MGOGORO: Malumbano ya UVCCM, Viongozi wastaafu na Hatima ya CCM

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umetangaza kuunda kamati maalumu ili kufanya mageuzi ndani ya umoja huo na kumuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Rais Jakaya Kikwete kwa kujivua gamba na kubadili mtazamo na kukidhi matarajio ya
wengi.

Aidha, umesema utahakikisha viongozi wa chama hicho wanaotoa matamko bila kufuata utaratibu, hawapati nafasi yoyote ya uongozi na chama kisiwateue kugombea nafasi yoyote katika uchaguzi ujao.

Wamekitaka chama hicho kuwaelekeza viongozi wake umuhimu wa kuzingatia maadili na nidhamu kwa kutumia vikao kuwasilisha hoja zao na si kutumia matamko kukidhoofisha na kujijengea umaarufu binafsi.


Aidha, wameitaka CCM kufanya semina elekezi kwa mawaziri na wakuu wa mikoa na wilaya baada ya kuteuliwa ili watambue dhamana na uhusiano wao na chama hicho na malengo na matarajio ya chama kutoka kwa wananchi.

Akisoma maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la UVCCM Taifa mjini Dodoma, Kaimu Mwenyekiti wa Umoja huo, Beno Malisa, mbali na kuunga mkono dhamira ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete ya kutaka CCM ijivue gamba, vijana hao walisema hata UVCCM inapaswa kujivua gamba.

Katika maazimio hayo, likiwemo la kumpongeza Rais Kikwete kwa kudhamiria kufanya mageuzi katika chama hicho kwa lengo la kukihuisha na kukirudishia mvuto kwa wanachama na wananchi hususani vijana, UVCCM wameona na umoja huo unahitaji kubadilika na kukidhi mahitaji hasa.

Malisa alifafanua kuwa kikao hicho kilichokutana Dodoma, kimeona kuwa umoja huo unahitaji kubadilika katika eneo la uanachama, uongozi, muundo, itikadi, uimarishaji wa uchumi, maadili na utendaji.

Ili kutekeleza dhamira hiyo ya kujivua gamba kama walivyosema, umoja huo umeunda kamati maalumu itakayofanya uchambuzi yakinifu wa namna ya kufanya mageuzi hayo chini ya uenyekiti wa kada wa umoja huo, Mohamed Bashe.

Baada ya kumaliza uchambuzi huo, kamati hiyo yenye wajumbe wengine sita, itawasilisha maoni na mapendekezo hayo katika vikao vya maamuzi, Baraza Kuu la UVCCM.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Riziki Pembe ambaye ni Mjumbe kutoka UVCCM Zanzibar, Fadhili Njagilo Mwenyekiti Vijana Iringa, Rojas Shemwele Mjumbe wa UVCCM Tanga, Daud Ismail kutoka UVCCM Zanzibar, Ashura Shengondo kutoka UVCCM Bara na Anthon Mavunde kutoka UVCCM Bara.

Mbali na kujivua gamba, Baraza hilo pia limelaani maandamano ya Chadema na walichoita kitendo cha viongozi wachovu wa Chadema kuendeleza chuki dhidi ya Serikali halali ya CCM.

Katika maazimio hayo, Baraza hilo limedai kubaini hila na njama zinapangwa dhidi ya Serikali na kuwataka vijana wote wa CCM na Watanzania kwa ujumla kukiogopa chama hicho cha Chadema.

Aidha, limewataka wanachama wote wa UVCCM kuwa tayari kukabiliana na njama hizo. Kuhusu tathimini ya uchaguzi uliopita, Baraza hilo limempongeza Rais Kikwete na Rais wa
Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kushika nafasi hizo, lakini limekishauri chama hicho kutazama upya mfumo wa kura za maoni wa kupata wagombea.

Mbali na mfumo huo, Baraza hilo pia limetaka chama hicho kitazame upya mfumo wa utoaji kadi za wanachama wakati wa uchaguzi wa wagombea na kuepuka makosa yaliyojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Kutokana na ushindi huo wa 2010, baraza hilo limeandaa mkakati wa kwenda kuwashukuru wananchi na vijana kwa kukipigia kura na limeagiza viongozi wote wa UVCCM kuhakikisha wanafanya mikutano na ikibidi maandamano ya kuwashukuru Watanzania kwa kukichagua CCM.

Baraza hilo pia lilijadili changamoto zinazojitokeza serikalini na zinazojitokeza kwa vijana na kutoa baadhi ya maagizo ya kufanyiwa kazi na Serikali.

Katika maagizo hayo, lipo la kutaka Serikali kuchunguza sababu za kupungua kwa ari ya baadhi ya watendaji wa Serikali katika kutimiza wajibu wao.

