MGOGORO: Malumbano ya UVCCM, Viongozi wastaafu na Hatima ya CCM

Ushauri wa bure kwa Sita, Mwakyembe, Magufuli, Kilango, Ole Sendeka na Tibaijuka. Ndege wa kundi moja huruka pamoja. Ukitembea na mwizi utakuwa mwizi. Kwa harakaharaka wote mnaonekana nyie ni watu wasafi katika dimbwi la mafisadi. Mnatumia nguvu nyingi sana kujibambanua na kuonyesha tofauti zenu na mafisadi.

Amueni sasa kujiunga na mafisadi kabisa ili nanyi muishi kwa amani, msitishiwe kuuwawa , nanyie anzisheni madili yenu kama ya Richmondi na dowans AU Jitoeni kama Mpendazoe ili mjiunge kundi linalo eleweka
kuwa sawa na dhamira zenu, najua mnalijua. Karibuni sana msingoje mpaka UVCCM wawafukuze.
 
yaani hili movu ni tamu kama la amitta bachani..yaani ngoja nisubiri sumaye aongee ndo ntajua muvu limekolea sasa hivi bado kwanza
 
Ushauri wa bure kwa Sita, Mwakyembe, Magufuli, Kilango, Ole Sendeka na Tibaijuka. Ndege wa kundi moja huruka pamoja. Ukitembea na mwizi utakuwa mwizi. Kwa harakaharaka wote mnaonekana nyie ni watu wasafi katika dimbwi la mafisadi. Mnatumia nguvu nyingi sana kujibambanua na kuonyesha tofauti zenu na mafisadi.

Amueni sasa kujiunga na mafisadi kabisa ili nanyi muishi kwa amani, msitishiwe kuuwawa , nanyie anzisheni madili yenu kama ya Richmondi na dowans AU Jitoeni kama Mpendazoe ili mjiunge kundi linalo eleweka
kuwa sawa na dhamira zenu, najua mnalijua. Karibuni sana msingoje mpaka UVCCM wawafukuze.

Tunataka kujenga vyama viwili vyenye nguvu acha wabaki huko ili tutakapo wamaliza mafisadi tubaki na watu wenye akili timamu kwenye vyama vyetu viwili kujenga nchi aliyotuwekea misingi baba wa taifa letu. Tutakuwa tunashindana kwa nguvu ya hoja na si kwa nguvu ya matumbo na ukubwa wa vitambi.
 
Kumbe CCM inakaribia kuzikwa...Hivi hawa jamaa wanaojiita UVCCM wanaposema eti sasa ni zamu yao kula maana hawajala kabisa na waachwe wale wanatuchukuliaje sisi watz? Ama kweli hili li nchi linapoelekea mi si paelewi. Ningesema najuta kuzaliwa tz ila siwezi kusema maana ntakuwa natukana...
Hivi hawa masharobaro wa CCM ambao CCM inawategemea kama watawala wa kesho tuwafanyeje?
 
ningependa kufahamu chanzo cha taarifa hii tafadhali au ndio zile za uchochezi.
 
Kumbe CCM inakaribia kuzikwa...Hivi hawa jamaa wanaojiita UVCCM wanaposema eti sasa ni zamu yao kula maana hawajala kabisa na waachwe wale wanatuchukuliaje sisi watz? Ama kweli hili li nchi linapoelekea mi si paelewi. Ningesema najuta kuzaliwa tz ila siwezi kusema maana ntakuwa natukana...
Hivi hawa masharobaro wa CCM ambao CCM inawategemea kama watawala wa kesho tuwafanyeje?
Labda wakaliloweshee to mingozi ndio wale maana kama ni nyama basi wajanja wenye meno katika taifa hili ndani ya CCM walishatafuna yote na taifa kuenenda tu ki-hobelahobela vile.

Kwa nini hawakuamka au kuamshwa mapema kula na wale magwiji ya UFISADI nchini kwa kipindi chote hicho. Sasa ndio kusema wanaposema kwa MAFISADI kwamba sasa ni zamu yao ya kula kama ambavyo wakua wakifanya hao wakubwa wao ndio tuseme mipango mingine ya KIFISADI lakini safari hii ikipitia UVCCM ndio iko njiani???
 
mmhhh...kumbe kazi bado tunayo watanzania....kumbe ufisadi hautaisha maana bado mafisadi wanazaliwa kila kukicha!!!
 
