NEC yathibitisha mgombea wa Chadema kujitoa kugombea Ubunge jimbo la Singida Kaskazini

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,832
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imethibitisha kumtoa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge Singida Kaskazini mgombea kwa tiketi ya Chadema, David Djumbe.

Mgombea huyo ameondolewa kwenye orodha baada ya kutimiza masharti kujitoa katika uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima alisema jana kuwa Djumbe alifuata maelekezo kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi.

“Kama Sheria inavyosema Kifungu cha 49(1)(2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 mgombea anaweza kujitoa kwa kuandika barua na kuisaini yeye mwenyewe pamoja na ahadi ya kiapo cha sheria alichoapa mbele ya hakimu.

“Tume haimkubalii wala haimkatalii sababu ni hiari yake. Amewasilisha taarifa hizo na Tume imemfuta katika orodha ya wagombea,” alisema Kailima alipoulizwa jana kuhusu hatima ya mgombea huyo.

Desemba 20, Djumbe aliwasilisha nyaraka za kujitoa katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Januari 13 mwakani akieleza kuwa jina lake lilipelekwa kimakosa.

Mkanganyiko ndani ya Chadema ndiyo uliosababisha jina la Djumbe kupelekwa NEC na kupitishwa kuwa mgombea ubunge Singida Kaskazini.

Wakati Chadema ngazi ya Taifa ikisema haitashiriki katika uchaguzi huo mpaka NEC itakapokutana na wadau kujadili changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi wa udiwani katika kata 43, uongozi wa chama hicho mkoani Singida ulipeleka Tume jina la Djumbe kuwa mgombea.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida, Shaban Limu alisema Djumbe aliteuliwa kugombea na kamati ya utendaji ya wilaya.

Alisema wakati anateuliwa uongozi wilaya na mkoa ulikuwa haujawasiliana na makao makuu kujua msimamo juu ya uchaguzi huo.

Jimbo la Singida Kaskazini liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya CCM, Lazaro Nyalandu kujivua uanachama wa chama hicho hivyo kupoteza nyadhifa zote ukiwamo ubunge. Alijiunga na Chadema.

Uchaguzi pia unafanyika katika majimbo ya Longido ambako matokeo ya uchaguzi wa ubunge ya mwaka 2015 yalibatilishwa na Mahakama; na Songea Mjini ambako aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya CCM, Leonidas Gama alifariki dunia.

Chanzo: Mwananchi
 
Nyalandu mpaka leo sijui ni kwa nini aliachia ubunge inawezekana ni maagano yake na waganga wa kienyeji
 
Safi sana waacheni CCM wajitekenye wenyewe wajichekeshe wenyewe.

Ushauri kwa NEC, kuliko kuteketeza mabilioni ya walipa kodi kwanini wasimtangaze tu mshindi kwa sababu tayari anajulikana.
 
MKURUGENZI-wa-Uchaguzi-wa-Tume-ya-Taifa-ya-Uchuguzi-NEC-Ramadhani-Kailima-620x308.jpg

HATIMAYE Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imethibitisha kumtoa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa Singida Kaskazini mgombea kwa tiketi ya Chadema, David Djumbe.

Mgombea huyo ambaye amekuwa akitangaza kujitoa huku NEC ikitangaza kutokidhi vigezo vya kujitoa jana Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima amethibitisha kumuondoa kwenye orodha ya wagombea baada ya kutimiza masharti ya kujitoa kwa mujibu wa sheria.

Mkurugenzi huyo amesema: “Kama Sheria inavyosema Kifungu cha 49 (1) (2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura 343 mgombea anaweza kujitoa kwa kuandika barua na kuisaini yeye mwenyewe pamoja na ahadi ya kiapo cha sheria alichoapa mbele ya hakimu.

“Tume haimkubalii wala haimkatalii sababu jambo hilo ni hiyari yake. Tayari amewasilisha taarifa hizo na Tume imemfuta katika orodha ya wagombea,” amesema Kailima.

Desemba 20, Djumbe aliwasilisha nyaraka za kujitoa katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Januari 13 mwakani akieleza kuwa jina lake lilipelekwa kimakosa.

Mkanganyiko ndani ya Chadema ndiyo uliosababisha jina la Djumbe kupelekwa NEC na kupitishwa kuwa mgombea ubunge Singida Kaskazini.

Wakati Chadema ngazi ya Taifa ikisema haitashiriki katika uchaguzi huo hadi NEC itakapokutana na wadau kujadili changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi wa udiwani katika kata 43, uongozi wa chama hicho mkoani Singida ulipeleka Tume jina la Djumbe kuwa mgombea.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida, Shaban Limu amesema Djumbe aliteuliwa kugombea na kamati ya utendaji ya wilaya.

Amesema wakati anateuliwa uongozi wilaya na mkoa ulikuwa haujawasiliana na Makao Makuu kujua msimamo juu ya uchaguzi huo.

Jimbo la Singida Kaskazini liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya CCM, Lazaro Nyalandu kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga Chadema hivyo kupoteza nyadhifa zake zote za chama na ubunge.

Uchaguzi huo wa marudio utafanyika pia katika majimbo ya Longido ambako matokeo ya uchaguzi wa ubunge ya mwaka 2015 yalibatilishwa na Mahakama; na Songea Mjini ambako aliyekuwa mbunge kwa tiketi ya CCM, Leonidas Gama kufariki dunia.
 
Hivi silaha aliyotumia Mwamwindi Siku hizi hazipo tukawamaliza hawa wajinga?
 
Sawa hata Raila aligomea hivyo hivyo na bado uchaguzi imefanyika na Kenyatta kaapishwa kuwa Rais. Kama kweli Mbowe na chama chake wana msimamo huo wanaousimamia basi awatake wabunge wote wa Chadema wajiuzulu. Ili uchaguzi urudiwe na wasishiriki ili tuwe na bunge la chama kimoja.
 
Back
Top Bottom