Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge wa CHADEMA Karagwe, Adolf Mukono, Wagombea udiwani Kata za Chanika na Kituntu wakamatawa na Jeshi la polisi

Deus J. Kahangwa

Senior Member
Jan 7, 2013
189
122
Mgombea Ubunge wa Chadema Karagwe, Adolf Mukono, wagombea udiwani Kata za Chanika na Kituntu wakamatawa na Jeshi la polisi

“Tumewakamata baada ya kupata malalamiko kutoka upande wa CCM wakidai kwamba Chadema hawana ratiba ya kufanya kampeni zozote katani Chanika. Tulipomwuliza Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya akatuthibitishia hilo. Nasi tumeona tuchukue hatua ili kuepusha shari. Lakini wahusika wanayo haki ya kupata dhamana ya kipolisi. Sisi tunawataka wagombea hawa wasitishe kampeni zao mpaka hapo mgogoro wao na Tume utakapomalizika,” anasema Henry Makwasa, OCD wa Karagwe kwa njia ya simu.

Kwa mujibu wa mashuhuda, na uthibitisho huu wa Henry Makwasa, ambaye ni OCD wa Karagwe, Jeshi la Polisi, limewakamata watu kadhaa akimwemo mgombea ubunge, Adolf Mukono, viongozi kadhaa wa Chadema, pamoja na wagombea udiwani wa Chadema katika kata za Chanika na Kituntu.

Tukio hili limejiri leo asubuhi baada ya jeshi la polisi kuvamia ofisi za Chadema katika Kata ya Chanika wilayani Karagwe. Tayari watu waliokamatwa wamesafirisha na jeshi la polisi hadi mjini Kayanga, kilometa zipatazo 10 kutoka katani Chanika.

Pamoja na Egbert Bazalengingo polisi wamewakamata wanachadema wengine wapatao nane, akiwemo mgombea udiwani wa Kata ya Kituntu, Josephat Ernest. Bazalengingo anasema kuwa yeye na timu yake walikuwa wanajiandaa kuanza safarari kutoka katika Ofisi za Kata ya Chanika zilizoko katika kijiji cha Chanika kwenda kufanya kampeni katika Kijiji cha Omulurama.

Mgomea ubunge Mukono na mgombea udiwani Ernest walizolewa na mapolisi hao wakiwa barabarani kati ya mji wa Kayanga na Kata ya Chanika, ambako watu wengine walikamatiwa.

Mgombea udiwani wa Chanika, Egbert Bazalengingo amemwambia mwandishi wa habari hizi kuwa, mapolisi hao waling’oa bendera zote zilizosimikwa kwenye eneo la ofisi za Chadema katika kata ya Chanika.

Pia, amesema kuwa, mapolisi hao wamechukua bendera zote zilizokuwa zimesimikwa kwenye pikpiki kadhaa ambazo zilikuwa zimepaki kwenye ofisi za Chadema za Kata.

Kwa mujibu wa Egbert Bazalengingo, kikosi cha mapolisi hao, kilifika kwenye ofisi cha Chadema Kata ya Chanika wakiwa wanaongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Peter Paul, akiwa ameshikilia karatasi yenye orodha ya majina ya viongozi na wanachama wa Chadema wa Kata ya Chanika.

Bazalengingo ameeleza kuwa, karatasi hiyo ndiyo ilitumiwa na jeshi la polisi kuwatambua na kuwakamata watu kadhaa. Mapolisi wanadaiwa kufika wakiwa na magari mawili, gari la Landrover pamoja na Canter.

Mbali na Kata ya Chanika, anakogombea Mgombea Egbert Bazalengingo, kuna Kata nyingine mbili zenye utata kama wa Chanika. Kata nyingine ni Bugene na Kayanga.

