Sasa ni dhahiri kuwa kuna mgogoro wa chini kwa chini ndani ya CHADEMA kati ya viongozi wake, ingawa viongozi wake wamekuwa wakifanya kila jitihada kuficha
Tukio la hivi karibuni viongozi wake wamekuwa wakifanya kila njia kuhakikisha suala la Mnyika kumtumia sms za vitisho Mh. Mwigulu Nchemba linamalizwa nje ya vyombo vya usalama, viongozi wamekuwa wakimshutumu sana Mnyika kwa uamuzi alioufanya wa kutuma sms za vitisho kwa Nchemba hali inayokifanya chama kutumia nguvu kubwa kushughulikia suala hilo, pia wamekuwa wakimshutumu kwa uamuzi wake wa kwenda kufanya mkutano huko Singida hadi kusababisha mauaji.
Pia umetokea msuguano kati ya Mbowe na Zitto kutokana na uamuzi wa Zitto kususia kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge pamoja na wabunge wengine wa CHADEMA baada ya kutokea msuguano kati Tundu Lissu na Werema, inasemekana siku hiyo Mbowe ambaye hakuwepo Bungeni alimtumia sms Zitto akimshutumu Zitto kwa uamuzi wake wa kubaki ukumbini wakati wenzake wanatoka nje, hata hivyo inasemekana Zitto alimjibu Mbowe kuwa suala lile lilikuwa kati ya Lissu na Werema hivyo lilikuwa halimhusu yeye,
NOTE: Kama hali iko hivi mapema itakuwaje wakikabidhiwa nchi, si watachinjana hawa
Nawasilisha!!!?