Kwa bahati mbaya nilikuta tayari progaram ikiwa imeanza kama nusu saa zaidi ila Kwa Michango ya Washiriki Mada ilìhusu hatma ya CCM.

Binafsi nimevutiwa sana na huyu kijana anaeitwa Sabato Nyamsano juu ya uelewa wake wa Mambo mengi yanayolihusu Taifa napia uwezo wake wa kujenga Hoja..

Akiiongelea UVCCM alifanya reference juu Ya ile Youth...Yakipindi cha Mwl na Jinsi Mwl alivyoipend nakujivunia Juu ya Uzalendo wake.

Akiiöngelea hii ya leo amehoji Je hao uv kweli ni vijana, Pili Je wanawawakilisha vijana wapi? Ni hawa wapiga debe, ni hawa Wamachinga au Mama ntilie.

Akahoji mbona wengi wao wanaishi katika Utajiri wa kutisha hawa wamefanya kazi wapi na lini mpaka kuwa na hizo mali, Mbona wanaonekana kununuliwa nakutumiwa!

Amewataka wajitafakari sababu Wanafanya Maigizo.
 
Yap...Jamaa yupo safi...confidence juu,anajenga hoja anajipanga......Bravo Sabato
 
Birigita na Only 83 nakubaliana na nyie ukweli nikwamba ingawa hata mie ni kijana hiyo hiyo age yake iv Huyu mwenzetu ni Hazina kubwa kwa Taifa kutokana na Uzalendo tu anaounyesha katika Mazungumzo yake na upeo wake wakupembua na kuchambua mambo naamini kabisa Watanzania akihitaji nafasi na Watanzania wakampa nafasi yakuimplimenti ivyo vitu atatuvusha kutoka level1 kwenda nyingine.
 
Nimemkubali huyu kijana jinsi anavyochambua,wasanii wa uvccm(matapeli)wanaojiwakilisha na matapeli wenzao
 
Nilivyoona Sabato nikafikiri ni Prof. Larry Sabato ataichambuaje uvccm? .. .. .. najiondokea
 
yap i've heard him anajua kujenga hoja kilichonifurahisha ni vile alivyosema watz wameshtukia usanii wa uvccm na kweli tushawastukia ni wasanii tatizo lao uvccm hawakai na watz wa kawaida sababu ya ukwasi wao so wanafikiri wametupata waende ktk vijiwe,sokoni au wapande daladala wasikie wanavyopondwa yaaani sasa ni NGASTUKAAA! Hatudanganyiki
 
UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umeanza kutekeleza kwa vitendo azimio lake la kuahidi kupambana na viongozi wa chama hicho wanaodaiwa kutoa matamko bila kufuata utaratibu, kwa kutangaza kumvua nafasi ya ulezi wa UVCCM Mkoa wa Tabora, Spika wa zamani, Samuel Sitta.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Baraza Kuu la UVCCM, lilitangaza baada ya kikao chake Dodoma, kuwa katika kukabiliana na viongozi hao, litahakikisha viongozi wa CCM wanaotoa matamko bila kufuata utaratibu, hawapati nafasi yoyote ya uongozi na chama kisiwateue kugombea nafasi yoyote katika uchaguzi ujao.

Walikitaka chama hicho kuwaelekeza viongozi wake, umuhimu wa kuzingatia maadili na nidhamu kwa kutumia vikao kuwasilisha hoja zao, na si kutumia matamko kukidhoofisha na kujijengea umaarufu binafsi.

Kutokana na utekelezaji wa azimio hilo, jana Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Tabora, Robert Kamoga, alitangaza kuwa wamemvua Sitta ulezi wa UVCCM Mkoa kutokana na kuendelea kutoa kauli licha ya azimio hilo. Sitta ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki mkoani humo, anadaiwa kuponzwa na kauli aliyoitoa na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari jana, akisema UVCCM inateswa na siasa za makundi na kuitaka itumie muda wake mwingi kutatua matatizo yake.

"Sasa tukianza kulumbana hapa, tutakuwa tunadhihirisha siasa za makundi. Kwa sababu kuna kauli ambazo ukiziangalia, unajua kabisa hizi zinatokana na kuteswa na siasa za makundi tu na hakuna jambo lingine," Sitta alikaririwa akisema jana akiwa jimboni kwake Urambo.
"Tumemsikia Sitta akisema vijana tuna matatizo … kwa hiyo hatuwezi kukaa na walezi wenye matatizo. Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa imekaa kikao cha dharura leo (jana) asubuhi, na kuamua kumvua nafasi yake ya Mlezi wa Vijana wa Mkoa," alisema Kamoga.