Wagombea udiwani wa Chadema katika Kata hizi tatu walienguliwa na wasimamizi wa uchaguzi wa Kata; wakakata rufaa, na rufaa zao kukubaliwa kupitia barua zilizoandikwa na Tume zikionyesha anwani ya NEC Dodoma.

Lakini baadaye kidogo, wagombea hawa waliitwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya hiyo, Godwin Kitonka, na kukabidhiwa barua nyingine kutoka NEC, safari hii zikiwa na anwani ya Dar es Salaam, wakitaarifiwa kwamba rufaa zao zimekataliwa. Barua za pili hazijaongelea wala kutengua barua za kwanza.

Kwa hiyo, wagombea wa Kata hizi tatu wanatumia barua zinazowaruhusu kushiriki uchaguzi kufanya kampeni za uchaguzi, wakati jeshi la polisi linatumia barua zinazowakataza kufanya kampeni kuwazuia.

Msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya aliyepitisha barua zote mbili na kuwapatia wagombea ameshindwa kutoa jawabu sahihi kuhusu maamuzi yanayogongana kutoka ofisi ile ile moja ya Tume. Ni mgogoro unaochafua taswira ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Mkuu wa Kituo cha Polisi wa Karagwe (OCD), aliongea na mwandishi wa habari hii na kukiri kuwatawanya wafuasi wa Chadema na kukamata baadhi yao, kama nukuu yake inavyoonyesha hapo juu.

Jitihada za kuongea na Msimamizi wa Uchaguzi wa Karagwe, Godwin Kitonka, hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokelewa.

“Naomba kujua utatuzi wa mgogoro wa kata za Bugene, Kayanga na Chanika umefikia wapi?” ni swali lilitumwa kwake kwa meseji na kufika, lakini pia halikujibiwa hadi habari hii inabandikwa hapa.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chadema Wilaya ya Karagwe, Amon Petro, hapo jana kati ya sita mchana na saa kumi na mbili jioni, Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wa Wilaya ya Karagwe, aliitisha kikao kilichojumuisha baadhi ya viongozi wa Chadema, OCD, OCCID na watu wengine kadhaa.

Ajenda kuu ilikuwa kuwataarifu viongozi wa Chadema kuwa kwa mujibu wa ofisi ya DSO Chadema hawapaswi kufanya mkutano wa siasa. DSO huyu alitumia nafasi hiyo kuwafahamisha viongozi wa Chadema kuwa atasimamia mtazamo wake huo kwa nguvu zake zote. Kikao hicho kilikwisha bila kufikia mwafaka.

Habari hii imeandaliwa na:

Deusdedith Jovin Kahangwa,
Simu: 0758341483/0682702333/0715386768
Email: deus.jovin@gmail.com
 
Polisi Angalieni sana hizo amri zenu kutoka juu mnazozitekeleza . Kuna amri halali na amri haramu . Sasa mkija kupelekwa the Hague msiseme hatukuwaambia .
 
Asante mwandishi kwa taarifa makini. Busara iwaongoze viongozi wa huko mnamharabia sana JPM na ccm kwa kura za huruma pia uthibitisho wa uchaguzi usio hurubna haki kinyume na sheria na tamko la Rais JPM.
 
Polisi usalama wa taifa Mkuruvenzi wote ni CCM itakuwaje tume iamrishe Wagombea warudishwe harafu kuwena baruwa nyingine iseme hawajareshwe charles mahera wa kutupwa kwenye tanuru la moto maana amejiandaa kusababisha vita nchk hii
 
Asante mwandishi kwa taarifa makini. Busara iwaongoze viongozi wa huko mnamharabia sana JPM na ccm kwa kura za huruma pia uthibitisho wa uchaguzi usio hurubna haki kinyume na sheria na tamko la Rais JPM.
Wengine Kule kwa Matiko wamevamia ofisi za Mbunge na kutumia nguvu kubwa kukamata walinzi kijambazi jambazi,hii ni aibu ya Mwaka.
 
Back
Top Bottom