MGOGORO: Malumbano ya UVCCM, Viongozi wastaafu na Hatima ya CCM

mleta hoja na huyo makonda wote hawaeleweki

Hivi UVCCM na "issues" zao zote hizo wanadhani kuna mtu hata anawajali?? I would rather watch cartoon network kuliko kupoteza muda na makonda
 
Matamshi ya UVCCM ya kuwashambulia waasisi wa chama hicho ni ya kujiamini na bila kukemewa na mwenyekiti wala katibu mkuu wa CCM.Mbona hayati baba wa taifa alikuwa akiwaita waandishi wa habari na kueleza kinacho mkera na hawakuthubutu kumkemea.Au sasa hakuna tena mtu au muasisi wa CCM anayeheshimika nchini?
 
Habari ya wametumwa na wakubwa sio jambo la kuuliza ni la wazi kabisa,, na kitendo cha baadhi ya viongozi walioko madarakani kusema eti vijana wana uhuru wa kutoa maoni yao ni wazi kabisa wanatekeleza tu maagizo kutoka kwa wakubwa. Cha kushangaza eti vijana wana uhuru wa kutoa mawazo yao, ila kina Sumaye na wengine kama Sita wakitaka kusema wamfuate raisi ama watumie vikao vya chama... Haiingii akilini na inaboa... wanataka kuficha nini??? Serikali hii imejaa visasi, chuki, ufisadi na uchafu mwiiiiingi!!
 
Umesema kweli kabisa na sasa wasome alama za nyakati kuwa watanzania hawadanganyiki.
 
Nimesoma mara tatu lakini sielewi! Naona nimeanza kupoteza uwezo wa kuelewa. Ngoja nijiandae na safari ya kwa babu
MJUE PAULO MAKONDA ( PART 2A):teeth:
Nawashukuru sana wachangiaji wa JF,maana hii ni demokrasia mpaka hapa nimeelewa kuwa wachangiaji tupo pamoja katika kuboresha.

Kama nilvyosema kuwa, katika medani ya siasa ni lazima uwe makini sana katika uchambuzi na sio kujitokeza na kusema,kwa maana kuwa"Kijana huyu alisema kuwa SEKRETARIETI YA UVCCM TAIFA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI IJIUZULU"………………Hapa kiuhalisia ni kuwa kada huyu bado ni mchanga wa siasa kwani bado anachanganya mambo kwani UVCCM inaongozwa na kanuni moja ambayo imewekewa ibara ya kwanza hadi mwisho, pia katika UVCCM kunatoa wajumbe kwenda sekretariet ya CCM Taifa,yaani katibu Mkuu wa UVCCM au Naibu Katibu Mkuu, si kweli kuwa sekretariet ipo kwenye structure ya UVCCM au UVCCM ina kamati ya utekelezaji kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa ambayo inaongoza mipango ya jumuiya hiyo ya kila siku

Pia kamati ya utekelezaji hupendekezwa na wajumbe wa baraza hilo la Taifa na si kata, iweje leo mjumbe wa mkutano mkuu toka kata CCM kwenda Wilaya aje na maamuzi haya?bila yeye kupitia vikao vyake vya kata?.mbona wajumbe wa kata hawana taarifa?.

Halafu ujumbe wa kata yake haujathibitishwa,binafsi ninamshauri kuwa kama ngazi ya kata inaweza kushinikiza Taifa,hii ni hatari!wajumbe wa kata zote Tanzania wenye nafasi kama yake,wakitoa matamko kama yake,ina tija kwa taifa?

Lengo si kumuumbua,ni kumshauri tu kuwa CCM ina vijana wa aina zote,yeye asitake kuburuza watu kwa maandalizi yake ya Uenyekiti wa UVCCM Taifa.

Binafsi nadhani kuwa, kwakuwa amekiuka kanuni za chama kama wenzake za kuongelea kwenye media,naye ajiuzulu!.nani msemaji wa kata yake ya Rau? Kada huyu amepotoka.