Katika mazungumzo yake kwa simu na gazeti hili, Kamoga alisema kutokana na hatua hiyo, wanapeleka taarifa yao kwa uongozi wa UVCCM Taifa kwa hatua zaidi za utekelezaji, lakini wameona ni vyema kuanza kutekeleza kwa vitendo Azimio la Dodoma, kwa sababu wanaamini Sitta ni mtu mwenye akili timamu.

"Tunaamini Mheshimiwa Sitta atatuelewa katika uamuzi huu, kwa sababu hawezi kuongoza watu wasio na akili. Tunaamini mchango wake unatosha sasa, kwa sababu kama ana jambo, alipaswa kulieleza katika vikao husika. Kwa hiyo, tunatekeleza Azimio la Baraza Kuu la kutaka viongozi watumie vikao kuzungumzia masuala ya chama," alifafanua Mwenyekiti huyo wa UVCCM.

Sitta amekuwa Mlezi wa Vijana wa Mkoa wa Tabora tangu mwaka 2003 na muda wake ulimalizika mwaka 2008, lakini uongozi mpya wa Vijana wa Mkoa ulipoingia madarakani, uliamua aendelee na wadhifa huo kwa kipindi kingine cha miaka mitano ambacho kingemalizika 2013.

Katika siku za karibuni, kabla ya kikao chake cha mwishoni mwa wiki Dodoma, viongozi wa UVCCM ‘waliwashambulia' viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwamo wastaafu kwa kile walichodai kutoa matamko yenye nia ya kukidhoofisha chama na kujitafutia umaarufu binafsi.

Miongoni mwa waliotajwa na UVCCM ni Sitta, na mawaziri wakuu wawili wa zamani, Frederick Sumaye na Edward Lowassa.

Mbali na Sitta, Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Mkoa wa Mara, Anthony Mtaka, naye amejikuta matatani baada ya kudaiwa kukiuka azimio hilo la Dodoma, kwa kuandika katika mtandao wa kijamii, Facebook, kuwa UVCCM inapaswa kwenda kunywa ‘kikombe' kwa ‘Babu wa Loliondo', kwa sababu imechoka.

Kwa upande wake, Sitta alisema hajapata taarifa za kuvuliwa nafasi hiyo na kusisitiza kuwa kama ndivyo hivyo, hakuna tatizo, yuko tayari kukubaliana na hali hiyo kutokana na kuwa na shughuli nyingi za kufanya.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu, alisema yeye ni mtu wa imani kubwa na hashangazwi na lolote, kwa kuwa dunia ya sasa imejaa mapambano na kwa kuwa ni mtu wa mapambano, uamuzi huo ni sawa tu.

"Kwanza nilishawahi kutishiwa kunyang'anywa uanachama wa CCM, Agosti mwaka jana, sina tatizo, ninaangalia tu hali kwani kama linatokea limepangwa na binadamu na nitayapokea kadri yatakavyokuja," alisema Sitta.

Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa, alisema uongozi wa UVCCM Taifa utajadili uamuzi huo wa Tabora na kauli ya Sitta na kutoa uamuzi wao kwa kuwa Sitta ni kiongozi wa kitaifa ndani ya chama, kwani ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Hata hivyo, Malisa katika mazungumzo yake kwa simu na gazeti hili, alifafanua kwamba wanachama wasitarajie, kwamba UVCCM itafanya uamuzi kinyume cha maazimio ya Dodoma.

Kuhusu uamuzi wa UVCCM Tabora kumvua Sitta ulezi, Malisa alisema uamuzi huo ni sahihi kwa kuwa wao ndio waliomteua katika nafasi hiyo na wana mamlaka ya kutengua uamuzi wao.

Akizungumzia kauli ya Mtaka kuwa umoja huo unatakiwa kupelekwa Loliondo kwa Babu, kwa kuwa umechoka, Malisa alisema Mtaka ni mjumbe halali wa Baraza hilo aliyekuwa Dodoma wakati wa maazimio hayo, hivyo pia watamjadili na kutoa uamuzi kuhusu kauli hiyo.

Source: Habari Leo
 
Nilijuwa tu lazima itakuwa hivi...Maana hivi juzi kati hapa huyu Sitta alitaka kuonana na mkuru lakini mambo hayakuwa vizuri huko ndani........
 
Back
Top Bottom