MGOGORO: Malumbano ya UVCCM, Viongozi wastaafu na Hatima ya CCM

Sitta: UVCCM ina matatizo

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), unateswa na siasa za makundi na kuutaka utumie muda wake mwingi sasa kutatua matatizo yake.

Juzi, Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa alisema umoja huo kupitia mkutano wake wa Baraza Kuu, umeazimia kwamba utahakikisha vigogo ambao wamekuwa wakizungumza nje ya utaratibu wa vikao vya CCM wanatupwa nje ya ulingo wa siasa za chama hicho tawala.

Hata hivyo, akizungumza kwa simu jana akiwa jimboni kwake, Urambo Mashariki, Sitta alisema: "Nadhani wao wenyewe wana matatizo ya kutosha. Sihitaji malumbano kwa sababu sijui shabaha yao lakini ninachoweza kusema ni kwamba wanateswa tu na siasa za makundi."

Spika huyo wa Bunge la Tisa, ambaye amekuwa akipinga hadharani ulipaji Sh94 bilioni kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans, aliitaka UVCCM kurejea misingi iliyorithi kutoka Umoja wa Vijana

wa Tanu (TYL), huku akisisitiza kwamba kinachohitajika sasa si malumbano, bali ni watu kufuata misingi ya uongozi bora, jambo ambalo anaamini kuwa litawezesha hata umoja huo kuwa na vijana safi.

"Sasa tukianza kulumbana hapa tutakuwa tunadhihirisha siasa za makundi. Kwa sababu kuna kauli ambazo ukiziangalia unajua kabisa hizi zinatokana na kuteswa na siasa za makundi tu na hakuna jambo jingine lolote," alisisitiza Sitta.

Alisema uhuru wa kutoa maoni ni mambo ambayo yametajwa ndani ya Katiba ya nchi hivyo, kinachohitajika ni kulinda misingi ya uadilifu ili kuondoa malumbano yanayotokana na msimamo wa kukemea maovu katika chama na Serikali. Sitta ni mwanasiasa wa pili kuzungumzia azimio hilo la UVCCM.

Juzi mara baada ya kutolewa kwa tamko hilo, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alisema anajiandaa kutoa msimamo wake kuhusu kauli hiyo ya UVCCM.
 
Chanzo: Mwananchi
 
Mi nadhan Mh. Sita amesita kidogo. Alitakiwa/alitaka kusema ccm kwa ujumla inamatatizo na inasumbuliwa na siasa za makundi. Ndio maana chama hakina msimamo wala hakishiki hatamu tena. Kuanzia m/kiti hadi wanachama wa kawaida wanalalamika. Wamepoteza mwelekeo na hawajui wachokifanya. Ni mgonjwa aliyepoteza matumaini. Wanangoja tu kuwa chama cha upinzani na hii inakuja very soon!
 
Kumbe hiki ndicho kilio cha sita. Tumekusikia

Napendekeza hayo yote mkayaongee pia ndani ya vikao vya chama ili chama kibaki imara.
 
CCM vipande vipande, raha tupu, ngoja mtoane macho wenyewe kwa wenyewe halafu mje mseme Chadema ndiyo inayowachonganisha, maana mkisha haribu hamkawii kutafuta mchawi, nyama pori nyie.
 
Walisema CDM wanataka kupindua nchi sasa nchi ya kupindua iko wapi???????? wakati nchi haina mtawala CCM hoi, serikali hoi, utajiri wa nchi unaporwa.CDM hawatapindua nchi ila wananchi itabidi wawakabidhi nchi kwani haina kiongozi kwa sasa na wananchi wanhitaji kuongozwa.PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS
 
Sasa SITTA umepiga penyewe kabisa Madogo hao wanajipendekeza kwa kundi flani wakijua likishinda 2015 wao watakuwa wametoka kimaisha, lakini wamesahau kuwa CDM hawajalala na uchaguzi wa 2015 utakuwa kufa na kupona yaani wazalendo wa TZ against Mafisadi wa TZ na wapambe wao. Hivyo wasitegemee mtelemko
 
Mzee Sita, ni miongoni mwa wachache ambao ni "MAPISHI" ya Mwalimu J.K ndio maana unadhubutu kukemea na kuonyesha uozo hadharini. Wengine wote utasikia wanasema tukutane kwenye vikao halali vya chama. Wakifika huko wanawaziba midomo na kukemewa vikali. Hao UVCCM ingekuwa vizuri kama wangeondokana na hayo makundi ili iwe rahisi kwao kutenda majukumu yao bila kuegemea upande wowte.
 