Paul makonda anaposema kuwa wale wanatetewa na mafisadi,je,ana uthibitisho gani kuwa ni kweli?kama naye hakuwa mmoja wa kundi la mafisadi hao. Anataka kuuaminisha umma kuwa wale wanaomsomesha na kumfadhili wamemtuma?Nina ushahidi wa kutosha kuwa anatumika kupitia matamko yake.

MAMBO MAZURI ALIYOWAHI KUFANYA PAULO MAKONDA
Bila kusema yaliyopo,kijana huyu aliwahi kuandaa makongamano ya dini na kualika wanaomfadhili waongee na jamii katika maandalizi ya urais wa mwaka 2015,hasa Moshi-Ushirika,Institute of Social Work pamoja na Stefano Moshi University.

Aliweza kuwa mchapakazi katika mambo ya jamii hali hata asipotumwa,ni dhahiri kuwa akishauriwa na akashaurika atakuwa kijana safi kwa miaka ijayo nje ya jumuia na chama tawala.Aache kutumika vibaya na kujitafutia maadui katika jamii.

MIPANGO YAKE YA MUDA MREFU.
Kutumia media kujitangaza ili kutimiza ndoto zake za kisiasa UVCCM, na kiuchumi katika kuelekea urais wa mwaka 2015-2025.Niseme kuwa atafute njia mbadala ya kuwahudumia watanzani kwani hana uwezo katika nyanja ya siasa na uongozi.

"kila kijana anaweza kuwa na urafiki au undugu na kiongozi yeyote wa kitaifa,tusifike mahali tukawa mbuzi wa kafara kwa maslahi ya viongozi hawa……….":panda:
 
Vijana tusiige siasa zisizo na tija. Pamoja na kuandika hoja hii kwa kirefu mimi kama kijana bado sikuungi mkono wala siungi uongozi wa UVCCM kwa mambo ambayo wanayatamka na kuyashikia bango. kinachoendelea UVCCM hakina tofauti na mambo ya kiswahili ya kuzodoana na kubwatizana mitaani. Haiwezekani waendelee kukiharibu chama na kukifanya kipoteze heshima iliyokuwa imejiwekea. Nashangazwa sana na watu wanaounga mkono matamshi ya hovyo yanayotolewa na umoja wa vijana. kwa mtu yeyote mwenye hekima haya ni mambo ya kukemea si vinginevyo!!!!!!
 
UVCCM chini ya makamu mwenyekiti wao walikuja na siasa za kujibu,wakawajibu Fredrick Sumaye na Samwel Sitta . Hatua hii ya kujititimua kuwajibu sio tu kwamba imewashushia hadhi yao bali pia imewafanya wakaonekana wakosaji mbele ya Wana CCM wenzao na watanzania kwa ujumla ambao bado wanawapa heshima ya Juu ndugu hawa wawili.

Kimaro aliekuwa mbunge wa Vunjo alisema ' Hao UVCCM wanasimamia umoja wa vijana gani wakati vijana wote walishaenda CHADEMA? huku UVCCM wenyewe wakiwaangalia bila kuwa na cha kuwafanya.waache kumtafuta mchawi ni nani kwani mchawi ni wao wenyewe - akawahimiza kuja na mikakati badala ya kuwa na matamko ambayo sikwamba tu hayana tija bali yanabomoa hadhi yao mbele ya Jamii .

Mheshimiwa Samwel Sitta ameongoza bunge la 9 kwa uzalendo mkubwa .Wabunge walipata kujadili mijadala ya msingi ikiwemo mkataba wa kisanii wa RichMond .Leo hii ni aibu kwa UVCCM kujaribu kupambana na Sitta. Wanasahau Heshima ya Sitta mbele ya jamii ni kubwa kuliko ya huo umoja wao .

