Mgogoro mkubwa wafukuta TBC

Mgogoro mkubwa wafukuta TBC

Sasa nimeamini kumbe rais wa china anataka kusaidia tbc kuna kitu anataka,jamani nimegundua kuna siri kubwa sana tbc,tunaomba mtwambie,kitu kingine nimegundua kuwa hakuna uhuru wa mwandishi katika tbc.so hatutafika sehemu kama wanasiasa wanaingilia uhuru wa vyombo vya habari
Ndani ya Taasisi ya Utangazaji Tanzania(TBC) kwa sasa kuna mgogoro mkubwa sana unafukuta chini kwa chini ukihusisha pande mbili kuu, yaani Wafanyakazi wa kawaida na Uongozi wa juu wa shirika hilo, kuhusu madai yafuatao na huku wakitaka Mkurugenzi mkuu wa sasa wa TBC afukuzwe na bodi ya shirika hilo ivunjwe;

1/Ubaguzi katika kupewa vyeo, Posho na marupurupu(Suala la Itikadi, Ukanda na Udini linatajwa sana)

2/Kuruhusu wanasiasa(Viongozi wa serikali na makada wa CCM) kuingilia wanavyotaka kazi za kitaaluma katika utoaji wa habari hususani kuhariri(Kuchuja) habari.

3/Kutokulipwa malimbikizo ya madeni ya madai ya siku za nyuma.

4/Utendaji Duni na Mbovu wa Mkurugenzi mkuu Clement Mshana hadi kufikia kumpa jina la dhihaka la 'BOYA'

5/Vitisho vya kufukuzwa kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohoji sana mwenendo mbovu wa shirika hilo kwa sasa.

6/Mvutano wa Chini kwa chini kati ya Wakurugenzi waliowekwa na Lowassa wakati akiwa waziri mkuu na wapya walioletwa na Pinda.

*Pia kuna issue ya mkataba tata(White Elephant) kati ya TBC na Startimes(Wachina!) ambao Terms, Conditions, Investment, Dividend na Shares havijawekwa wazi na sawasawa, japokuwa Mkurugenzi mkuu na Bodi yake ya sasa wanadai wameurithi tu lakini sio 'wapishi' kamili wa hicho kilichopikwa!!
 
Pasco
Labda ufafanue ni siri ipi ya serikali inayofaa kutunzwa?
kuingiliwa kazini au kunyimwa uhuru wa kufanya kazi kulingana na taaluma yako nayo ni siri?
Sio kila siri ni siri.
Tuseme ukijua mwajiri wako ni fisadi au mfujaji wa mali ya umma unakaa kimya kwa vile ni siri kusema ya boss wako?
nadhani usikimbilie kusema mwajiriwa anapaswa kutunza siri
angalia credibility ya hizo siri.
siri ambazo zina walakini au zina maslahi kwa watu wachache sio siri..
Watanzania tumelelewa uoga tu na unafiki kwa vile tunaogopana
Bila hivo nchi haitafika popote
Ni vema tumejua uozo wa TBC ili tuipiganie iwe mali ya umma
ni chombo chetu,kinaendeshwa kwa kodi zetu lazima tujue yanayojiri humo.

.

Mkuu Lokissa, hapa tunazungumzia vitu viwili tofauti, mimi nazungumzia utii wa sheria bila shuruti kwa kufuata, sheria taratibu na kanuni!, mimi niliwahi kuwa mtumishi wa umma, na miongoni mwa mambo ya msingi sana kwa mtumishi wa umma, ni pamoja na kutunza siri za serikali!.

Kusema ukweli daima is one thing, na utunzaji wa siri za serikali is another thing, kama ilivyo katika familia, unapogundua wife wako kacheza rafu, unatangazia majirani na mataifa?, ili iweje?. Utumishi wa umma umeweka kanuni na taratibu za kila jambo!, sasa hili la kuwatangazia mataifa matatizo yao ya ndani ndio ili iweje?!.

Hata hao wanasheria, nao wana yao ambayo wanayajua kwa ukweli halisi, lakini bado wanamshauri mteja wao akanushe!.

TBC ni taasisi nyeti, inayohitaji uvumilivu na ustahimilivu wa hali ya juu kuwepo pale!, sisi tulioshindwa hayo, tulifungwashwa virago vyetu tukatimuliwa!, na akipatikana aliyeyaleta haya humu jf, anatakiwa kufungashwa!. Channels za malalamiko zipo, hapa jf wanaleta mambo yao ya ndani ya nini?!. Huku ni kumwaga tuu mpunga kwenye kuku wengi!.

Pasco.
 
hivi hii tbc bado ipo? mie nilishapiga marufuku tv yangu kuonyesha hii kitu, huwa nahisi inanakula sana umeme

Teh teh teh.
HII TBC MIMI NAIPENDWA KWASABABU YA TAARABU TU.
Siwezi angalia habar kamwe.
Alafu ukitaka umeme ukatikekatike we weka TBC.
 
Sifa kuu ya kwanza kwa mtumishi wa umma ni kutunza siri za serikali!.
Whoever aliyezitoa taarifa hizo nje, amekiuka masharti yake ya ajira na akipatikana ni summary dismissal!.
Pasco.
Nje ni wapi huko wakati sisi ndio mabosi wao inabidi tuarifiwe ili tuchukue hatua hata kama ni kuandamana
 
Mwanachi sokoni ni 800/= Uhuru, HabariLeo ni 500/= lakini hilo la 800/= linauzika sana zaidi kupita hayo ya 500/= kazi nzuri ya Tido.
 
Pasco
Labda ufafanue ni siri ipi ya serikali inayofaa kutunzwa?
kuingiliwa kazini au kunyimwa uhuru wa kufanya kazi kulingana na taaluma yako nayo ni siri?
Sio kila siri ni siri.
Tuseme ukijua mwajiri wako ni fisadi au mfujaji wa mali ya umma unakaa kimya kwa vile ni siri kusema ya boss wako?
nadhani usikimbilie kusema mwajiriwa anapaswa kutunza siri
angalia credibility ya hizo siri.
siri ambazo zina walakini au zina maslahi kwa watu wachache sio siri..
Watanzania tumelelewa uoga tu na unafiki kwa vile tunaogopana
Bila hivo nchi haitafika popote
Ni vema tumejua uozo wa TBC ili tuipiganie iwe mali ya umma
ni chombo chetu,kinaendeshwa kwa kodi zetu lazima tujue yanayojiri humo.
Mkuu Lokissa, taasisi kama familia, inazo siri za kawaida, secrets, zipo za restrictions na inazo siri za confidential, nakumbuka tulipokuwa wadogo, tulikatazwa hata kutangaza tumekula nini!, yako mambo ya operations za policies, issues za policies ni public, issues za operations ni mambo ya ndani, kama yana matatizo, zipo taratibu za kuyashughulikia!.

Kiukweli kuna tofauti kati ya taasisi za serikali, na taasisi za umma, yaani government media vs public corporations!. T TBC is supposed to be a public television, but its still a government TV, hivyo watumishi wa TBC ni watumishi wa serikali, wanawajibu wa kutunza siri za serikali!.

Pasco.
 
Hii ni moja tu kati ya mifano iliyo hai. Chombo chochote kinachoendeshwa na CCM siku zote ni kibovu kwani hawana utaalam na maadili mema ya utawala.
 
Haa ... jamani mkurugenzi tido kumbe alishaondoka....!
 
bado Pasco hujaeleza ni siri zipi zinafaa kuwa confidential
na je kwa mtoa mada kuanika uozo amevunja miiko ipi?
lazima wewe kama mchambuzi wa sheria ujue what is supposed to be confidential
na yale maingiliano ya watala ktk kudidimiza uhuru wa wanahabari ktk kutoa habari katika chombo chetu cha taifa nako tuite ni confidential?
Ifike mahali tukubali ukweli bila kuwa wanafiki.

Mkuu Lokissa, taasisi kama familia, inazo siri za kawaida, secrets, zipo za restrictions na inazo siri za confidential, nakumbuka tulipokuwa wadogo, tulikatazwa hata kutangaza tumekula nini!, yako mambo ya operations za policies, issues za policies ni public, issues za operations ni mambo ya ndani, kama yana matatizo, zipo taratibu za kuyashughulikia!.

Kiukweli kuna tofauti kati ya taasisi za serikali, na taasisi za umma, yaani government media vs public corporations!. T TBC is supposed to be a public television, but its still a government TV, hivyo watumishi wa TBC ni watumishi wa serikali, wanawajibu wa kutunza siri za serikali!.

Pasco.
 
TBC nashindwa kuitambua vyema kazi zake kama SU hasa kunapokuwapo na shida au janga ktk taifa mfano lilipoanguka gorofa yenyewe inaweka kipindi cha mapishi,baadaye taarabu huwa najisikia vibaya itazame KBC utaipenda
 
Mkuu Salim Kabora, nimekubali, na hatua zifuate!.
P.

Aghhh mwanangu Pasco naziaminia nondo zako bhana muhimu kulinda maslahi ya ofisi lakini ikiwa too much selflike inabidi tujitenge kiaina.......
 
Tido alikuwa jembe pale, sasa kupeana kwa huyu ni mjomba madhara yake ndo hayo.
 
Back
Top Bottom