MGOGORO: Malumbano ya UVCCM, Viongozi wastaafu na Hatima ya CCM

Niliona kidogo jamaa (yule mdogo mdogo) yuko poa, ila muda ule ule Aljazeera walikua wanaonesha kichapo alichokula Ghadafi and was more interesting kuliko hizi siasa za CCM, yule bwanasijui anaitwa mwakayii(wa je tutafika?) ukimsikiliza vizuri utagundua ana uCCM mwingi sana ndani yake
 
<p>
It's another political blow, many more to come..
</p>
<p>&nbsp;</p>
Kumbe mtu makini na principled kama Sitta alikuwa mlezi wa UVCCM, kijiwe cha vijana wachovu wa fikra na mwelekeo ambao akili yao yote iko kwenye "mshiko" anaotoa Rostam na Lowassa? Nani hajui kuwa UVCCM wamefilisika kisiasa, hivyo wanawagwaywa vijana wenzao wa CHADEMA na kuishia kuhangaika na akina Sitta? Nani mwenye imani na UVCCM inayotawaliwa na mawazo ya raia wa Somalia, Bashe? Sitta jisikie huru kuondoka huko!
 
UVCCM ni kikundi cha wahuni.mtu kama sitta hawezi kuwalea.hao wanahitaji mtu kama lowassa,rostam chenge au tambwe hiza.
 
Si UVCCM bali ni RIZ 1 kwani umoja huu ni photocopy ya huyo mtu akiamua anaweza ata akawapa mabomu wajilipue
 
Umoja wa vilaza wa chama cha mapinduzi hauwezi kuendana na fikra elekezi na endelevu ka za mzee sita.wao waendelee tu kuwa chini ya hao mafisadi papa na si kwa mzee mwenye msimamo ka sita.
 
Mimi namwaona Mh. Sita kama Baba Mzazi na UVCCM-Tabora kama watoto wake. Sasa swali langu kwa UVCCM-Tabora ni kwamba ukimkosea mzazi wako akakuonya na kukusema unamwambia kuanzia leo wewe sio mzazi wangu, halafu unaenda kumtafuta mzazi mwngine ambaye ukikosea anaona kawaida tu? Wakumbuke kuwa wao kama vijana wanatarajia kuwa viongozi siku sijazo, hawataki kukosolewa ni aina gani hiyo ya viongozi wajao. HALAFU SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI, WATAKUNJIKA HAO WAKISHA KUWA WAKAVU? (WAKUBWA)?
 
UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umeanza kutekeleza kwa vitendo azimio lake la kuahidi kupambana na viongozi wa chama hicho wanaodaiwa kutoa matamko bila kufuata utaratibu, kwa kutangaza kumvua nafasi ya ulezi wa UVCCM Mkoa wa Tabora, Spika wa zamani, Samuel Sitta.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Baraza Kuu la UVCCM, lilitangaza baada ya kikao chake Dodoma, kuwa katika kukabiliana na viongozi hao, litahakikisha viongozi wa CCM wanaotoa matamko bila kufuata utaratibu, hawapati nafasi yoyote ya uongozi na chama kisiwateue kugombea nafasi yoyote katika uchaguzi ujao.

Walikitaka chama hicho kuwaelekeza viongozi wake, umuhimu wa kuzingatia maadili na nidhamu kwa kutumia vikao kuwasilisha hoja zao, na si kutumia matamko kukidhoofisha na kujijengea umaarufu binafsi.

Kutokana na utekelezaji wa azimio hilo, jana Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Tabora, Robert Kamoga, alitangaza kuwa wamemvua Sitta ulezi wa UVCCM Mkoa kutokana na kuendelea kutoa kauli licha ya azimio hilo. Sitta ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki mkoani humo, anadaiwa kuponzwa na kauli aliyoitoa na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari jana, akisema UVCCM inateswa na siasa za makundi na kuitaka itumie muda wake mwingi kutatua matatizo yake.
“Sasa tukianza kulumbana hapa, tutakuwa tunadhihirisha siasa za makundi. Kwa sababu kuna kauli ambazo ukiziangalia, unajua kabisa hizi zinatokana na kuteswa na siasa za makundi tu na hakuna jambo lingine,” Sitta alikaririwa akisema jana akiwa jimboni kwake Urambo.
“Tumemsikia Sitta akisema vijana tuna matatizo … kwa hiyo hatuwezi kukaa na walezi wenye matatizo. Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa imekaa kikao cha dharura leo (jana) asubuhi, na kuamua kumvua nafasi yake ya Mlezi wa Vijana wa Mkoa,” alisema Kamoga.