Waendelee kutoa matamko,CHADEMA wao wanamkakati na kwa sasa karibu vyuo vikuu vyote wana matawi yaliyo hai . Wasomi hawa watakapoenda vijijini mwao watakuwa mabalozi wakubwa kwa sera za chama chao . Hapa ndipo tofauti itakapoonekana kwani kuna tofauti kubwa sana kati ya fikra hai na fikra mfu.
 
vile vitoto vya UVCCM havina adabu hata kidogo. vimerithi tabia hii kutoka kwa baba zao Umoja wa Wazee wa CCM (UWCCM).
 
A Chama Cha Mapinduzi (CCM) youth wing (UVCCM) National Executive Council member Mrisho Gambo has been removed from his post as member of the UVCCM executive council in Arusha District over allegations of sabotaging his party during last year's election campaigns.
The decision was reached by the UVCCM regional executive council, which met in Longido District. It was also proposed that Gambo be relieved of other ranks he is holding.
A meeting in which 32 members out of 54 participated strongly condemned a statement issued by the UVCCM’s regional administration in relation to statements issued by retired top government officials.
The statement was read by Arusha regional UVCCM chairperson James Ole Millya, who said the meeting unanimously reached the decision after being satisfied with the evidence to prove the allegations.
Signs that Gumbo could face such measures were apparent much earlier even before the meeting started, particularly from a section of UVCCM members who seemed to have a different stance from the party's.
Gambo was accused of spreading scandalous information against CCM contestant for Arusha constituency Dr Batild Buriani, who lost to Chadema’s Godbless Lema.
It was said that among the evidence provided included harsh words that Gambo uttered against the contestant, making statements in public that he would not cast his vote in favour of Dr Buriani or participate in campaigning for her.
Millya insisted the meeting had the party’s constitutional mandate to do what they did adding that UVCCM had also written to higher organs at national level so that they would take a similar action if he held other positions.
“We have lost confidence in him, we cannot allow a snake among us. We are preparing a letter that will be sent to higher leaders within UVCCM,” said Millya. He noted that the party would get rid of all members, who happened to be double-crossers, adding that if they wanted to join opposition parties, then they should do so.
Commenting on that issue by phone, Gumbo said he would never entertain hypocrisy, arguing that since some party members entertained hypocrisy, it was losing people’s confidence.
“Our party constitution states very clearly that I will only say the truth and never instigate chaos. I personally will not do things just to satisfy my own tummy and I’ll always use my rational thinking,” he said.
He said he was planning to convene a press conference on Thursday and would explain his position.
He claimed that due to this influence, four members of the Wing’s meeting (names withheld) met at Mount Meru Hotel on Sunday night and prepared a statement, which he claimed was leaked even before the meeting.

SOURCE: THE GUARDIAN
 
The episode is just beginning!
uNKNOWINGLY THAT BY DOING SO, they are fueling the wave of change!
 
no one is clean..so far youths dnt loose your courage, UVCC/CCM belong to 'whales' and quiet obviously you wont survive there ...unless otherwise CDM is/becomes your HOST !..are you there??
 
WAKATI mpasuko ukionekana kuongezeka ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na viongozi wastaafu, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa ,amesema haoni tatizo lolote.
Akizungumza kwa simu kutoka jijini Nairobi, Kenya jana, Msekwa alisema wanaoona kuna mgogoro kati ya UVCCM na wastaafu, hayo ni maoni yao.

“Hayo ni yako, hayo ni yako, hakuna malumbano ndani ya UVCCM na chama. Kwa heri," alisema Msekwa.
Kauli ya Msekwa imekuja wakati kuna kila dalili ya tofauti za kimtazamo ndani ya UVCCM, kuhusu kauli za Baraza la umoja huo dhidi ya viongozi wastaafu.

Wakati huohuo, kada wa zamani wa CCM sasa Mbunge Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda, amefananisha malumbano ndani ya chama tawala na maisha ya mbwamwitu porini, ambao kila mmoja hujifuta damu asionekane kama kala mzoga.

