Mgogoro wa DR Congo na Rwanda wafikia pabaya

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Ubelgiji na Ufaransa Wamekuwa wakivuna shamba la Madini la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kulifaidi pasipo kupanda kitu.

Nchi ya Congo ni moja katika ya nchi duniani zenye utajiri mkubwa wa madini lakini ajabu ni kwamba Congo ni kati ya nchi 10 maskini zaidi duniani!

Kumekuwa na mgogoro wa DR Congo na Rwanda, mgogoro huo kwa sasa umefikia pabaya kwani DR Congo imempa Balozi wa Rwanda, Vincent Karenga saa 48 kuondoka.

Congo inaituhumu Rwanda kuwa inawasapoti na kuwaunga mkono waasi wa M23.

Hata hivyo Rwanda siku zote wamepinga madai hayo! Kumekuwa na suluhisho za kidiplomasia lakini zote hizo hazikufua dafu mpaka sasa Rais wa Congo yuko tayari kutumia nguvu za kijeshi kutatua suala hilo, Rwanda imejibu na kusema wako tayari kwa hatua zozote za kichokozi za Congo.

Nchi hizi mbili ni washirika wa Afrika Mashariki, hivo basi lolote litakalojitokeza basi lina athari kwa Jumuiya yote ya Afrika Mashariki.

Ufaransa na Ubelgiji wanajua kila kitu kinachoendelea.

Afrika yafaa kuungana na kumpiga adui.
 
Waafrïka bana...mnafanya upumbavu wenu huko mnauana mnakuja mnasingizia wazungu

Mfano Juzi uchaguzi wa Kenya umefanyika vizuri, Raila akakataa matokeo na kupanga vurugu, baadae akaja kukiri mwenyewe kuwa mabalozi wa nchi za Ulaya ndio walimtuliza
Ila angekataa na kuvuruga tungelaumu wazungu tena, ndio maana dunia nzima inaona Waafrika ni manyani tu
 
Samia awasuluhishe tumechoka na migogoro isioisha na Wakimbizi.
Katika mambo ambayo inanilazimu kusifu Tanzania ni hili la mgogoro huu wa DRC.

Nashukuru sana kwamba Tanzania haikujifanya mjuaji na kujiweka kimbelembele katika swala zima.

Kukaa kwake pembeni na kuangalia hali inavyokwenda kumeipa heshima, na mwishowe inawezekana ndiyo ikawa na majibu ya ufumbuzi wa mgogoro wenyewe.
 
Tanzania kukaa kwake kimya huku ikiendelea kubeba mzigo wa wakimbizi ni ujinga wa kiwango cha SGR
 
Waafrïka bana...mnafanya upumbavu wenu huko mnauana mnakuja mnasingizia wazungu

Mfano Juzi uchaguzi wa Kenya umefanyika vizuri, Raila akakataa matokeo na kupanga vurugu, baadae akaja kukiri mwenyewe kuwa mabalozi wa nchi za Ulaya ndio walimtuliza
Ila angekataa na kuvuruga tungelaumu wazungu tena, ndio maana dunia nzima inaona Waafrika ni manyani tu
Dah, mkuu 'Johnny Sack', kuwatetea hao wazungu, pamoja na uzuzu wetu ni jambo gumu sana kulifanya.

Ninakubaliana nawe juu ya upumbavu wetu, lakini kuwatetea hao watu? Hapana.
 
Tanzania kukaa kwake kimya huku ikiendelea kubeba mzigo wa wakimbizi ni ujinga wa kiwango cha SGR
Hapana.
Kwanza wakimbizi ni kutoka Burundi na Rwanda, kwa hiyo huo mzigo unaouona wewe ni 'mirage' tu inayotoka kwenye ubongo na kupitia machoni.
Kuna wakati na nafasi ya kufanya kazi hiyo kwa heshima, siyo kurukia tu jambo mradi uonekane nawe umo, kumbe huna lolote la maana unaloweza kuchangia katika kutafuta ufumbuzi.
 
Back
Top Bottom