Katika mazungumzo yake kwa simu na gazeti hili, Kamoga alisema kutokana na hatua hiyo, wanapeleka taarifa yao kwa uongozi wa UVCCM Taifa kwa hatua zaidi za utekelezaji, lakini wameona ni vyema kuanza kutekeleza kwa vitendo Azimio la Dodoma, kwa sababu wanaamini Sitta ni mtu mwenye akili timamu.

“Tunaamini Mheshimiwa Sitta atatuelewa katika uamuzi huu, kwa sababu hawezi kuongoza watu wasio na akili. Tunaamini mchango wake unatosha sasa, kwa sababu kama ana jambo, alipaswa kulieleza katika vikao husika. Kwa hiyo, tunatekeleza Azimio la Baraza Kuu la kutaka viongozi watumie vikao kuzungumzia masuala ya chama,” alifafanua Mwenyekiti huyo wa UVCCM.

Sitta amekuwa Mlezi wa Vijana wa Mkoa wa Tabora tangu mwaka 2003 na muda wake ulimalizika mwaka 2008, lakini uongozi mpya wa Vijana wa Mkoa ulipoingia madarakani, uliamua aendelee na wadhifa huo kwa kipindi kingine cha miaka mitano ambacho kingemalizika 2013.

Katika siku za karibuni, kabla ya kikao chake cha mwishoni mwa wiki Dodoma, viongozi wa UVCCM ‘waliwashambulia’ viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwamo wastaafu kwa kile walichodai kutoa matamko yenye nia ya kukidhoofisha chama na kujitafutia umaarufu binafsi.

Miongoni mwa waliotajwa na UVCCM ni Sitta, na mawaziri wakuu wawili wa zamani, Frederick Sumaye na Edward Lowassa.

Mbali na Sitta, Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Mkoa wa Mara, Anthony Mtaka, naye amejikuta matatani baada ya kudaiwa kukiuka azimio hilo la Dodoma, kwa kuandika katika mtandao wa kijamii, Facebook, kuwa UVCCM inapaswa kwenda kunywa ‘kikombe’ kwa ‘Babu wa Loliondo’, kwa sababu imechoka.

Kwa upande wake, Sitta alisema hajapata taarifa za kuvuliwa nafasi hiyo na kusisitiza kuwa kama ndivyo hivyo, hakuna tatizo, yuko tayari kukubaliana na hali hiyo kutokana na kuwa na shughuli nyingi za kufanya.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu, alisema yeye ni mtu wa imani kubwa na hashangazwi na lolote, kwa kuwa dunia ya sasa imejaa mapambano na kwa kuwa ni mtu wa mapambano, uamuzi huo ni sawa tu.

“Kwanza nilishawahi kutishiwa kunyang’anywa uanachama wa CCM, Agosti mwaka jana, sina tatizo, ninaangalia tu hali kwani kama linatokea limepangwa na binadamu na nitayapokea kadri yatakavyokuja,” alisema Sitta.

Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa, alisema uongozi wa UVCCM Taifa utajadili uamuzi huo wa Tabora na kauli ya Sitta na kutoa uamuzi wao kwa kuwa Sitta ni kiongozi wa kitaifa ndani ya chama, kwani ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Hata hivyo, Malisa katika mazungumzo yake kwa simu na gazeti hili, alifafanua kwamba wanachama wasitarajie, kwamba UVCCM itafanya uamuzi kinyume cha maazimio ya Dodoma.

Kuhusu uamuzi wa UVCCM Tabora kumvua Sitta ulezi, Malisa alisema uamuzi huo ni sahihi kwa kuwa wao ndio waliomteua katika nafasi hiyo na wana mamlaka ya kutengua uamuzi wao.

Akizungumzia kauli ya Mtaka kuwa umoja huo unatakiwa kupelekwa Loliondo kwa Babu, kwa kuwa umechoka, Malisa alisema Mtaka ni mjumbe halali wa Baraza hilo aliyekuwa Dodoma wakati wa maazimio hayo, hivyo pia watamjadili na kutoa uamuzi kuhusu kauli hiyo.
 