Shibuda alirusha kombora hilo kipindi ambacho CCM imejikuta kwenye malumbano kati ya vigogo wake na UVCCM.
"Nimekaa CCM miaka 43. Sikuwa napenda iondoke madarakani, lakini sasa lazima Watanzania wafikirie chama mbadala," alisema.

Shibuda bingwa wa kutumia tamathali za semi kwenye mazungumzo yake, alisema CCM hivi sasa ni sawa na pori la mbwamwitu ambalo kila mmoja hujaribu kujipangusa damu ili asijulikane madhambi yake.
Alifafanua kwamba vijana wa chama hicho, nao wamekuwa vibaraka wa makundi kwa kutaka maisha bora na kusahau mbele watakuwa watwana zaidi.

"CCM ya sasa haimtetei mnyonge, vijana ambao wakati wa Tanu walikuwa na msimamo madhubuti kulinda maslahi ya taifa sasa wanashiriki kurejesha utwana kwa kuwa vibaraka wa makundi ya kisiasa," alisisitiza.

Mbunge huyo alisema umefika wakati Watanzania wanapaswa kutambua vyama vya siasa ambavyo ni Saccos na kampuni, vinavyofanya siasa kutafuta ruzuku na vile vinavyotetea maslahi ya jamii.

Shibuda alisema hali ilivyo sasa malumbano ndani ya CCM inaonyesha sehemu kubwa ni watu wanaopigania maslahi binafsi na kusahau wananchi.

Katika kuonyesha msisitizo, Shibuda aliweka bayana kwamba kutokana na malumbano hayo kati ya wazee na vijana, imeonyesha jinsi CCM ilivyotoka kwenye misingi yake iliyorithi kutoka Tanu, ndio maana rasilimali za nchi zinaporwa wao wanazozana.

Akijivunia rekodi yake ya ukada wa CCM tangu Tanu kwa miaka 43, Shibuda aliponda utaratibu wa vikao kushughulikia matatizo na watu wachafu ndani ya chama, kwani havina tija.

"Mimi nimekaa ndani ya CCM kwa miaka 43, mambo ya vikao nikupoteza muda tu. Ndio maana niliapa kutopeleka tatizo langu kwenye kikao chochote, kwani haviwezi kutenda haki," alisisiiza Shibuda.
SOSI: MWANANCHI
 
Umri unamsumbua huyo mzee... Anamdanganya nani? Hata mtoto wa primary analiona kama anabisha amuulize Lowassa watoto walivyo na vision now days, aliulizwa swali akashindwa kulijibu mpaka sasa hivi!
 
Umri unamsumbua huyo mzee... Anamdanganya nani? Hata mtoto wa primary analiona kama anabisha amuulize Lowassa watoto walivyo na vision now days, aliulizwa swali akashindwa kulijibu mpaka sasa hivi!

Uko sahihi mkuu si unaona Makonda alivyomtolea uvivu Lowasa huyu huyu kuwa hafai kuwa kiongozi wa umma...Vijana siku hizi wanadhubutu kusema bila woga ... (Ila sijajua kama hili la Makonda ni muendelezo wa vijana wa CCM kuwakosea heshima viongozi wa kuu wa Chama waliouanzisha 2011)...!
 
Karibu kwenye mjadala huu ambao unalenga kujitathimini kwa vijana juu ya heshima yao kwa wazee. Mjadala huu utakuwa unarejea matukio mbali mbali ambayo yamefanywa na vijana.Kuanza na naweka orodha a matukio ya wanasias vijana dhidi ya viongonzi wao.

Nitaanza kwa kutoa mifano:-

1. Mwampamba na Sonza walipokuwa Chadema walikuwa wanatuhumiwa kuwavunjia heshima viongozi (wazee wa chama) wa chama chao mitandaoni....na inasemakama mpaka sasa wanafanya hivyo.

