Kuna msululu mkubwa wa wagombea wa Chadema kujiengua hata kama majina yao yameshapitishwa, kama alivyokengeuka Slaa kuacha ubunge na kukurupukia Uraisi ,ndivyo hivyo wengi wa wachadema watakavyofanya alimuradi kuharibu kura za wanananchi.
Maalim Mwiba,
Naona swala la Dr. Slaa kugombea Urais limekukera sana ... pole sana ndugu yangu. Ambacho bado sijaelewa mpaka sasa, ulitaka CUF pekee ndio ipambane na CCM? Mbona vyama vingine vyote vimeweka wagombea na sijawahi kukusikia ukiwasema vibaya? Mgombea wa TLP (Mutamwega) alishawahi kuwa Mbunge huko kwao Mara, sijakusikia ukimsema aende kugombea Ubunge?
Tangu Kampeni zimeanza Prof. Lipumba ametembelea mikoa 4 tu [Lindi, Mtwara, Ruvuma na Mbeya]. Baada ya hiyo ziara akatoa tathimini ya CUF kwamba malengo yao ni kuchukua viti 20 huku Tanganyika. Sasa kama chama kina malengo ya kushinda majimbo 20 tu, ni kura zipi za wananchi ambazo zitakuwa zimeharibika?
Tukiweka ushabiki pembeni, CCM hawalii na Lipumba, wanalia na Dr. Slaa maana ndiye threat kwao na anawanyima usingizi. Ndio maana JK ameshindwa kuhudhuria shughuli za kisiasa nje nchi ambazo kwa kawaida tumezowea kuona anaenda mwenyewe, mfano, Mkutano wa UN, pale Rwanda na Burundi alipomtuma Pinda aende. Unadhani hiyo ni kawaida?
Ni haki yako kutetea CUF, lakini sioni hoja katika swala la Dr. Slaa kugombea. Sana sana ningemuomba kaka yangu Prof. Lipumba apumzike. Wenzake aliogombea nao kuanzia 1995 wameishawaachia wengine. Mrema na Cheyo wako majimboni. Akina Sengondo Mvungi, Mbatia, Mbowe na wengineo, walijaribu once wakashindwa wakawapisha wengine.
Kama Lipumba angesimama against Kikwete, CCM wasingehitaji kupiga kampeni kwa kuwa ungekuwa ni ushindi wa chee. Sasa hizo kura alizoharibu Dr. Slaa ziko wapi?