ALISEMA PIA HAWA WANAOJIITA UVCC WAMEKOSA MAADILI YA KITANZANIA ALIFANYA REFERENCE YA TAMKO LAO LA KIPUUZI WALILOMTUKANA SANA DR SLAA NA AKASEMA KAMA WANAWAWAKILISHA VIJANA WA KITANZANIA HAYA SIYO MAADILI YETU,HATA KAMA NI SIASA HUWEZI KUMTUKANA BABA YAKO KWA KUWA YUKO CHAMA KINGINE

NI KWELI DOGO YUKO VIZURI NA NINAFIKIRI SIO CHADEMA KWANI ALISEMA YEYE ANACHAGUA PAKA ANAYEWEZA KUKAMATA PANYA HAIJALISHI RANGI WALA UMBO LA HUYO PAKA

hongerz sana SABATO kama hujajiunga CHADEMA kuna kadi yako ninayo niPM
 
System kubwa ikioza hata suasystem nayo huoza,hakika huu uozo,kuna rafik yangu moja yumo ndan ya uvccm kashiriki vikao dodoma,lakn kanambia yanayofanyika huko ni those wth power to clear paths to their people.inasikitsha but thats the reality.
 
Ni vizuri; itazidi kumthibitishia kuwa huko aliko siko!!

anza kufanya nae mazungumzo kuna vijana wengi muda si mrefu watakimbia chama kwa pamoja na kuna mawaziri takribani 5 wanahitaji sababu tu za kutoka kwao kwahiyo usilale mazungumzo yaanze ni kipindi kizuri zaidi cha kujijenga
 
Mlezi akisema una matatizo unamkataa....sasa maana ya kuwa mlezi ni nini? Awe anakusifia hata ukikosea? Hutaki aseme kwa sauti, unataka akunong'oneze!
 
Hata mimi alinigusa, sidhani kama uvccm watakua na ujasiri wa kujibu hata moja ya hoja zake, siamini hivyo
 
Mzee six, hao watoto uvisisiem hawana adabu na walikuwa wanakuona kama baba wa kambo ambaye analea watoto wasio wa kwake na wakikua na kupata maarifa wanaanza kumkataa.
 
Kwa muda mrefu nimefuatilia kauli na matamko yanayotolewa na Uongozi wa UVCCM, inavyoelekea hawa jamaa hawako sawa kiakili, kimaadili n.k. Kauli wanazozitoa ni ishara tosha kuwa umoja huu sasa unashida. Sijajua tatizo lao hasa ni nini, maana tunachoshuhudia sasa hivi ni mambo ya kihuni ambayo ni tofauti kabisa na aina ya umoja wa vijana tuliokuwa tunaufahamu.

UVCCM ya akina Guninita sio hii, na kama hali hii itaendelea na CCM taifa itaendelea kuwavumilia na kuwastahi kwa sababu zozote zile naamini watakuja kujuta. UVCCM sasa agenda yao kubwa ni kuwatusi na kuwavunjia heshima viongozi au watu waliokuwa viongozi wa CCM, vijana hawa ambao naamini kuna aliyewatuma, hawataki mtu yeyote atoe tamko linalokikosoa chama. Hali hii itasababisha uhasama kati ya wanachama hivyo kusababisha makundi ambayo yatasababisha uadui kati ya wanachama. Hii ni hatari maana ikitokea hivyo huenda ndiyo dalili za mwisho wa CCM. Mara kadhaa nimesikia matamko yakidai CHADEMA wanaleta chokochoko ili kuvuruga amani ya Tanzania, hii sio kweli!! Mimi nadhani kama CCM kinataka amani ya kweli ndani ya CCM yenyewe na taifa kwa ujumla lazima wao wenyewe waonyeshe mashikamano wa hali ya juu, hizi chokochoko za UVCCM ni dalili mbaya ya uvunjifu wa amani ya Taifa kwani inavyoelekea vijana hawa sasa hivi wametumwa ili kukivuruga chama na wanachama, kujenga uadui ndani ya chama na nje ya chama.

Nafikiri wakati umefika sasa kwa CCM kuwa adibisha hawa watoto ambao wanaleta utamaduni ambao sio tabia ya ccm, hakuna sababu ya kuwa na umoja wa aina hii hivyo ni lazima kamati kuu ya ccm itakapo kaa iwape onyo kali wahuni hawa hata ikibidi kuwafukuza uanachama. Vinginevyo CCM itajuta kuwa na UVCCM ya aina hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom