Uchaguzi 2020 Mgombea Ubunge Kinondoni kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Saed Kubenea amesema anatarajia kushinda uchaguzi wa jimbo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,979
MGOMBEA Ubunge Kinondoni kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Saed Kubenea amesema anataraijia kushinda uchaguzi wa jimbo hilo kwa wastani wa asilimia 52.8 hadi 58.2.

Kubenea ametoa kauli hiyo leo tarehe 26 Oktoba 2020 wakati anazungumza na wanahabarii jijini Dar es Salaam, kuhusu mwenendo wa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni.

“Tuna uwezo wa kushinda uchaguzi huo ikiwa wapiga kura watakuwa kati ya 160,000 na 250,000 kati ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. Sisi tuna amini tutashinda kati ya asilimia 52.5 na 58.2 kama uchaguzi huo utakua huru,” amesema Kubenea.

Hata hivyo, Kubenea amesema ushindi utakuwa mwembamba kutokana na hatariu ya kugawana kura kati yake yeye na Mgombea Ubunge wa Kinondoni kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Susan Lyimo.

Kubenea amesema ana uhakika wa kushinda uchaguzi huo kutokana na mpinzani wake wa karibu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakubaliki kwa wananchi wa Kinondoni.

“Tuna uhakika wa kushinda na kwa sababu mgombea wa CCM hakubaliki. Hana watu amezungukwa na genge la kina madenge CCM wenyewe wanalalamika chama hakipo kimegawanyika. Hana mizi chini,” amesema Kubenea.

Kubene amesema wananchi wa Kinondoni wanahitaji mtu anayefanana nao, na kwamba yeye ana hizo sifa.

“Wananchi wa Kinondoni wanahitaji kuona mtu ambaye wanalingana kimaisha. Wakati wananchi wa Kinondoni wanazama kwenye maji yeye anakaa ghorofani. Wakati wananchi wanaishi na shida ya maji yeye anakaa ghorofani. Kinondoni inahitaji mtu anayefanana na shida zao na huyo sio mwingine wananiona ni mimi,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema ana uhakika wa kushinda kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Kinondoni na jiji la Dar es Salaam wanafahamu namna wabunge wa vyama vya upinzani walivyopigania masilahi yao.

“Pia wakati halmashauri iko Ukawa tulisimama kidete wananchi waliobomolewa nyumba zao walipwe fidia. Hivyo wananchi wanajua wabunge wa CCM hawakuchukua juhudi zozote kuishauri Serikali iwlaipe wananchi,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema ana uhakika wa kushinda kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Kinondoni na jiji la Dar es Salaam wanafahamu namna wabunge wa vyama vya upinzani walivyopigania masilahi yao.

“Pia wakati halmashauri iko Ukawa tulisimama kidete wananchi waliobomolewa nyumba zao walipwe fidia. Hivyo wananchi wanajua wabunge wa CCM hawakuchukua juhudi zozote kuishauri Serikali iwalipe wananchi,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema “Wananchi wanajua mpinzani wetu CCM iliongoza Kinondoni tangu nchi ipate uhuru lakini haina shule ya high level. Wananchi wanajua kwamba katika huduma zetu ya sekta ya afya sio nzuri imefikia hatua mwili wa marehemu huwezi kuuondoa bila kuulipia. Mama mjazito akifanyiwa operesheni analipa.”

Mwanasiasa huyo amesema sababu nyingine itakayomfanya ashinde uchaguzi huo, ni kufanikiwa kwake kuwafikia wananchi katika maeneo yote, licha ya kuchelewa kufanya kampeni.

“Mimi nitashinda kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kazi kubwa ambayo tumeifanya katika kampeni ambapo kwa muda mchache tumefanikiwa kufika kata zote 10 na mitaa 51 ya jimbo la Kinondoni,” amesema Kubenea.

Amesema katika kampeni zake alifanikiwa kufikisha sera zake kwa wananchi wa jimbo hilo.

“Tumeweza kuwasilisha hoja zinazowakabili wananchi wa Kinondoni ikiwemo suala la mafuriko na Mungu hua si athumani alileta baraka mbaya siku moja kwa kuleta mafuriko Dar es Salaam, wananchi wakaona wakakumbushwa juu ya adha ya mafuriko. Tulipoenda zungumza nao walikuwa ni mashahidi wa jambo lililowaathiri wakati wa uchaguzi,” amesema Kubenea.

1603716988013.png
 
Kubenea aliamini CDM imekufa, badala ya kukaa wakatafakari na wenzake, akasepa. Huko hapati kitu!
 
Badala ya kwenda kuongea na wapiga kura wake, yeye anaongea na “Waandishi wa Habari”

Huyu bwana Ubungo kaikimbia kwa aibu na kamuachia kazi ngumu sana Boni kuwin back imani ya wana Ubungo iliyopotea.

Yaani Ubungo imegeuzwa shamba la bibi. Mbunge wa CHADEMA anakula pesa miaka mitano, anavuta kiinua mgongo chake cha TZS. 250M+ then anahama jimbo just like that na kwenda kujaribu kwingine
 
Dar es salam inarudi Ccm

Tuliwachagua Chadema wakaishia kututesa na kupandisha kodi za kufanya biashara hadi Rais Magufuli alipoingia kati kwa kutoa vitambulisho
 
Back
Top Bottom