Hawa wanaojiita UVCCM walitakiwa wacharazwe viboko ingekuwa enzi zile za ukoloni maana mambo na hoja zao hazifanani na ya umoja wa chama chochote zaidi ya chama cha mahayawani
 
ccm vipande vipande, raha tupu, ngoja mtoane macho wenyewe kwa wenyewe halafu mje mseme chadema ndiyo inayowachonganisha, maana mkisha haribu hamkawii kutafuta mchawi, nyama pori nyie.

mchawi wa ccm yuko ndani ya ccm! Watamalizana wao kwa wao.
 
..safiiii saaaaaaaana na bado!! Laaana ya watanganyika hiyooo!! Wanafikiri machozi ya watanganyika wanaoumizwa na ufisadi wao yataenda bure?? Kudadadadeki wapi F. Sumaye? Sema tukusikie?? Wapi Mwakyembe? Madogo hao umewasikia?
 
mhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! iko kazi!!!!!! kuvuja kwa pakacha...................
 
Haiwezekani CCM ikawa na makundi kisha UVCCM ikakosa makundi. Wacha wajiue wenyewe maana wanajua kuwa hawatakiwi na People's Power bali wanadumu kwa kuchakachua. Kiyama chao ni 2015 watazikwa. Tushangilie ukombozi uko karibu Mama Tanganyika anarudi.
 
Vita ndani ya CCM sasa ishaanza rasmi hawa vijana hawawezi kuvaa kiatu ya kina Sitta patamu hapo. Kambi ya Sitta ipo fiti subirini mpira unavyoanza kuchezwa. Hawa madogo wamekosea kobonyeza kidude.

CHADEMA we tulia tu ucheki move hiyo...hadi ikifika 2014 majeruhi kibao, then unakokota ngoma kiulainii...
 
Ndani ya uvccm kuna kundi kubwa sana linalounga mkono kambi ya lowassa na kuna kundi dogo linaloongozwa na baadhi
wa wajumbe wa mkoa wa pwani linalomuunga mkono jk. Hakuna namna ambayo baraza kuu la uvccm linaweza kufikia maamuzi ya kufanana. Lowassa na jk hawapikiki chungu kimoja.
 
Sitta: UVCCM ina matatizo

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), unateswa na siasa za makundi na kuutaka utumie muda wake mwingi sasa kutatua matatizo yake.

Juzi, Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa alisema umoja huo kupitia mkutano wake wa Baraza Kuu, umeazimia kwamba utahakikisha vigogo ambao wamekuwa wakizungumza nje ya utaratibu wa vikao vya CCM wanatupwa nje ya ulingo wa siasa za chama hicho tawala.

Hata hivyo, akizungumza kwa simu jana akiwa jimboni kwake, Urambo Mashariki, Sitta alisema: "Nadhani wao wenyewe wana matatizo ya kutosha. Sihitaji malumbano kwa sababu sijui shabaha yao lakini ninachoweza kusema ni kwamba wanateswa tu na siasa za makundi."

Spika huyo wa Bunge la Tisa, ambaye amekuwa akipinga hadharani ulipaji Sh94 bilioni kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans, aliitaka UVCCM kurejea misingi iliyorithi kutoka Umoja wa Vijana

wa Tanu (TYL), huku akisisitiza kwamba kinachohitajika sasa si malumbano, bali ni watu kufuata misingi ya uongozi bora, jambo ambalo anaamini kuwa litawezesha hata umoja huo kuwa na vijana safi.

"Sasa tukianza kulumbana hapa tutakuwa tunadhihirisha siasa za makundi. Kwa sababu kuna kauli ambazo ukiziangalia unajua kabisa hizi zinatokana na kuteswa na siasa za makundi tu na hakuna jambo jingine lolote," alisisitiza Sitta.

Alisema uhuru wa kutoa maoni ni mambo ambayo yametajwa ndani ya Katiba ya nchi hivyo, kinachohitajika ni kulinda misingi ya uadilifu ili kuondoa malumbano yanayotokana na msimamo wa kukemea maovu katika chama na Serikali. Sitta ni mwanasiasa wa pili kuzungumzia azimio hilo la UVCCM.

Juzi mara baada ya kutolewa kwa tamko hilo, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alisema anajiandaa kutoa msimamo wake kuhusu kauli hiyo ya UVCCM.
Haha... its funny the whole bunch of CCM/UVCCM cretins cant beat Sitta... Kazi kubwa wamefanya bure kawamaliza kwa maneno machache...hawa ndio viongozi wa kesho wa CCM hawawezi hata kuja na Idea mpya zaidi ya huyu mzee Sita. Hapa ndipo ninapowapenda vijana wa CHADEMA wao huto version moja tuu..CCM A na CCM B(TL, CUF, NCCR, etc) vichwa vinazunguka.
Sijui wana Budget tena warudi dodoma waka Amend haya maazimio..?
 
Back
Top Bottom