Hali waliyosema imeendelea kuwakatisha tamaa wananchi na hata wanaCCM na hivyo kujenga chuki dhidi ya Serikali halali ya CCM.
HABARI LEO
 
UVCCM kupambana na kina Sitta, Sumaye na Lowassa

Baraza Kuu UVCCM lawaka moto Dodoma


Mbunge amwaga mamilioni
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mbunge wa Viti Maalumu kundi la Vijana, Catherine Magige, jana alimwaga mamilioni ya fedha akitoa Sh50,000 kwa kila mjumbe wa Baraza hilo, akisema kuwa ilikuwa ni ya kuwapa chakula cha mchana.


Agenda zawa siri

Katika hatua nyingine, jana waandishi wa habari waligonga ukuta walipotaka kujua ajenda za mkutano huo baada ya kuelezwa kuwa uongozi hautaweza kuwapa ajenda hizo, badala yake wanawaweza kupewa vitu vingine ikiwemo ratiba.


sasa hapa wanaenda mbali, yani na shida za wananchi, hawa jamaa na posho za vikao bado wanapeana 50,000 kila mmoja kama hela ya chakula cha mchana TU.....hii ni kuonyesha jinsi gani wanajijali wao wenyewe, ukiangalia kwa undani (labda kama muandishi wa hii habari alikua anawakandamiza UVCCM) hawajagusia mambo ya msingi yanayo sumbua na wananchi na taifa kwa ujimla. wameishia kugombana na kuzumngumzia namna ya wao kuendelea kushikilia madaraka....
 
I dont know how sustainable hili tamko litakua kwani CCM wanatabia ya kusema kitu kingine na kufanya kingine

Haya tuone....
 
Samahani hii kidogo ,hivi ni huyu huyu bashe tunayemjuwa ndio anaongoza hii kamati mupya?
 
KUJIVUA GAMBA HAKUTAWASAIDIA WAO UVCCM WALA BABA/MAMA SAO CCM!!!!Huu wanaofanya ni usanii tu.
Principle ya nyoka kujivua gamba ni sawa na kubadilisha vazi(kanzu/shati/msuli n.k). Nyoka ANABAKI YULEYULE whether ni cobra mwenye sumu kali au nyoka yoyote kama koboko,kifutu n.k.

Ndicho wanachofanya UVCCM na watakavofanya baba zao CCM.Watabadilisha mavazi lakini ni walewale CCM/UVCCM MAFISADI,WANAFIKI,WAONGO NA WABABAISHAJI.

Tanzania inahitaji mabadiliko kamili, A COMPLETE CHANGE kwa maana ya KU-OVERHAUL THE WHOLE GOVERNMEMNT SYSTEM NA KUWEKA SERIKALI MPYA ITAKAYOONGOZWA NA CHAMA TOFAUTI NA CCM.
 
vijana msilale lale x2 vijana msilale bado mapambano, vijana wenzangu ni wakati wamabadiliko watake wasitake .honest speaking kuwa kijana kuwepo ccm unaona viongozi wako wanavyoprove failure wanagombania madaraka na wewe unaendelea kuwa support ni ufinyu wa mawazo inafahamika wazi vijana wengi walio ccm wanafuata maslahi zaidi they see kuwa ccm ni njia mbadala ya matatizo yao(ukosefu wa ajira, wanavyuo fedha za kujikimu) wakati we need INFINITE SOLUTION LA TATIZO NA INFINITE SOLUTION N MABADILIKO KWENYE MFUMO MZIMA
JAMANI TUKO DUNIANI NYINGINE
 
Hawa UVCCM na CCM wenyewe wanashangaza sana. Huyu Bashe si ndo huyu aliyetaka kugombea ubunge nzega wakasema siyo raia??!! Makamba akasema wanamvua uanachama, wanamvuoa nyadhifa zote ndani ya CCM.

Ni huyu huyu leo kateuliwa na uvccm kuongoza hiyo tume, keshakuwa clean kiasi hicho??. Ama kweli kwenye siasa za CCM usipokuwa mnafiki utaonekana hufai. Haya yetu macho na hilo zoezi la kujivua gamba. Mimi nilidhani wana-flush akili zao, kumbe wanajivua gamba ili waje na kasi mpya, lakini ni wale wale. Tumewasoma.
 
mohamad bashe!!!!!!!!!!!!!! hussein bashe!!!!!!!!!!!!!!!!!! au? napata kizunguzungu kidogo. hawa ni ndugu au? majibu yatakuja coz coz tuna great thinkers jamvini.
 
Hii ni episode mpya na itakuwa na kisasi..ndani yake kwa waliomtamka kuwa sio raia....tusubiri mwanzo mwisho wa episode
 
Gamba lipi wanalojivua!!?? CCM yenyewe ndo gamba tunalopigana watz kuliondosha tukiongozwa na hiyo chadema mnayoilaani. Haki ya nani sasa ni dhahili mwisho wenu umefika, kamati ya kujivua gamba inaongozwa na msomali!!!!
 
Sina hakika Kama hii kamati inanguvu ya kuwashughulikia the so called "wabomoa chamA cha mApinduzi isije ikawa ni mbinu ya kuwasafisha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom