..Dah! Mkuu Pasco kuna wakati huwa Unaniangusha kweli!
Huu ni Mmoja wapo.
Hebu nisiseme mengi lakini turudi shule zetu zilee zilizokuwa shule halafu tukumbushane maana ya Misemo na Methali hizi:
1. Mficha Uchi, Hazai.
2. Mficha Ugonjwa Kifo Kitamuumbua.
3. Kufa na Tai Shingoni.
4. Msema Kweli ni Mpenzi wa Mungu.
5. Kufagia na kusumiza Uchafu chini ya Zulia badala ya Kuutupa Nje.
6.
7.
....Ngoja niwapishe na wenzangu waje kuongezea hapa......:yo:
Sio hilo tuu,hata kusoma habari ambazo ni uongo na uzushi wa dhahiri lazima sura na nafsi vitofautiane. Mfano umepewa scrip imeandikwa " Katika miaka 50 ya uhuru wetu chama Tawala CCM kimeboresha maisha ya Mtanzania kwa kiwango cha juu kuliko mataifa mengi kusini ya jangwa la Sahara na sasa ahadi ile ya maisha bora kwa kila Mtanzania imetimia ....."hata mtangazaji akiwa anatangaza taarifa utamwona anavyotangaza kwa unyonge kama amelazimishwa vile kumbe hajalipwa mshahara
So far kuusema ukweli, TBC ndio the best TV Station in Tanzania kwa vifaa,
manpower na majengo, kinachohitajika ni Mshana ku open up a bit kuruhusu outside productions ku boost up their limited creativity!.
Ila pia whoever aliyeleta hii kitu humu jf, huyo hafai kabisa kuendelea kuwa mtumishi wa umma!. Mambo kama haya yalipaswa kuwa siri za ndani za serikali!.
Mimi nimefanya kazi TBC na kuna mengi ya hovyo na ya ajabu nimeyashuhudia lakini hakuna hata siku moja nimewahi kusema humu TBC hivi au TBC vile!. Hawa watakuwa ni hawa vijana wapya walio ajiriwa juzi juzi wasio na uvumilivu wa kiserikali wanataka kutuaibishia shirika letu!.
Hawa ni wa kutafutwa na kuadabishwa!.
Pasco.
hata senti moja ya mtanzania maskini haita kwenda bure,,nakwambia itakwenda na mtu,leo tbc wamepokwa watanzania na kupewa ccm,chombo ambacho ni mali ya watanzania,tbc imekua ni kijiwe cha ccm,inakwenda kukesha chimwaga kurusha live mambo ya chama,huku watanzania wakinyimwa hata burudani ya timu yao ya taifa inapocheza,matangazo yanakatizwa halafu kanajitokeza kamtu kanasema tunajiunga live dodoma chimwaga,huu ni upuhuzi ambao auwezi kuruhusiwa kuendelea kwenye mashirika ya uma,leo mtu yoyote wa ccm akitaka kupiga propaganda kwa cdm,huyoooooo tbc anapewa kipindi na kutekeleza mambo yake,nawapongeza sana hawa wafanyakazi wa tbc hambao hawataki tena kutumiwa na vibaraka wa ccm,,,,,na mimi nawaunga mkono huyu bw,mshana hafai hafai aendezake akapewe ukuu wa wilaya,na senti za kodi za watanzania zitawa tafuna,muda si mrefu kitaeleweka,mshaanza kushikana uchawi! Ngoma inogile..kodi zetu zinawalaani.
Mjukuu wangu, unapotoa hoja wenzako wanaipima ili waitekeleze kwa nia nia ya kuboresha mapungufu yaliyojitokeza. Kwa hoja yako hii unawapa shida wenzako na pia hujamtendea haki aliyekupeleka shule, hoja zako zinaonyesha uwezo wako. Ngoja niachane na wewe.Wajukuu zangu, mtoa habari anaonyesha wazi anaegemea upande wa wanaopinga menejiment, ndiyo maana hata jina la dhihaka la kiongozi wake amelitaja. Lakini ukisoma kwa kina unaona kuwa kuna vita kati ya watu wa EL na wa mtoto wa mkulima kama mtoa mada alivyodai. Kama ndivyo hivyo, hapo pana hujuma ya hali ya juu kati ya kundi moja dhidi ya lingine.Nimekuwa nikufuatilia sana wamiliki wa TV binafsi walivyo na chuki na TBC, inawezekana hicho kilichoandikwa ni mpango tu wa kuwataka wenye uwezo mdogo wa kufikiri kama mjukuu wangu YOYO wakimbilie kuropoka. Katika sakata hili unahitajika utulivu, kuchunguza kwa kina na kutoa maamuzi yenye tija na wala siyo ya jazba. Wajukuu zangu si mnajua tena Bunge ndo hilo linaanza, wajanja wanatanguliza hoja ili watu wa mjengoni waidake na kuitolea maamuzi ambayo yanaweza yakawa mazuri au vinginevyo. No research no right to speak.
So far kuusema ukweli, TBC ndio the best TV Station in Tanzania kwa vifaa,
manpower na majengo, kinachohitajika ni Mshana ku open up a bit kuruhusu outside productions ku boost up their limited creativity!.
Ila pia whoever aliyeleta hii kitu humu jf, huyo hafai kabisa kuendelea kuwa mtumishi wa umma!. Mambo kama haya yalipaswa kuwa siri za ndani za serikali!.
Mimi nimefanya kazi TBC na kuna mengi ya hovyo na ya ajabu nimeyashuhudia lakini hakuna hata siku moja nimewahi kusema humu TBC hivi au TBC vile!. Hawa watakuwa ni hawa vijana wapya walio ajiriwa juzi juzi wasio na uvumilivu wa kiserikali wanataka kutuaibishia shirika letu!.
Hawa ni wa kutafutwa na kuadabishwa!.
Pasco.
Mkuu Wambi, hivi Tido, ni walimbwaga au mkataba wake ulikwisha?!.Walipombwaga Tido walithani atatetereeka... Sasa ana bonge la ofisi Mwananchi. Poleni tbc
.ucha kuongea kama siio mwanasheria kasema ukweli na ukweli ndio dira ya maendeleo bila ukweli nchi itayumba ukweli ndio utatuweka huru nampongeza mtoa mada
Sijui kama tunahitaji TBC kwani tangu nizaliwe hapa maeneo yetu (kyerwa) inasikika usiku tu kupitia MW peke yake.