2. Nape wa CCM inasemakana aliwahi kutoa kauli ya kuudhi na kuvunja heshima kwa wazee...kuwa wao wanasubiri kufa tu...!

3. Kijana (sina hakika kama ni mwanasiasa sana) aliwahi kumpiga kibao Mzee Mwinyi(Rais mstaafu) hadharani akipinga maelezo ya Mzee Mwinyi.

4. Vijana wa UVCCM waliwahi pia kuwatukana viongozi wa chama chao pia. Ushahidi huu hapa chini

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uvccm-viongozi-wastaafu-na-hatima-ya-ccm.html

5. Pia na Mbunge wa Arusha Mh. Lema naye inasemekana anawavunjia heshima wazee wa CCM

6. Serukamba Mbunge wa Kigoma aliwatukana wazee kwa vijana waliokuwa bungeni na waliokuwa wanasikiliza kupitia runinga na redio...pale alipotamka tusi kwa lugha a kiingereza.

7. Mh. Lissu aliwahi pia kutamka kuwa ...neno...SILLY....bungeni...hilo pia ni kuwa wavunjia heshima wazee kwa vijana...
8. mweshimiwa waziri Kijana Mkaa wa mia aliwahi kusema anaongea na mwenye mbwa wala haongei na mbwa...huko huko bungeni(kama nimekosea nisahihisheni).

8. Orodha ni ndefu....ila kabla sijahau pia...kuna na suala la Makonda, Paul kumkwida Jaji Warioba.

Sasa kwa matukio haya na mifano mingine....huko mitaani. Vijana tumeangukia/wameangukia wapi mpaka sasa wanasahau umuhimu wa utamaduni wetu watanzania wa kuwaheshimu wazee. Ni nini kifanyike ili kurudisha heshima ya vijana kwa wazee?

Karibu kwenye mjadala.

SOURCE:VIJANA NA HESHIMA KWA WAZEE: Tumebadili utamaduni wetu wa Kitanzania...!?
 
mh
Katibu Mkuu,
Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM),
Morogoro Road/Opposite to Lumumba street,
S.L.P 0000,
DAR ES SALAAM.

YAH:HATIMA YA UVCCM NA SIASA ZA CCM/TANZANIA.

Nimesoma habari mbali mbali kuhusu Maazimio ya kikao cha Baraza kuu la UVCCM wiki iliyopita mjini Dodoma,nina haya yafuatayo:-
1.Hivi Hussein Bashe ni mtu sahihi kwa sifa na uwezo wa kuisaidia UVCCM itimize majukumu yake kwa CCM na Watanzania? Hii ina maana mtu huyu awe mwenyekiti wa kamati ya kukusanya na kupendekeza Muundo na mahitaji ya UVCCM ya sasa na ijayo kufuatia kauli ya mhe.Rais kikwete kuwa CCM lazima ijivue Gamba ,UVCCM mnaona Hussein Bashe anaweza kusimamia mabadiliko tarajiwa? Biashara na Siasa zitenganishwe UVCCM, pia Wasomali hawawezi kutusaidia kuiendeleza nchi yetu; vinginevyo UVCCM ibinafishwe kwa wageni kama viongozi wa sasa mmeshindwa.
2.UVCCM kuweni mbele katika hoja nzito za kitaifa badala ya kutaka kuzuia demokrasia ya uhuru wa mawazo/kujieleza kwa kuwataka wanaCCM wasiongelee mambo ya taifa lao mpaka vikao rasmi vipitishe,hii sio sahihi hata Wamarekani wanajadili nini maslahi ya nchi yao kuingia kijeshi nchini Libya na jana spika wa Bunge la Marekani Mhe.John A.Boehner amemwandikia Barua Rais wake Mhe.Barrack Obama awajulishe Wamarekani malengo halisi ya kwenda Libya na kwa vipi watapima mafanikio hayo(www.nytimes.com/Boehner presses Obama on Libya Action) maana Majeshi yameingia Libya kwa Azimio la UN na ARAB LEAGUE sio Bunge lao.
3.UVCCM isiige siasa za Afrika kusini kati ANCYL vs ANC au JULIUS MALEMA vs JACOB ZUMA
kwa kufanya hivyo mtavuruga CCM maana vijana ndio tegemeo la CCM,na nyinyi hamtakuwa salama pia.
4.UVCCM Jaribuni kuwa watafiti ili muweze kumshauri m/kiti wa CCM Taifa hasa masuala muhimu nchini kwa vijana yakiwemo (a).Mgawo wa umeme unavyoua Biashara ndogo ndogo(hizi ni ajira za vijana),
(b)Udhaifu wa management ktk vyuo vikuu ulivyokero kwa wanafunzi,(c )Kuongeza "competences" kwa Graduates maana kwa sasa wengine wanahitimu wakiwa bado dhaifu kutokana na mfumuko wa vyuo vikuu nchini,(d).Ombeni mfumko wa bei uwe controlled maana hela ina kosa thamani kama zimbabwe,etc.
Nakutakia kazi njema,
Ndimi
Mussa Mnyeti-0787 330518,
Mwanachama wa UVCCM/CCM.

