Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,361
- 2,734
Naongea haya nikiwa na machungu sana baada ya kuona fitina zinazoendelea kwenye jimbo la Nkenge ambapo baada ya kuondolewa Assumpter Mshama na nafasi yake kuchukuliwa na Dr. Kamala hujuma za ajabu zimeanza.
Inaelekea UKAWA wameamua kuwa mgombea wa UKAWA atakayewania jimbo hilo ni kutoka NCCR – Mageuzi. Sina Ugomvi na NCCR ila ukweli ni kuwa NCCR huku haipo. Mgombea kutoka CHADEMA ndiye anayejulikana bwana Valerian Rugarabamu. Huyu kashiriki kuanzisha misingi na matawi ya CDM kila kata.
Pia maajabu ni kuwa, NCCR katika uchaguzi ujao haina mgombea hata mmoja katika kata 20 za Missenyi, wakati katika kata zote hizo CHADEMA imesimamisha wagombea wa Udiwani. Kinachonishangaza wanaoshangilia UKAWA kumsimamisha mgombea kupitia NCCR – Mageuzi ni watu wa CCM.
Habari nyingine zinadai kuwa iwapo huyo mama wa NCCR atasimamishwa, mwisho wa siku atajiondoa na bwana Kamala apite kiulaini maana huyo mama anaweza kupewa cash nzuri. Huyu Kamanda anayejulikana, aliyepigana kuanzisha matawi na misingi ya chama, akashinda kwenye kura za maoni, leo hii eti ampishe mwingine basi nafuu hata angekuwa ni ndani ya chama lakini chama kingine ambacho hakina hata mgombea mmoja ngazi ya kata?????!!!!!
Pamoja na hayo, huyu bwana wa CDM anaambiwa basi ahamie NCCR!!!! Ghafla!! Hii haiwezekani. Ninachotaka kuwaambia CHADEMA kama mmeona maeneo yote ndo kuna watanzania wenye uchungu na nchi yao, mkaona Kagera ndo mkoa wa kufanyia majaribio na experiment kwamba tupate mabadiliko au tusipate basi to hell with us, itatugharimu. Msiwachezee wananchi(umma) kabisa.
Kwa sababu hizi CHADEMA na Ukawa kwa ujumla, gawaneni majimbo lakini pasipo kutukwaza sisi wananchama kwa kuleta kitu ambacho hata hakipo. Sehemu mnapoona Chama flani kinakubalika wekeni mgombea wa chama husika. Ni sawa muda huu kule kwa akina Kafulila mkamsimamishe mgombea kutoka chama cha NLD au kule kwa akina Joshua Nassari mpeleke CUF.
Fanyeni changes ambazo hazina direct confusion kama ya Babu Duni kuwa mgombea mwenza.
Tambueni katika Sensa ya 2012 Tanzania, Kagera inashika nafasi ya (nne 4) kwa wingi wa watu ikitanguliwa na Dar, Mwanza na Mbeya. Hivo acheni utani aisee ina watu million (2.46) Kama mpango wa hujuma ni wa CCM, basi kuweni makini.