ina wanakwaya zaidi ya 40 ina maana itatolewa katika kampeni au hii ni kiini macho tu.
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nafikiri maana ya hicho kipengere ni kwamba mgombea chini ya hiyo kanuni ya mpaka bilioni moja anaweza kuhudumia mpaka watu 50 ambao watakuwa wanaunda team ya kampeni yake.

  Kama TOT watahudumiwa na mgombea basi inatakiwa wawemo kwenye hiyo namba lakini kama watajitolea wenyewe au kuwa sponsored nje ya utaratibu nafikiri itakuwa ruhusa.

  Utekelezaji wa hiyo kanuni nafikiri utakuwa mgumu sana. Huenda ingelikuwa busara kama wangeweka kiwango cha fedha tu na kuacha hilo la namba ya watu kwenye kampeni.

  Tatizo kubwa kwa TZ sio sheria bali utekelezaji wa hizo sheria ndio unakuwa mbovu. Sheria ambayo haitekelezwi ni hatari kuliko kutokuwepo kwa sheria hiyo.
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hiyo kitu safi sana, na inapendeza kweli kweli
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama hii ni sawa; kwa sababu sheria inataka gharama kuingiwa na vyama vya siasa siyo makundi nje ya vyama vya siasa; kwa hiyo i suppose gharama ya TOT itaingiwa na CCM.

  Ndiyo maana tumesema ni sheria mbaya.. na hapa bado haijafika kwenye utekelezaji.

  Tatizo ni sheria; ni sheria zenyewe zinazofanya utekelezaji wake kuwa mbaya au matokeo yake yawe yasiyotarajiwa. Fikiria sheria ya Madini, Maadili ya Umma na TISS... utekelezaji wake umekuwa mbaya kwa sababu ni sheria mbaya. So is this one.
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nani atamjulisha Msajili wa vyama kama TOT haihudumiwi na mgombea au Chama kwa sababu tunajua TOT hata mishahara wanalipwa na chama na kama TOT itahudumiwa na sponsor nje ya chama huoni kama tutakuwa tunarudi kule kule ambako tunataka kutoka, naungana na wewe unaposema utekelezaji wa sheria hii utakuwa mgumu sana.
   
 9. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hm!! Bilioni moja.

  Hivi huwa nilazima kutengeneza zile khanga, T-shirt na kofia?

  Hebu fikiria ni mambo mangapi ya maendeleo yanaweza kufanyika kwa hiyo bilioni?
   
 10. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  viongozi mbumbu hawawezi kuficha umbumbu wao ndio maana wanajitokeza na sheria za ajabu na kuacha mambo ya maana.

  kitachofanyika hapa ni kuwanyanyasa wa[pinzani tu.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Injia.. hivi kweli unafikiri gharama ya bilioni moja ni nyingi!? Yaani, tumchague Rais kwa uwekezaji usiozidi nyumba moja ya Gavana? are you kidding me.. Badala ya kuweka ushindani uwe huru, wa haki na wa wa wazi sasa wameamua kuuzima kabisa. Sasa mkishatumia bilioni moja na zimebaki wiki tatu za kampeni mnafanya nini?
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu, unashangaa hiyo, wakati ndo wamepunguza kishenzi?
  Nadhani kabla ya hapo ilikuwa ina'range kwenye 5 bn au zaidi!
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi, kwenye demokrasia unaweza vipi kuwazuia watu kutumia haki yao ya kujieleza kwa njia halali kwa kuwawekea kizuizi cha matumizi ya fedha? Je, Rais Kikwete akiwa ni incumbent akitaka kuzungumzia kwenye radio na Tv mara kwa mara kwa kisingizio cha shughuli za serikali je wagombea wengine wa upinzani watapewa nafasi ya kujibu? au ndiyo itakuwa 'yeye ni rais"?
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Well.....this is still advantage CCM. How many opposition parties can spend Tsh1billion per election per candidate(correct me if I'm wrong)? I think this is more of a limit on CCM presidential candidates and not presidential candidates as a whole.

  By the way.....just thinking out loud.....mheshimiwa anaogopa kuna makundi yanayo weza yakawa na funds zaidi ya za ***** lake? Maana hizi sheria za miezi michache kabla ya uchaguzi zina raise questions nyingi.
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Jibu la swali lake ndicho kinachotakiwa na CCM 'mnazimika completely' mkiongeza pesa mtakuwa mmevunja sheria hata mgombea wenu akishinda atavuliwa mahakamani, mimi nabashiri mwaka huu kutakuwa na kesi nyingi sana za kupinga matokeo maana kuna loop holes nyingi zinazoonekana kwa macho bila hata kuvaa miwani
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sasa pia mkumbuke kuwa sheria hii inabana zaidi baadaye (siku tisini) lakini kabla ya hapo mtashuhudia CCM ikifanya fundraising kubwa n.k Kila ninavyoangalia ninachoona ni kuwa sheria hii itaiumiza CCM zaidi na hasa wagombea wapya ambao majina yao hayajulikani sana.
   
 17. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Msaada kwenye tuta.........naomba gharama za.........
  TV air time say 2hrs Tsh.........
  Semi trailer moja Tsh..........
  Gari 5 ndogo za kampeni Tsh.............
  Safari(mafuta nk)........
  Malazi.........
  Chakula+vinywaji...........
  Banners+flyers...........
  kukodi vyombo(muziki)
  Posho..............
  + +.........
  Jamani hivi bilioni bado ipo nafikiri kuna wabunge wengine watakampeni kwa baiskeli kama sio punda maana mil.40 ni gharama ya gari moja tu masikini Diwani wangu na wagombea wa ubunge Zanzibar eti wasizidishe mil.7, these people are not serious.
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kuna mechanism gani in place ya kujua kiasi kilichotumika katika uchaguzi?
   
 19. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  ndio maana nikasema viongozi mbumbu hawaachi kuonesha umbumbu wao.wametoa hii hesabu bila kufikiria ni kukurupuka tu ,nadhani hii ni moja ya sheria zinazotungwa kwenye mabaa au meza za chakula nyumbani.jitu linaamka tu linaamua kutunga sheria bila kufanya utafiti wowote.

  billioni 1 ambayo chenge alisema ni "vijisenti" unaenda kusema ndio kiwe kiwango cha kufanyia kampeni ? billioni 1 ambayo wameenda kumjengea gavana wa bot nyumba ndio hiwe kiwango cha mwisho mtu kutumia kwenye kampeni? kweli nchi yetu ina viongozi ambao wako makini na ufanyaji kazi wao?

  mie naona viongozi wetu wanafanya masiala sana kwenye swala la kuongoza nchi.wanafikiri kuwa kiongozi wa nchi sawa na kuongozi biashara yao binafsi ambayo unatoa maamuzi yako ya ajabu ajabu wakati wowote.
   
 20. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MFA1, umeteleza kidogo. Hiyo pesa hata RA hathubutu kutamka

  Inawezekana wao wameshapiga hesabu zao wanajua dau hilo hamna anayeweza kulifikia. Hata kwa helikopta.
   
Loading...