mjini
 
Karibu kwenye mjadala huu ambao unalenga kujitathimini kwa vijana juu ya heshima yao kwa wazee. Mjadala huu utakuwa unarejea matukio mbali mbali ambayo yamefanywa na vijana.Kuanza na naweka orodha a matukio ya wanasias vijana dhidi ya viongonzi wao.

Nitaanza kwa kutoa mifano:-

1. Mwampamba na Sonza walipokuwa Chadema walikuwa wanatuhumiwa kuwavunjia heshima viongozi (wazee wa chama) wa chama chao mitandaoni....na inasemakama mpaka sasa wanafanya hivyo.

2. Nape wa CCM inasemakana aliwahi kutoa kauli ya kuudhi na kuvunja heshima kwa wazee...kuwa wao wanasubiri kufa tu...!

3. Kijana (sina hakika kama ni mwanasiasa sana) aliwahi kumpiga kibao Mzee Mwinyi(Rais mstaafu) hadharani akipinga maelezo ya Mzee Mwinyi.

4. Vijana wa UVCCM waliwahi pia kuwatukana viongozi wa chama chao pia. Ushahidi huu hapa chini

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uvccm-viongozi-wastaafu-na-hatima-ya-ccm.html

5. Pia na Mbunge wa Arusha Mh. Lema naye inasemekana anawavunjia heshima wazee wa CCM

6. Serukamba Mbunge wa Kigoma aliwatukana wazee kwa vijana waliokuwa bungeni na waliokuwa wanasikiliza kupitia runinga na redio...pale alipotamka tusi kwa lugha a kiingereza.

7. Mh. Lissu aliwahi pia kutamka kuwa ...neno...SILLY....bungeni...hilo pia ni kuwa wavunjia heshima wazee kwa vijana...
8. mweshimiwa waziri Kijana Mkaa wa mia aliwahi kusema anaongea na mwenye mbwa wala haongei na mbwa...huko huko bungeni(kama nimekosea nisahihisheni).

8. Orodha ni ndefu....ila kabla sijahau pia...kuna na suala la Makonda, Paul kumkwida Jaji Warioba.

Sasa kwa matukio haya na mifano mingine....huko mitaani. Vijana tumeangukia/wameangukia wapi mpaka sasa wanasahau umuhimu wa utamaduni wetu watanzania wa kuwaheshimu wazee. Ni nini kifanyike ili kurudisha heshima ya vijana kwa wazee?

Karibu kwenye mjadala.

SOURCE:VIJANA NA HESHIMA KWA WAZEE: Tumebadili utamaduni wetu wa Kitanzania...!?
Sina hakika kama kimefanyika kitu kwa vijana rejesha nidhamu
 
Back
Top Bottom